Matokeo chanyA+ online




Thursday, July 9, 2020

RAIS. DKTMAGUFULI, MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU WAFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU BALOZI MSTAAFU JOB LUSINDE KUTOA POLE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafiwa nyumbani kwa Marehemu Balozi Job Lusinde Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wafiwa nyumbani kwa kwa Marehemu Balozi Job Lusinde Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mke wa Marehemu Balozi Job Lusinde, Mama Sara Lusinde aliyekaa katikati mwenye kilemba cheupe mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kutoa pole nyumbani kwa Marehemu Balozi Lusinde Uzunguni jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Msemaji wa Familia ya Marehemu Balozi Job Lusinde, Waziri Mkuu Mstaafu John Samweli Malecela wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Marehemu Balozi Lusinde Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika kwenye kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere Marehemu Balozi Job Lusinde aliyefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Msemaji wa Familia ya Marehemu Balozi Lusinde, Waziri Mkuu Mstaafu John Samwel Malecela mara baada ya kutoa pole Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika kwenye kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere Marehemu Balozi Job Lusinde aliyefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya kifo cha Marehemu Balozi  Job Lusinde nyumbani kwa marehemu Uzunguni  Jijini Dodoma leo Julai 09,2020 alipofika kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya marehemu mzee Job Lusinde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mjane wa marehemu Mzee Job Lusinde Bibi Sarah J. Lusinde alipofika nyumbani kwa marehemu Uzunguni Jijini Dodoma leo Julai 09,2020 kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya marehemu mzee Job Lusinde.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mjane wa marehemu Mzee Job Lusinde Bibi Sarah J. Lusinde alipofika nyumbani kwa marehemu Uzunguni Jijini Dodoma leo Julai 09,2020 kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya marehemu mzee Job Lusinde.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Julai, 9. 2020, amehani msiba wa Mwanasiasa Mkongwe nchini, Balozi Job Lusinde.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Msemaji wa Familia ya Marehemu Balozi Lusinde, Waziri Mkuu Mstaafu John Samwel Malecela mara baada ya kutoa pole Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri)
Rais  Dkt. John  Magufuli leo tarehe 09 Julai, 2020 amekwenda kutoa pole kwa familia ya Balozi Mstaafu Job Lusinde aliyefariki dunia tarehe 07 Julai, 2020.

Msiba wa Balozi Mstaafu Lusinde upo nyumbani kwake Kilimani Jijini Dodoma.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekwenda nyumbani hapo akitokea Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambako ameongoza Kikao cha Kamati ya Maadili na Usalama na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM.

Akiwa nyumbani kwa Marehemu Balozi Mstaafu Lusinde, Rais Magufuli amekutana na Mjane wa Marehemu Bi. Sara Lusinde, ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu ambapo ameeleza kuwa kuguswa na kifo cha Balozi Mstaafu Lusinde na kwamba daima atamkumbuka kwa mchango wake alioutoa akiwa Waziri wa Ujenzi, ushauri wake mzuri na moyo wake wa upendo na ukweli.

Rais Magufuli ameeleza kuwa wakati wa utumishi wake Balozi Mstaafu Lusinde alikuwa mzalendo wa kweli, mchapakazi na aliyetetea maslahi ya Tanzania nchi ya nchi, na kwamba hata alipostaafu aliisemea vizuri Dodoma.

Amewataka wafiwa wote kuwa wastahimilivu na kumpuzisha salama hapo kesho tarehe 10 Julai, 2020 atakapozikwa.
Viongozi wengine waliofika kutoa pole ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 

No comments:

Post a Comment