Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Barabara ya mkoa huo, Dk. Binilith Mahenge akiongoza kikao cha Bodi ya Barabara
ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe walipata taarifa za maendeleo ya
ujenzi wa barabara mkoani humo kutoka Tanroad na Tarura Desemba 16, 2020
jijini Dodoma.
Dk. Mahenge amezitaka Tarura na Tanroads kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika kwa kupata maoni na ushauri wao kabla ya kuanza ujenzi wa barabara na madaraja katika maeneo yao ili kujenga miradi imara inayozingatia jiongrafia na historia ya eneo husika.
Mhandisi wa Barabara wa Tanroads, Clement Ngirwa akielezea
katika kikao hicho, kuhusu utaratibu wa kupandisha hadhi barabara na majukumu ya
Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara katika Hadhi Stashiki.
Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde akichangia hoja akitaka
uwepo utaratibu wa barabara za jamii nazo kutengea fedha kwa ajili ya
matengenezo.
Mbunge wa Kondoa Vijijini, Dk. Ashatu Kijaji akichangia hoja wakati wa kikao hicho kwa
kuzitaka Tarura na Tanroads kuwa na watalaamu wenye ueledi ili waweze kujenga
miradi imara kuiiko wanaojenga miradi ya barabara na madaraja dhaifu ambayo
mvua ikinyesha inabomoka kirahisi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi hiyo, Sambala
Said
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment