Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amepongeza
uamuzi wa Hoteli ya Serena wa kufungua hoteli hiyo tangu ilipofungwa kwa
ajili ya kuweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya
Corona.
Amezitoa
pongezi hizo Jijini Dar es Salaam wakati akishiriki hafla ya
kufungua hoteli ya Serena ambayo imekuwa ni muhimu katika kuwahudumia
Watalii wengi wanaotoka na kuingia kutoka Nchi za nje kabla na baada ya
kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Hoteli ya Serena iliyopo Jijini Dar es Salaam baada ya janga la Corona kufuatia kufungwa kwa takribani miezi mitatu ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya ugonjwa huo, Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Godwin Mollel na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pamoja na Wadau wengine wa Utalii.
Amesema
uamuzi huo wakufungua hoteli hiyo unatoa ujumbe mzito Duniani kuwa
Tanzania ipo salama na ipo tayari kwa ajili ya kuwapokea Watalii.
Amesema
kurudi kwa biashara hiyo kunarudisha uhakika wa maisha ya watu
takribani 450,000 ambao wameajiriwa moja kwa moja katika sekta ya
Utalii.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Anthony Mavunde akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu pamoja na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Dkt.Godwin Mollel pamoja na wadau wengine wa Utalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya kufungua Hoteli ya Serena iliyokuwa imefungwa kwa takribani miezi mitatu ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya ugonjwa wa Corona
Amesema
Ugonjwa wa Corona uliiathiri jamii katika nyanja za kiuchumi na
kijamii baada ya watu wengi kupoteza ajira zao na wengine kuachishwa
kazi kutokana na janga hilo
Amesema
uamuzi huo wa Hoteli ya Serena kuifungua hoteli hiyo kunaleta mwanga wa
matumaini kwa Watanzania wanaoitegemea Sekta ya Utalii katika kuendesha
maisha yao.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza
wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es
Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi
vya Corona
"
Ninawashukuru Hoteli ya Serena kwa kupeleka ujumbe kwa Wawekezaji wetu
wote ambao wanaogopa na kufunga biashara zao kwa ajili ya Ugonjwa huo.
Hata
hivyo ametoa wito kwa jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya
ugonjwa wa Virusi vya Corona na kuwa ugonjwa huo bado upo lakini
hauwezi kukimbiwa ni lazima tujifunze kuishi nao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona
"
Tunamshukuru sana Rais, Mhe.John Pombe Magufuli kwa kufanya maamuzi ya
kufungua anga ambapo tunaamini biashara ya Utalii na biashara ya anga
zinategemeana kwa kiasi kikubwa.
Amesema
uamuzi huo umeifanya biashara ya utalii kuweza kurejea kwa vile tayari
mashirika ya ndege ya Ethiopia, Emirates, KLM na Quatar yameanza kuja
nchini.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Dkt. Goldwin Mollel akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa virusi vya Corona
Naye,
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto, Dkt.
Goldwin Mollel amewataka Wadau wa Sekta ya Utalii ikiwemo Wamiliki wa
Hoteli kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Wizara
yake ili kuhakikisha usalama wa Wageni na wenyeji wanaowahudumia Watalii
Akizungumzia
uamuzi huo wa kuifungua hoteli hiyo amesema inatuma ujumbe kwa
Wawekezaji wengine kuwa Tanzania ipo salama kwa i na Watanzani wapo
tayari kwenda nchi za nje kwa ajili ya kutafuta shughuli za kibiashra.
Naibu Waziri wa
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Anthony
Mavunde akizungumza wakati wa hafla ya kufungua rasmi Hoteli ya Serena
ya jijini Dar es Salaam iliyokuwa imefungwa ili kuweza kukabiliana na
mlipuko wa virusi vya Corona
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu, Thomas
Mihayo amesema tangu anga lilipofunguliwa kumeonesha dalili njema ya
ujio wa idadi kubwa ya watalii
"
Kuna matumaini makubwa ya kupata watalii wengi zaidi kwa mfano siku ya
jana ndege ya Shirika la KLM ilitua Uwanjaa wa ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro ( KIA) ikiwa na kabiria 200 kati ya hao 45 ni watalii
waliokuja nchini kwa ajili ya kutalii" alisema Jaji Mstaafu Mihayo.
Amesema
hiyo ni dalili njema katika sekta ya Utalii nchini, " Miezi mitatu
iliyopita tulikuwa hatupokei watalii kabisa kwa hofu ya janga la Corona.
No comments:
Post a Comment