Wananchi wa Kijiji cha Mgazi wilayani Igunga mkoani Tabora wakichota maji katika bomba la mradi wa maji waliopelekewa na Shirika lisilo la kiselika la Kusaidia na Kuhamasisha Maendeleo (DESPO) kwa Ufadhili
wa Mfuko wa Ushirikiano wa Tanzania na Japan uitwao (Tanzania/ Japan Food Aid
Counterpart Fund) wakati wa hafla ya kukabidhiwa mradi huo iliyofanyika jana.
Mkazi wa Kijiji cha Mgazi, Hawa Igunda akitoka kuchota maji kwenye bomba la mradi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli.
Bwawa la maji lililochimbwa na Shirika lisilo la kiselika la Kusaidia na Kuhamasisha Maendeleo (DESPO)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja, viongozi wa DESPO na Wananchi wa Kijiji cha Mgazi baada ya kulikagua bwawa hilo.Mwenyekiti wa Bodi wa DESPO, Stanley Kayabu, akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa bwawa hilo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiselika la Kusaidia na Kuhamasisha Maendeleo (DESPO) , Fedes Mdala (kulia) akimueleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Revocatus Kuuli (kushoto) wakati akikagua mradi wa Maji wa Kijiji cha Mgazi kabla ya kukabidhiwa juzi kwa Wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiselika la Kusaidia na Kuhamasisha Maendeleo (DESPO) , Fedes Mdala (mbele) akiongoza msafara wakati wa ukaguzi wa mradi huo.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja, viongozi wa DESPO na Wananchi wa Kijiji cha Mgazi baada ya kulikagua bwawa hilo.
Ng'ombe wakinywa maji kwenye birika lililotengenezwa na DESPO.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, Akisalimiana na Mfugaji Unga Pangalijah ambaye alipeleka mifugo yake kunywa maji katika birika hilo.
Hapa wakiangalia bomba linalopeleka maji Kijiji cha Mgazi kutoka katika bwawa hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, akikabidhiwa ndoo ya nyanya alizopewa kutoka moja ya bustani iliyoanzishwa pembezoni ya bwawa hilo ambalo limeongeza fursa ya kilimo kwa wananchi wa Kijiji cha Mgazi.
Hiki ndicho kisima kilicho kuwa kikitumiwa na wananchi wa kijiji hicho kwa ajili ya kupata maji ya matumizi ya nyumbani na mifugo kabla ya kupelekewa mradi huo na DESPO.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgazi, Thomas Kijjah akizungumza kwenye hafla hiyo.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, akizungumza na wananchi kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgazi, Thomas Kijjah akisaini mkataba wa makabidhiano wa mradi huo. Mkataba huo ulisainiwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, Mkurugenzi Mtendaji wa DESPO, Fedes Mdala na Meneje wa RUWASA, Christopher Saguda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja, viongozi wa DESPO na Wananchi wa Kijiji cha Mgazi katika hafla hiyo.
Wakina mama wakitoka kuchota maji katika bomba la mradi huo.
Meneje wa RUWASA, Wilaya ya Igunga, Christopher Saguda akizungumza kwenye hafla hiyo.Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji cha Mgazi, Abby Gajabi, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, akimkadhi, Mwenyekiti wa mradi huo, Makaranga Twiri, Cheti cha Usajili wa Jumuiya ya Watumiaji Maji (CBWSO) wa kijiji hicho.
Mkazi wa Kijiji cha Mgazi akilishukuru shirika hilo, kwa kuwapelekea mradi huo.
Mwenyekiti wa mradi huo, Makaranga Twiri, akizungumzia faida za mradi huo.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja, viongozi wa DESPO na Wananchi wa Kijiji cha Mgazi.
Na Dotto Mwaibale, Igunga
Wananchi wa Kijiji cha Mgazi kilichopo Igunga mkoani Tabora wameondoka na kero ya muda mrefu ya kupata maji baada Shirika lisilo la kiselika la Kusaidia na Kuhamasisha Maendeleo (DESPO) lenye makao yake makuu Mkoa wa Tabora kufanikiwa kuwachimbia bwawa na kupeleka maji katika kijiji hicho.
Mafanikio ya kazi hiyo ya kupeleka maji katika kijiji hicho yametokana na ushirikiano mkubwa baina ya shirika hilo, wananchi wa Kijiji cha Mgazi na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa Ufadhili wa Mfuko wa Ushirikiano wa Tanzania na Japan uitwao (Tanzania/ Japan Food Aid Counterpart Fund) .
