Mapema RC Kunenge akiongozana na wajumbe wa
kamati ya usalama ya Mkoa wamefika Katika eneo hilo na kushuhudia uwepo
tope linalotoka ardhini na kupanda Katika uso wa ardhi jambo
lililosababisha baadhi ya nyumba kutitia, kupasuka nyufa na mifugo
kutitia jambo lililosababisha taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.
Kutokana
na hali hiyo RC Kunenge amemuelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kinondoni kuweka alama za hatari Katika eneo hilo wakati Serikali chini
ya taasisi ya Geologia na utafiti wa Madini Tanzania ukiendelea kupia
ukubwa wa eneo lililoathirika.
Pamoja na hayo RC Kunenge amesema
Serikali inaangalia utaratibu wa kuwapatia wananchi wa eneo hilo Viwanja
vingine ili waweze kuendelea na maisha kama awali.
Kwa upande
wake Mtafiti kutoka taasisi ya Geologia na utafiti wa Madini Bwana
Gabriel Mbogoni amesema matokeo awali wamebaini chanzo Cha tope hilo ni
mgandamizo uliosababishwa na uwiano wa maji na chembechembe za udongo
kuharibika na kusababisha tope ambalo linasukumwa kutoka chini kwenda
kwenye uso wa ardhi.
Aidha Bwana Mbogoni amesisitiza kuwa tope
hilo wamelipima na kukuta likiwa na joto la kawaida hivyo halina
uhusiano wowote na ile volcano inayorusha majivu na Moto utokanao na
miamba iliyoiva hivyo eneo hilo kwa Sasa ni tete na halifai kwa shughuli
za Ujenzi Wala makazi.
Sunday, November 22, 2020
RC KUNENGE AWAELEKEZA WAKAZI WA KUNDUCHI MTONGANI AMBAO NYUMBA ZAO ZIMEHARIBIWA NA "VOLCANO YA TOPE" LINALOTOKA ARDHINI KUHAMA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Aboubakar Kunenge amewaelekeza baadhi ya Wakazi wa eneo la Kunduchi
Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na ujiuji wa volcano ya tope
linalofuka kutoka ardhini kuhama Mara moja ili kujikinga na maafa wakati
Serikali inaendelea kufanya utafiti wa kujua ukubwa wa eneo
lililoathirika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment