Mjumbe wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Henry Mwimbe (kushoto) akikagua vifaa vya ujenzi wa Umeme vya mradi wa Kampuni ya kusambaza Umeme ya Ccce Co Ltd inayo sambaza umeme vijiji vya Wembere na Ntwike wilayani Iramba mkoani Singida. Kulia ni Wafanyakazi wa kampuni hiyo
Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwashitaki na kuwafilisi wakandarasi watakaoshindwa kumaliza kwa wakati shughuli za usambazaji wa nishati ya umeme kwenye maeneo waliyokabidhiwa ifikapo Juni,30,mwaka huu.
Mjumbe
wa Bodi ya REA, Henry Mwimbe aliyasema hayo alipokuwa akitembelea na
kukagua mradi wa usambazaji nishati ya umeme vijijini katika wilaya ya
Iramba unaotekelezwa na Kampuni ya Ccce Co Ltd kwenye vijiji vya Wembere
na Ntwike wilayani Iramba.
Raia wa China Wafanyakazi wa kampuni hiyo wanao tekeleza mradi huo
Majadiliano kabla ya kwenda kukagua mradi huo
Aidha
Mwimbe alifafanua kwamba kutokana na mkataba walioingia na Makampuni
yanayosambaza nishatai hiyo kwa hali hiyo hawatakuwa na huruma na wala
hawataweza kuongeza muda wa mkataba hata siku moja na badala yake
watazingatia yale waliyokubaliana kwa nujibu wa mkataba waliosaini nao.
“Na
uzuri ndani ya mkataba kunaelezwa majukumu ya kila pande kwenye huo
mkataba na ainaelezwa pia unaposhindwa kutekeleza kile ulichopaswa
kufanya kwa mujibu wa mkataba,nini kinafuata kuna kushitakiwa pale,kuna
kufilisiwa pale.”alisisitizs mjumbe huyo wa Bodi ya Rea.
Transfomer zikiwa eneo la mradi tayari kwa kufungwa
Hata
hivyo Mjumbe huyo wa Bodi ya Rea aliweka wazi pia kwamba kwa mtu mwenye
kampuni ambayo anataka kampuni yake iende mbele kuna akutopewa kazi na
kuongeza kwamba haadhani kama kuna kampuni inawerza kuendelea
kujiendesha bila kazi na mteja wake mkubwa ni serikali kupitia rea
kuwapatia kazi hizo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa REA, Mhandisi Elineema Mkumbo aliweka
wazi kuwa katika mradi huo ambao ni wa tatu mzunguko wa kwanza
unatekelezwa katika mikoa 25 ya Tanzania na lengo lilikuwa ni kupeleka
katika vijiji 3,559.
Mjumbe wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Henry Mwimbe (kulia) akikagua vifaa vya ujenzi wa umeme vya mradi huo
Kwa
mujibu wa Mhandisi Mkumbo mpaka ifikapo Juni,30 mwaka huu vijiji hivyo
3,559 viwe vimepatiwa umeme na kukamilika kwa vijiji hivyo kutakuwa
kumepelekea zaidi ya asilimia 70 ya vijiji vya Tanzania kuwa na
miundombinu ya umeme.
Hata
hivyo wakati awamu ya tano inachukua madaraka mwaka 2016 Tanzania
vijiji 2,018 vya Tanzania ndivyo vilivyokuwa na umeme na hadi kufikia
Aprili,mwaka huu vijiji vilivyokuwa na umeme vilikuwa 9,200.
Nguzo zikiwa eneo la mradi wilayani Iramba
Na Ismailly Luhamba, Singida
Kwa aupande wake Meneja Mradi wa Mradi wa Wakala wa Nishati vijijini (REA) awamu ya tatu,Mhandisi Baraka Mhagama alibainisha kwamba mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 90 na asilimia kumi zilizobakia ni zile ambazo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto mbali mbali.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na usafirishaji wa vifaa na kwamba kama inavyofahamaika sera ya Rais ni kwamba asilimia kubwa ya vifaa vinunuliwe ndani ya nchi.
“Asilimia kubwa ya changamoto ni katika uletaji wa vifaa kama mnavyojua sera ya Rais ni kwamba asilimia kubwa ya vifaa ichukuliwe ndani kwa hiyo kwa wasambazajai wetu wa ndani kidogo uwezo wao ulikuwa sio mzuri hasa kwa nguzo lakini tuliweza kupambana nazo na mwisho wa siku tumezipata za kutosha.” alisema Mhagama.
No comments:
Post a Comment