Akizungumza jana katika hafla ya kukabidhi mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Fedes Mdala alisema mradi huo umechukua miaka mitatu hadi kukamilika.
Mdala alisema Julai 27, 2013 shirika hilo lilipokea barua kutoka ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Mgazi ikiomba mradi wa kuchimbiwa bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya mifugo.
Alisema katika barua hiyo, ilielezwa kuwa ifikapo mwezi wa nane visima vilivyopo hukauka na wananchi kulazilimika kutembea umbali wa hadi kilometa 12 kwa ajili ya kupata maji na wakati mwingine kulikuwepo na magonjwa ya mlipuka kutokana na ukosefu maji ya kutumia majumbani na pia kumekuwepo na kesi za kubakwa wanawake na magomvi ndani ya ndoa kutokana na muda mwingi ambao wamama wamekuwa wakitumia kwenda kutafuta maji.
Mdala alisema kutokana na hali hiyo Halmashauri ya Wilaya pamoja na Mbunge walifanya jitihada za kutafuta suruhisho la changamoto ya maji lakini kutokana na ufinyu wa bajeti jambo hilo halikuwa limewezekana.
"Kwa shida iliyokuwepo wananchi walichangishana fedha kwa ajili ya kuanzisha mradi wa maji hadi kiasi cha Tsh 750,000/= lakini kwa bahati mbaya haikuwezekana" alisema Mdala.
Alisema baada ya kupokea barua hiyo uongozi wa DESPO uliketi na kutathmini ombi hilo, na baadaye timu ya wataalam walifika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa ajili ya kujirizisha zaidi juu ya changamoto iliyoripotiwa na Kijiji cha Mgazi.
Alisema Ofsi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ilitoa ushirikiano mkubwa kwa kuteua mtumishi mmoja ambaye aliongoza timu ya wataalam hao kutoka DESPO kwenda Kijiji cha Mgazi kwa ajili ya kukutana na uongozi wa kijiji na kujionea hali halisi ya tatizo la maji.
Alisema katika ziara hiyo iliyofanyika mwezi Oktoba 2013, timu ya wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga na DESPO ilifanya kikao na Viongozi wa Serikali ya Kijiji kujadili changamoto ya uhaba wa maji kwa matumizi ya mifugo pamoja na binadamu katika kijiji hicho.
"Timu hiyo ilifanikiwa kuona vyanzo vilivyokuwa vinatumiwa kwa ajili ya kupata maji na ukweli hali ile ilisikitisha sana kuona wapo binadamu ambao hadi karne hii tena kwenye zama hizi wanaweza kutumia maji yaliyochanganyika na udongo tena yanapatikana kwa shida" alisema Mdala.
Alisema baada ya hapo mchakato wa kuanza ujenzi wa mradi huo ulianza huku Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ikiwa mstari wa mbele katika kuhakikisha shughuli zote za mradi zinakamilika kwa kiwango kilicho kusudiwa kwa kutoa usafiri, wataalamu, na wasimamizi wa mradi.
Akizungumzia ushiriki katika mradi huo Ofisi ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Igunga, alisema imekuwa mstari wa mbele kwa kuhakikisha umoja wa watumiaji maji wa Mgazi unakamilika na kusajiliwa. Lakini pia Meneje wa RUWASA, Christopher Saguda, ambaye kwa bahati nzuri ndiye alikuwa Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kabla ya kuteuliwa nafasi aliyonayo kwa sasa, ameshiriki kwa sehemu kubwa katika ufuatiliaji na ufanikishaji wa mradi huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, alilipongeza shirika hilo kwa kukamilisha mradi huo na kuomba kupeleka mradi mwingine katika wilaya hiyo.
"Nawaombeni mtuletee mradi mwingine na mradi mlioukamilisha utakuwa wa mfano katika wilaya yetu na mikoa mingine hongereni sana" alisema Kuuli.
Kuuli aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuutunza mradi huo na kuwa mtu atakaye bainika kuuhujumu hawata muonea huruma.
Katika hatua nyingine Kuuli aliwaomba wananchi hao kuyachemsha maji hayo kabla ya kunywa ili kujikinga na maradhi ya matumbo.
No comments:
Post a Comment