Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, akielezea maagizo sita
aliyotoa ili kuboreshwa soko la madini ya Tanzanite, Mji mdogo wa
Mirerani, Wilayani Simanjiro, kushoto ni msaidizi wake Mussa Mgogosi.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, RC Charles Makongoro Nyerere, ametoa maagizo sita
kwa sekretarieti ya Mkoa huo na viongozi wa Mamlaka ya Mji mdogo wa
Mirerani ili kuboresha soko la madini ya Tanzanite.
RC
Makongoro amesema miongoni mwa maagizo hayo ni upatikanaji wa
hatimiliki wa ekari 250 za eneo lililotengwa la ujenzi wa soko hilo.
Amesema
hati hizo za ekari 250 zitakabidhiwa kwa halmashauri ya wilaya ya
Simanjiro na ameagiza baada ya wiki tatu hati miliki hizo ziwe
zimekamilika na wahusika kukabidhiwa.
“Baada
ya hati hizo kupatikana shughuli ya ujenzi wa magorofa mawili ya
Tanzanite city zitaanza mara moja ili ofisi mpya za masoko ya madini
zijengwe,” amesema Makongoro.
Amesema
pia ameagiza apatiwe taarifa kamili ya gharama za ujenzi wa majengo
mawili ya ghorofa ya Tanzanite city, ambayo yatakuwa soko la wadau wa
madini ya Tanzanite.
“Mara
baada ya kupatikana kwa hati hizo Wizara ya Fedha na Mipango itatoa
fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo mawili makubwa ya ghorofa,”
amesema Makongoro.
Amesema
pia ameagiza kuundwa kwa kamati tatu ikiwemo kamati ya ujenzi, kamati
ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi na kamati ya mapokezi na amewapa ridhaa
ya kufanya kazi.
Amesema
pia ameagiza usalama uboreshwe kwani hivi sasa madini ya Tanzanite
yanasafirishwa duniani kutoka Mirerani mara baada ya ofisa madini mkazi
Fabian Mshai kutoa kibali.
Amesema
hivi sasa wadau wa madini wanaendelea na biashara yao ya madini ya
Tanzanite kwenye soko lililopo benki ya NMB na soko la mfanyabiashara
Paul Mollel.
Mkazi
wa mji mdogo wa Mirerani, Mashaka Jororo amesema jitihada za serikali
zinaonekana katika kufanikisha ukamilishaji wa soko la madini ya
Tanzanite mji mdogo wa Mirerani.
No comments:
Post a Comment