Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametimiza
ahadi ya kutoa vyerehani 10 kwa wanafunzi waliohitimu mafunzo ya
ushonaji kutoka Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Mpanda
wanaotoka katika mazingira magumu.
Akizungumza katika halfa hiyo
Mkoani Katavi, Profesa Ndalichako amesema ahadi hiyo aliitoa mwaka
2018 baada ya kuwakuta vijana wadogo wamemaliza masomo ya darasa la saba
na kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari na kujiunga na mafunzo
ya ushonaji katika chuo hicho kupitia msaada wa kanisa
No comments:
Post a Comment