Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amesema Chama kinaunga mkono juhudi na malengo ya serikali katika kuenzi, kutunza na kuendeleza historia ya ukombozi wa Afrika.
Aidha, amewaomba Watanzania kutembelea kituo cha historia ya ukombozi kilichopo Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza na kujua kazi kubwa iliyofanywa na wapigania uhuru na wana ukombozi wa Afrika, huku Tanzania kikiwa kitovu cha harakati hizo.
Kinana aliyasema hayo leo, alipotembelea ofisi za Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kuboresha majengo yake na kutunza kumbukumbu muhimu.
Ndugu Kinana Amesema CCM inaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni katika kuhifadhi historia na utamaduni wa Tanzania kwa kuwa kufanya hivyo ni kuilinda nchi na utamaduni wake.
Pia Alisema kutokana na wingi wa historia ya ukombozi iliyopo Tanzanmia na kazi kubwa iliyofanyika chini ya Mwalimu Nyerere, kituo hicho kina umuhimu mkubwa.
Makamu Mwenyekiti Kinana aliwahimiza Watanzani kufika zilipo ofizi za program hiyo kwa ajili ya kuona historia ya ukombozi na jinsi Tanzania ilivyoshiriki, pia kuona shughuli na viongozi mbalimbali waliojitoa kufanikisha.
Awali, akizungumza kabla ya kumkaribisha Kinana, Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamadudi, Mohammed Mchengerwa, alimshukuru kwa uamuzi wake huo wa kutembelea ofisi za programu.
Mchengerwa alisema kuanzishwa kwa programu hiyo ni wazo lililobuniwa na Watanzania kutokana na uwepo wa histori kubwa ya harakati za ukombozi, kisha kuushirikisha Umoja wa Afrika (AU) ambao uliridhia jambo hilo na kuagiza makao makuu yawe Tanzania.
Aidha, Waziri Mchengerwa alisema Tanzania inashirikiana na nchi mbalimbali ambapo baadhi zimefungua matawi ya programu hiyo ikiwemo Angola, Msumbiji, Zimbabwe, Afrika Kusini na Namibia.
Alisema lengo la wizara yake ni kutengeneza kituo ambacho kitakuwa cha kisasa kitakachotoa fursa ya kuona historia ya ukombozi katika vifaa vya kisasa vya kidigitali.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo na kuzungumzia picha mbalimbali za Urithi wa Utamaduni na huku waziri wa wizara hiyo akishuhudia, wakati Kinana alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akifurahi pamoja na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamadudi, Mohammed Mchengerwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu wakisoma Chapisho la Hotuba Mbalimbali za Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere alipotembelea maktaba ya wapigania ukombozi Kusini mwa Afrika, alipotembel alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa ameongozana na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Mohamed Mchengerwa (kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa kutoka Wizara hiyo, Boniface Kadili alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya vifaa mbalimbali Vilivyotumika wakati wa Harakati za ukombozi wa Afrika kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Boniface Kadili huku waziri wa wizara hiyo akishuhudia, wakati Kinana alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya Maeneo mbalimbali ya Ukombozi wa Afrika nchini Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Boniface Kadili huku waziri wa wizara hiyo akishuhudia, wakati Kinana alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment