Mchengerwa ameyasema hayo Aprili 19,221 wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo ambapo amesema
taasisi zote hapa nchini ambazo zina watumishi wa umma wajipange,
watenge bajeti zao kuhakikisha kwamba wanapita kwenye taasisi hii ili
tuweze kupikana zaidi.
"Na wale ambao tunaamini wanaweza
kutusaidia, tuwatumie. Tunao Wakuu wa Mikoa ambao wana uzoefu zaidi,
waiteni na kuwatumia ili kuendelea kutoa elimu. Wakuu wa Mikoa na Wilaya
ambao ni vijana na pengine wanadhani wao wakishateuliwa ndiyo
wameshamaliza, kwamba hakuna mamlaka ya kuwachunguza na kuwafuatilia, ni
lazima tuzingatie sana,” amesema Waziri huyo.
Aidha, Waziri
Mchengerwa ametoa msisitizo kuhusu suala la utendaji kazi kwa wizara,
idara na taasisi zote za serikali; ikiwemo kuhakikisha kwamba stahiki za
watumishi wa umma zinapatikana kwa wakati na kwa mujibu wa sheria,
kuhakikisha watumishi wanaokaimu nafasi mbalimbali kwa muda mrefu
waweze kuthibitishwa katika nafasi hizo.
Endapo wana sifa zinazostahili, na kuhakikisha maadili na taratibu za utumishi wa umma zinazingatiwa ili kuleta ufanisi katika kazi na huduma zitolewazo kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment