Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof, Kitila Mkumbo amesema Tanzania itendelea
kushirikiana na India katika kuhakikisha mazingira bora ya kibiashara
kwa wafanyabiashara pamoja na kuendeleza za uhusiano wa kidplomasia
kijamii na kiuchumi katika nchi hizo.
Prof Mkumbo ameyasema hayo
alipokuwa akishiriki katika mkutano kibiashara kwa njia ya mtandao
kati ya India na Tanzania uliofanyika katika ofisi za Wizara zilizopo
Mtumba jijini Dodoma.
Mkutano huo umelenga kujadiliana kuhusu
fursa za biashara zilizopo, kuimarisha ushirikiano wa kibiashara,
kubadilishana uzoefu na kuonyesha maeneo muhimu ya biashara kati ya
India na Tanzania.
Akiongea katika kikao hicho kilichohudhuriwa
na Balozi wa India nchini Tanzania na Balozi wa Tanzania nchini India,
pamoja na wenyeviti wa wafanyabiashara katika nchi hizo, Waziri Prof
Mkumbo amewashauri wawekezaji kutoka India kuwa wakiwekeza Tanzania
wataweza kuuza bidhaa na huduma zao katika nchi za Afrika Mashariki
(EAC) na nchi za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika(SADC) bila
ushuru wa forodha na ukomo wa kiwango cha bidhaa kama ilivyo kwa kwa
wafanyabiashara wa Tanzania.
Akiwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza
Tanzania, amesema kuwa Tanzania ni mwananchama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) yenye ukubwa wa soko lenye idadi ya watu wasiopungua
milioni 177. Pia Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Maendelea Kusini
mwa Afrika yenye ukubwa wa soko lenye idadi ya watu zaidi milioni
300. Vilevile Tanzania iko katika hatua za mwisho za kukamilisha
majadiliano ya uanzishaji wa Eneo huru la Biashara Afrika litakalokuwa
na ukubwa wa soko lenye idadi ya watu isiyopungua bilioni 1.5.
“Hivyo,
kwa kuzingatia jinsi India ilivyoendelea katika Sekta ya Viwanda na
Biashara, nawahimiza wafanyabiashara wa India kuja hususani wenye
Viwanda kuja kuwekeza katika maeneo ya fursa zilizopo Tanzania hasa
katika uongezaji wa thamani wa mazao ya kilimo, ngozi na madini”.
Aidha,
Prof Mkumbo alizisihi taasisi za Serikali Tanzania na India kufanyia
kazi vikwazo vya kibiashara hususan vikwazo visivyo vya kiushuru (non-
tariff barriers) ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa na huduma baina
ya nchi hizo huku wakizingatia ushindani katika biashara. Pi aliainisha
kuwa kwa sasa Tanzania inatekeleza Mpango wa “Blue Print” unaolenga
kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia biashara na uwekezaji.
“
Nafikiri hatutakubaliana kuwa mazao ya kilimo kutoka Tanzania kama
viungo, mbaazi za kijani, korosho na ufuta ambavyo vinahitajika zaidi
India lakini havina soko la kuaminiaka," Amesema Prof Mkumbo.
Vilevile, Waziri amesema ili kutimiza azma hiyo ya kuendeleza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo, Serikali ya Tanzania na India imeanzisha Tume ya pamoja ya Biashara ( Joint Trade Commission (JTC)) inayokutana mara moja ambapo mkutano wa JTC unatarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment