Mwenyekiti
wa Jumuia ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma, kumshukuru Mungu
kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa amani na utulivu. Kushoto ni
Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Askofu Oswald Mlay na Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Askofu Evance Chande. PICHA NA RICHARD
MWAIKENDA
Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma.
Mwenyekiti
wa Tume ya Maridhiano Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salumu amewasihi
watanzania kuendelea kumshukuru Mungu kwa wema aliowatendea baada ya
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kufanyika kwa salama na amani.
Ameyazungumza
hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, akiwa
pamoja na wajumbe wa tume ya kitaifa ya maridhiano na wa mkoa wa Dodoma.
Aidha,
Sheikh Alhad Mussa amesema kuwa inatakiwa sasa baada ya uchaguzi
kumalizika salama ni kuungana kuendelea kuiombea kwa Mungu serikali
iliyoshinda iongoze vema.
"Tunashukuru
Mungu Uchaguzi umeisha kwa amani na salama, kilicho mbele yetu ni
kuungana kuendelea kuiombea Mungu Serikali iliyopo madarakani ituongoze
salama.
Katika
chaguzi zote kuna kushinda na kushindwa, huwezi kukubalika na kila
mmoja haiwezekani, manabii wa Mwenyezi Mungu na hata Wacha Mungu
hawakukubalika nao walipingwa, hii ni desturi ni jambo la
kawaida,"amesema Sheikh Alhad.
Ameshauri
upande ambao haujaridhika usisababishe vurugu, bali ufuate taratibu
zilizopo ikiwemo ya kisheria na hata jumuia hiyo inaweza kuweka mambo
sawa.
"Kubwa
tunawaomba Watanzania Nchi yetu iendelee kuwa salama na utulivu,
tunahitaji nchi yenye amani ili tuweze kufanya shughuli zetu kwa
ukamilifu bila bughudha yoyote, tusijaribu kuchezea amani iliyopo,
tutajuta, tuna mifano mingi ya nchi mbalimbali zilizochezea amani,
kuirejesha ni ngumu sana."
Amesema
viongozi wa Dini walimlilia sana Mungu ili Uchaguzi uvuke kwa salama na
amani, hivyo inabidi kumshukuru Mungu kwa wema wake aliotutendea. na
kwamba wakifanya hivyo Mungu atatuzidishia.
Alimalizia
kwa kutoa shukrani kwa viongozi wote walioiombea kwa Mungu nchi wakati
wa mlipuko wa ugonjwa wa corona na Uchaguzi Mkuu na sasa iko salama
hivyo tuendelee kumshukuru Mungu naye ataendelea kutusikiliza.
No comments:
Post a Comment