Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa na watendaji wa Shule ya
Viziwi ya Libermann wakionesha Hundi iliyochangiwa na uongozi wa shule
hiyo wakati wa Harambee maalum ya kuchangia vifaa vya shule na vifaa
saidizi kwa wanafunzi wenye uziwi wa shule hiyo, Hafla hiyo ilifanyika
tarehe 25 Septemba, 2021 katika shule hiyo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa Kilele cha
Harambee Maalum ya ununuzi wa vifaa vya kielimu na saidizi pamoja na
maadhimisho ya Somo wa Shule za Libermann iliyofanyika Septemba 25, 2021
shule ya Libermann Viziwi iliyopo kata ya Kawe, Halmashauri ya Manispaa
ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Shule inamilikiwa na Shirika la
Mapadri wa Roho Mtakatifu (Spiritans) Kanda ya Tanzania
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi mchango wake kwa Bw.
Karoli Tarimo, Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya ununuzi wa vifaa vya
kielimu na saidizi kwa wanafunzi wenye uziwi katika shule ya Libermann
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia miundombinu ya
kufundishia watoto wenye mahitaji maalum wa shule ya Libermann Viziwi
alipotembelea kukagua mazingira ya shule hiyo.anayetoa maelezo ni Bi.
Neema Shiyo Mnzava, Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Shule ya Libermann Viziwi Bi. Neema Shiyo Mnzava
akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama miundombinu
ya kufundishia wanafunzi wenye uziwi alipotembelea shule hiyo.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Libermann Viziwi wakionesha ndoto zao baada ya
masomo kwamgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama (hayupo pichani) wakati wa hafla ya Harambee maalumu ya ununuzi
wa vifaa vya shule na saidizi kwa wanafunzi hao.
Meneja
wa Kampuni ya Jatu PLC Bw. Mohamed Simbano akikabidhi msaada wa mchele
kwa uongozi wa Shule ya Libermann Viziwi na katikati ni mgeni rasmi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa Shule ya Libermann Viziwi mara baada ya kumkabidhi zawadi
wakati wa hafla hiyo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akicheza wimbo maalum wa Mjomba
band wa kuhamasisha harambee hiyo na wanafunzi wa Shule ya Libermann
Viziwi wakati wa hafla hiyo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akishiriki maombi maalum ya
kuombea Shule ya Libermann Viziwi pamoja na sala maalum ya sikukuu somo
wa shule hiyo (Francis Maria Libermann) iliyoambatana na harambee hiyo.
Padre
Philip Athanas Massawe C.S.Sp, Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu
(Spiritans) Kanda ya Tanzania, akieleza historia ya Shirika wakati wa
Harambee maalum ya kuchangia vifaa vya shule na Vifaa saidizi kwa
wanafunzi wenye uziwi wa shule hiyo.
Msanii
Mrisho Mpoto (Mjomba) akitoa burudani ya kuhamasisha uchagiaji wa vifaa
vya shule na saidizi kwa wanafunzi wa shule ya Libermann Viziwi.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
…………………………………………………………
NA.MWANDISHI WETU
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
ameongoza harambee maalumu ya ununuzi wa vifaa maalumu vya kielimu na
saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya Libermann
Viziwi.
Halfa hiyo ilifanyika tarehe 25 Septemba, 2021
iliambatana na kumbukumbu ya Somo wa Shule zetu Mwenyeheri Francis Maria
Paul Libermann na pamoja na maadhimisho ya wiki ya Viziwi Duniani.
Waziri
alionesha kufurahishwa na hatua ya uongozi wa shule hiyo kwa kuona
umuhimu wa kusaidia watoto wenye mahitaji maalum na kuendesha harambee
hiyo ili kuwa na vifaa na kuboresha masuala yanayowahusu ili kuwa na
mazingira rafiki ya ufundishaji na kuhakikisha wanatimiza ndoto zao.
“Nimefurahishwa
sana na uamuzi wenu wa kuadhimisha wiki hii ya Viziwi Duniani kwa
kufanya harambee ya kupata fedha za uendeshaji na ununuzi wa vifaa
maalumu vya kielimu na saidizi kwa wanafunzi wetu Wenye Ulemavu.
Hongereni sana,”alesema Waziri Mhagama.
Waziri alieleza
kuwa kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kwa mwaka 2019/2020,
Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 55.9 ambapo milioni
2.5 kati yao ni Watu wenye Ulemavu. Aidha, kwa kipindi kirefu Watu
Wenye Ulemavu wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali katika
kutafuta fursa na huduma za kijamii ikiwemo elimu.
“Watu wenye
ulemavu wamekuwa wakiachwa nyuma katika masuala mbalimbali likiwemo hili
la elimu, niendelee kuiasa jamii kuwapa kipaumbele na kuwawezesha ili
wapate elimu itakayotoa fursa ya kuonesha uwezo walio nao bila kujali
hali zao,”alisisitiza Waziri Mhagama.
Akisoma taarifa ya shule
hiyo Mwalimu Mkuu Bi.Edister Massawe alisema shule inalenga kuunga mkono
jitihada za Serikali katika kuto elimu bora kwa watoto wa Tanzania hasa
wenye mahitaji maalum kama vile viziwi pamoja na kuwapa fursa watoto
wenye ulemavu kupata elimu bora, kusaidia familia zao kwa kuwapatia
ufadhili na udhamini kwa watoto hao ili wajikwamue kielimu.
“Shule
hii ya Viziwi inatoa elimu hiyo bure na imejikita kuwasaidia ili
kuwafanya wabadilike wawe wenye kujitambua, kugundua na kuendeleza
vipaji vyao na kuwajengea uwezo kwenye nyanja za ufundi na biashara ili
waweze kushiriki katika masuala ya ujasiriamali, utunzaji wa mazingira
na afya,”alisema Edister.
Akiongoza ibada maalumu ya kuombea
shule na kumbukumbu ya Somo wa Shule zetu Mwenyeheri Francis Maria Paul
Libermann Padre Philip Athanas Massawe C.S.Sp, Mkuu wa Shirika la Roho
Mtakatifu (Spiritans) Kanda ya Tanzania, alisema jamii iwe mstari wa
mbele bila uoga kuwainua watu wenye mahitaji maalum kwa kuwajengea
ujasiri na kuwatambua kwani kufanya hivyo ni sehemu ya ibada na
kujipatia baraka mbele za Mungu kwa kuwaangalia wahitaji.
“Taifa
tuondoe uwoga na kuwainua watu wenye ulemavu na kuwaona wanaweza na
kuwainua bila kuacha kuwaombea kuyafikia malengo yao,”alieleza Padri
Philip
Shule ya Libermann Viziwi inamilikiwa na Shirika la Mapadri wa Roho mtakatifu (spiritans) Kanda ya Tanzania. Shule ipo kata ya Kawe, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Shule ilisajiliwa rasmi tarehe 11 Septemba, 2019 na kupewa namba za usajili EM. 17973 yenye kaulimbiu isemayo “Moyo mmoja roho moja (One heart one Soul).Ni shule pekee ya viziwi inayotumia mtaala wa Kingereza kwa kufundishia na kujifunzia na ina uwezo wa kuchukua wanafunzia 210 kuanzia ngazi ya awali mpaka darasa la saba.
No comments:
Post a Comment