Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kaskazini Unguja,Angelina Adamu
Malembeka amesema kuna umuhimu wa masheha wa mkoa huo kupatiwa vitendea
kazi ili kurahisisha kazi zao katika maeneo yao ya kazi.
Kauli
hiyo ameitoa jana wakati akikakabidhi pikipiki 12 kwa masheha wa shehia
za mkoa huo zenye thamani ya sh.milioni 26 ambapo alisema pikipiki hizo
zitawarahisishia kazi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi
pikipiki hizo Mbunge huyo alisema kuwa kitendo cha utoaji wa pikipiki
umekuja baada ya kuona changamoto zilizojitokeza kipindi cha kampeni
katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema katika kipindi hicho
cha kampeni masheha hao walikuwa hawana taarifa rasmi kutokana na kuwa
kila mara taarifa zinabadilika na ndipo alipoona haja ya kuwapatia
vitendea kazi hizo ili kuwawezesha kuzunguka kwenye maeneo yao yote ili
kuwa na taarifa rasmi.
Mbunge huyo alisema pikipiki hizo
zimetolewa kwa wilaya ambapo pikipiki tano zilitolewa kwa masheha wa
wilaya ya Kaskazini 'A' na wilaya ya Kaskazini 'B' katika mkoa huo wa
Kaskazini Unguja kutokana na kuwa maeneo yao ni makubwa na hawana
vitendea kazi.
"Tunapohitaji taarifa zinazohusu shehia zao huwa
zinachelewa au zimekuja bila ya uhalisia hivyo mategemeo yetu pikipiki
hichi zitatufanya tupate taarifa kwa wakati," alisema
Alisema
pikipiki hizo zitawapa nafasi za kufanya kazi na kupeleka kupata taarifa
kwa wakati sambamba na kujenga mahusiano haina ya viongozi wa Chama na
serikali.
"Masheha ni viongozi wa Serikali hivyo kutaweza
kuwasaidia wananchi kwa ukaribu zaidi kwani masheha ni viongozi wa
Serikali nasi tunawasaidia katika kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,"
alisema
Hata hivyo, aliwataka masheha hao kuzitumia kwa uangalifu
kwa kuvaa kofia ngumu 'helmenti' na kuendesha kwa mwendo wa kawaida ili
kuweza kuepusha ajali zilizokuwa si za lazima pamoja na kufuata sheria
za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Naye,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa
Kaskazini Unguja, Maryam Muharami Shomari, alisema kutolewa kwa pikipiki
hizo, zinaonyesha wazi kuwa Mbunge huyo anatambua umuhimu wa masheha
kutokana na kumekuwepo kwa umuhimu wa sheha katika kufanya kazi zao kwa
umakini.
Pia, aliwataka Wabunge wengine kuendeleza aliyoyaanza
Mbunge huyo ili kuweza kukamilisha idadi ya masheha waliokuwepo katika
Mkoa huo kupata vitendea kazi katika Mkoa na wilaya zao.
Naye
sheha wa shehia ya Matemwe, Vuai Faraji Mcha, alisema amefarijika
kupatiwa pikipiki hizo na kwamba kuahidi kuitumia pikipiki hizo kuwa
lengo lilokusudiwa ili kuona hali ya kiutendaji inakwenda kama
ilivyopangwa pamoja na kumuahidi mbunge huyo kufanya kazi kwa lengo la
kupatiwa.
No comments:
Post a Comment