Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa (wa pili kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Wilaya ya Manyoni, Robert Chalamaganza (kushoto) moja ya mzinga wa nyuki kati ya 20 yenye zaidi ya sh.milioni 1.2 ililiyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka jana kwa ajili ya kuanzisha mradi waufugaji nyuki katika Shule ya Sekondari ya Mkwese. Wengine ni Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Manyoni.
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Manyoni, Leah Gervas (kulia) akimvika skafu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa mara baada ya kuwasili kwa ziara ya siku moja wilayani humo mkoani Singida jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mkoa wa Singida, Mwalimu Ephraim Kolimba.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund
Mndolwa amewataka wanachama wa jumuiya hiyo, kuhakikisha wanakipa
ushindi CCM, wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka
huu.
Mndolwa
alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na wanachama wa jumuiya hiyo
wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida katika ziara yake ya kikazi ya siku
moja.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Manyoni, Ally Omary.
Mwekezaji wa shule hiyo, Askofu Williams Wilson Yindi, akielezea historia fupi ya shule hiyo. |
“Rais
wetu Dkt.John Magufuli amefanya kazi kubwa ya kutuletea maendeleo hivyo
zawadi kubwa ya kumpa ni kuhakikisha tunampa kura nyingi za kutosha
wakiwemo wabunge na madiwani” alisema Mndolwa.
Alisema
kujiandikisha katika daftari la wapiga kura hakutoshi kinachotakiwa ni
siku ikiwadia ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi kuanzia wakina mama,
vijana nawanaume.
Viongozi wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Manyoni wakijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mkoa wa Singida, Mwalimu Ephraim Kolimba (wa pili kuli)
Mkutano ukiendelea.
Katika
ziara hiyo Mndolwa alikabidhi mizinga 20 ya nyuki aliyoitoa Mbunge wa
Jimbo la Manyoni Mashariki Daniel Mtuka kwa ajili ya kuanzisha mradi wa
ufugaji nyuki katika Shule ya Sekondari ya Mkwese yenye thamani ya zaidi
ya sh.milioni 1.2.
Pamoja
na mambo mengine Mndolwa alizindua luninga iliyonunuliwa na mbunge huyo
kwa ajili ya kuangalia wanafunzi wa shule hiyo, lengo likiwa ni
kujifunza vipindi mbalimbali.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wazazi Taifa, Focus Mushi, akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka, akizungumza.
Katibu wa UVCCM, Mkoa wa Singida, George Silindu akizungumza.
Katibu wa CCM Wilaya ya Manyoni, Dafroza Lucas, akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Alexandrina Katabi, akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa, akizungumza.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mkwese wakiwa shuleni wakimsubiri kumpokeea Dkt. Mndolwa.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Dkt. Denis Nyiraha, akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi, Yahaya Masere, akizungumza.
Katika
hatua nyingine Dkt. Mndolwa amemhakikishia Mwekezaji wa shule hiyo,
Askofu Williams Yindi atapewa mkataba wa kuindesha shule hiyo,
inayomilikiwa na jumuiya ya Wazazi.
“Nikuhakikishie
kuwa hadi ifikapo Augosti 15 mwaka huu kama hakutakuwa na hatua yoyote
iliyofikiwa kuhusu mchakato wa kupata mkataba wa uendeshaji wa shule hii
baina yetu na wewe naomba nipigwe risasi ya kichwani” alisema Mndolwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa, akipokea zawadi.
Zawadi ya asali ikipokelewa.
Zawadi ya asali ikipokelewa.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Manyoni, Igembya Wambura, akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa.
Vijana wa UVCCM Wilaya ya Manyoni wakifanya gwaride kabla ya kuvalishwa Skafu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Edmund Mndolwa.
Na DottoMwaibale, Manyoni
Hatua ya Dkt.Mndolwa kutoa agizo hilo ilikuja baada ya mwekezaji wa sekondari hiyo kueleza kuwa ameboresha miundombinu ya shule ambayo ilikuwa imeharika, ikiwa ni pamoja na kuchimba visima vya maji, kuweka umeme, ukarabati wa majengo zikiwemo nyumba za walimu, madarasa, mashine ya kusaga, ununuzi wa vifaa vya kufundishia, kununua vifaa vya maabara na zana zingine.
“Mhe.Mwenyekiti uwekezaji nilioufanya katika shule hii unafika zaidi ya sh.milioni 80 lakini hadi leo hii sina mkataba wowote kati yangu na jumuiya ya wazazi, ambao ndio wamiliki wa shule.” AlisemaYindi.
Yindi aliongeza kuwa waliipokea shule hiyo januari 2019 ikiwanawanafunzi 40 na wafanyakazi 10 hadi kufia Machi, 2019 waliongeza wanafunzi 37 nakufikia 77, huku idadi ya wafanyakazi ikifikia 17, na mwaka huu wameongeza wanafunzi hadi kufikia 103 na wanatarajia kupata wanafunzi wengi zaidi kadri watakavyo zidi kuimarisha miundombinu ya shule na taaluma.
Aidha, Mndolwa aliomba wanachama wa jumuiya hiyo kujenga tabia ya kulipia kadi zao ili fedha zitakazo patikana zisaidie katika shughuliza za uendeshaji wa jumuiya hiyo ambayo haina vyanzo vingi vya mapato.
No comments:
Post a Comment