Matokeo chanyA+ online




Sunday, October 11, 2020

MAJALIWA: MAFUNDISHO YA DINI YANACHANGIA AMANI NCHINI


Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amesema mchango wa viongozi wa dini  Nchini bado unahitajika katika kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano katika jamii.

Akizungumza baada ya kufungua msikiti wa Rahman uliopo katika kijiji cha Kwamndolwa wilayani Korogwe mkoani Tanga, Waziri Mkuu Majaliwa amesema mafundisho ya viongozi wa dini katika jamii yana nafasi muhimu katika kuendeleza amani nchini.

Pia amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuwafundisha Watoto wao mafundisho mbalimbali ya dini ili wawe raia wenye  hofu ya MUNGU.


Kwa upande wake Mufti wa Tanzania SHEIKH ABOUBAKAR ZUBEIR BIN ALLY  ametoa wito kwa Masheikh na Viongozi wa dini nchini kuendelea kuweka msisitizo juu ya amani ya nchi.

Msikiti huo umejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya AL FIRDAUSI ambayo imekuwa ikijenga misikiti, madrasa, kutoa misaada pamoja na kuchimba visima kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Ufunguzi huo wa Msikiti, umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, viongozi wa serikali akiwemo  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Kasongwa pamoja na wakazi wa Kwamndolwa.


No comments:

Post a Comment