Mkuu
wa Wilaya Kibiti Mkoa wa Pwani Gulamhussein Shaban Kifu wa pili (kulia)
wakishirikiana kukata utepe na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya (TPB)
Plc Sabasaba Moshingi (katikati), kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Deo
Kwiyukwa, wakishirikiana uzinduzi wa madarasa mawili na madawati na
ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kilale iliopo Ikwiriri Mkoani
Pwani, anaoshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hio, Zainabu Ndole,
(kushoto) na wengine wafanyakazi wa benki hio. Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Majanga (RISK), Moses Manyatta.
Mkuu
wa Wilaya Kibiti Mkoa wa Pwani Gulamhussein Shaban Kifu, (mbele)
wakishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya (TPB) Plc Sabasaba
Moshingi kukata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa mawili na madawati
na ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Kilale iliopo Ikwiriri Mkoani
Pwani, wengine wanao shuhudia ni baadhi ya walimu na wafanyakazi wa
benki hio .
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya (TPB) Sabasaba Moshingi wakati wa sherehe za
kukabidhi madarasa mawili na ofisi za walimu, katika Shule ya Msingi
Kilale Ikwiriri mkoani Pwani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya (TPB) Sabasaba Moshingi(kulia) akifurahia jambo
na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani Mkuu wa Wilaya Kibiti
Gulamhussein Shaban Kifu katika sherehe za kukabidhi madarasa mawili na
ofisi za walimu, katika Shule ya Msingi Kilale Ikwiriri mkoani Pwani.
Na Mwandishi Wetu, Kibiti
Benki ya TPB imekabidhi madarasa mawili, ofisi ya walimu, madawati 50 na
samani za ofisi katika Shule ya Msingi Kikale iliyopo Wilaya ya Kibiti
mkoani Pwani.
Mradi
uliogharamu fedha Sh.milioni 57.8 na ulikabidhiwa kwa uongozi wa shule
na Mkuu wa Wilaya Kibiti Gulamhussein Shaban Kifu aliyeambatana na
viongozi mbalimbali wa Kibiti.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw.
Sabasaba Moshingi alisema benki hiyo ilianza mradi huo baada ya kupokea
maombi kutoka shuleni hapo yakieleza changamoto ya majengo kwa ajili ya
wanafunzi katika shule hiyo yenye wanafunzi takribani 327.
"Tunafahamu
shule hii ni kongwe sana, na kwa kipindi cha muda mrefu ilikuwa
ikikabiriwa na changamoto ya madarasa,"amesema Sabasaba na kuongeza
"Benki yetu ni miongoni mwa wadau wakubwa wa elimu nchini, na ni jukumu
letu kusadia shule hizi zilizopo pembezoni ili nao pia wapate elimu
katika mazingira bora na salama.
"Kama
tulivosikia awali mradi wote umegharimu Shilingi milioni 57 na laki 8,
ambacho ni kiasi benki imetoa kutoka katika faida yake ambayo inapata
kila mwaka."
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya Kibiti Gulamhussein Shaban Kifu ameupongeza
uongozi wa benki ya TPB kwa majengo mazuri ya madarasa na ofisi katika
shule ya msingi Kikale.
"Nina
amini benki hii inapokea maombi mengi sana kwa mwaka kwa ajili ya
kusaidia jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, ila Kikale mmekuwa
miongoni kwa shule zenye bahati kwa mwaka huu kupata msaada huu kutoka
TPB.
"Tunaahidi
kuwa Wilaya ya Kibiti itakuwa bega kwa bega na benki hii katika
kuhakikisha wananchi wa Kikale na Kibiti kwa ujumla wanapata huduma za
kibenki kupitia benki hii,"amesema Kifu.
No comments:
Post a Comment