Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan
Abbasi, ametangaza kuwa kutokana na urithi mkubwa wa sanaa uliopo nchini
ikiwemo muziki, filamu, ngoma na uga mwingine, sekta hiyo inapaswa
kuhakikisha inaiburudisha jamii yetu ya wachapakazi ipasavyo na kwa
kuanzia Serikali kwa kushirikiana na wadau itaratibu Tamasha kubwa la
aina yake la Muziki na Sanaa litakalotumia jina la moja ya vivutio
vikubwa vya utalii hapa nchini. Adha, amesema kuanzia mwakani Serikali
pia itashirikiana na wadau kurejesha tuzo za muziki na sekta nyingine za
Wizara hiyo.
"Moja ya kazi kubwa ya sekta ya sanaa nchini ni
kuhakikisha jamii yetu inayochapa kazi sana kwa sasa inaburudika
ipasavyo, sasa naona sanaa inakuja tu pale panapokuwepo mdhamini au
mwandaaji fulani asipokuwepo hakuna matukio na nchi iko kimya.
"Wasanii wakoungana watajaza Uwanja. Twende Tutateremsha wasanii wetu wote ambao ni urithi wa sasa na baadaye wa nchi hii halafu tuone kama watu hawatakuja," alisema Dkt. Abbasi akiwa katika siku ya tatu ya kukutana na wadau wa sanaa kwa kukutana na wasanii wa Bongo Movie.
No comments:
Post a Comment