Matokeo chanyA+ online




Wednesday, July 8, 2020

WIZARA YA ELIMU KUENDELEZA UBUNIFU WA WASHIRIKI 70



Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetenga zaidi ya Shilingi milioni 870 kwa ajili ya kuendeleza ubunifu wa washiriki 70 wa Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2020.



Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi 21, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. William Ole Nasha amesema Wizara kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wabunifu wachanga kwa kuanzisha kumbi za atamizi za ubunifu mpya 17 zilizowezesha kuanzishwa kwa makampuni machanga 94 yanayolenga kutatua changamoto katika jamii.


Amesema makampuni hayo yamezalisha ajira rasmi kwa wananchi takribani 600 na zisizo rasmi 15,000.

No comments:

Post a Comment