Na.WAMJW- Dar es Salaam.
Wazalishaji
wa dawa na vifaa tiba wote nchini wametakiwa kuongeza kasi ya
uzalishaji dawa kwa kushirikian na Bohari ya Dawa(MSD) ili kuondokana na
changamoto ya bidhaa hizo nchini.
Rai hiyo ilimetolewa Leo na
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-
Afya Prof. Abel Makubi wakati alipotembelea Bohari ya Dawa na kuongea
na wazalishaji wa dawa na vifaa tiba nchini.
"Tunawashukuru kwa
uzalendo wenu wa kuwekeza nchini, pokeeni salamu kutoka kwa Waziri wa
Afya Dkt. Dorothy Gwajima na Manaibu Waziri".
Hata hivyo Prof.
Makubi amewataka wazalishaji hao kushirikiana na MSD katika kuhakisha
dawa zao zinawafikia wananchi wa vijijini ili kuweza kutatua changamoto
ya Dawa Kwenye vituo vya kutolea Huduma za afya nchini.
Aidha,
Katibu Mkuu huyo amewahakikishia Wazalishaji hao kuwa Serikali ipo
tayari kushirikiana nao na kuhakikisha eneo la uzalishaji dawa linakua
ili kupunguza utegemezi wa dawa kutoka nje ya nchi.
"MSD ni
chombo chetu Cha kuwatumikia wananchi hivyo ni vyema kukipa ushirikiano
ili upatikanaji wa dawa,vifaa na vitendanishi ziwepo wakati
wote".Alisisitiza Prof. Makubi.
Aliongeza kuwa ni wakati Sasa wa
kuanza ukurusa Mpya kati ya Wazalishaji na MSD kwani utawala Bora
unajengwa kwa misingi ya Uzalendo, Uaminifu, na Kuaminiana .
Kwa
upande wa Bei za bidhaa za Dawa, Katibu Mkuu huyo aliwataka Wazalishaji
kukaa pamoja na MSD kupitia upya bei za bidhaa ili ziwe na uhalisia wa
soko bila kuumiza Wananchi.
Licha ya hayo Prof. Makubi
amewaahidi kuwa Serikali itawalipa kwa wakati Wazalishaji wote ambao
watatoa ushirikiano wa kuleta dawa na vifaa kwa wakati na kwa ukamilifu.
Nao Wazalishaji hao ambao ni wamiliki wa viwanda vya dawa na
bidhaa nyinginezo za afya nchini wameahidi kutoa ushirikiano kwa
Serikali katika kuboresha upatikanaji wa dawa nchini na kuuunga mkono
Serikali iliyoko madarakani inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Tuesday, April 20, 2021
WAZALISHAJI WA DAWA NCHINI WATAKIWA KUONGEZA KASI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment