Matokeo chanyA+ online




Wednesday, July 6, 2022

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA PROF. GODIUS KAHYARARA AMESEMA SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMEDHAMIRIA KUIONA TANZANIA INAKUWA LANGO LA UCHUMI WA BARA LA AFRIKA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuiona Tanzania  inakuwa lango la Uchumi wa Bara la Afrika kwa kuwa na Viwanda vikubwa ambavyo vitasaidia kupeleka Bidhaa kwenye Soko la Afrika  kuongeza ajira na pato la Taifa.

Prof. Kahyarara pia amewakaribisha Wawekezaji kuwekeza katika Sekta   mbalimbali  za kipaumbele nchini hususani Sekta ya  Viwanda, Utalii,  Nishati, uvuvi, usafirishaji  ( Reli, Anga na Majini) na uchumi wa bluu.

Prof. Kahyarara ameyasema hayo Julai 05, 2022 alipokuwa akifungua Kongamano la Wawekezaji, Wauzaji na Wanunuaji lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es salaam kama sehemu ya Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalianza tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022

Akifungua Kongamano hilo, Prof Kahyarara amewashauri  wawekezaji wawekeze Tanzania kwa kuwa iko mahali pazuri  kijiografia kwa kuwa na bahari inayowezesha usafirishaji wa mizigo,  Raslimali za kutosha na  Reli ya Kisasa inayoiunganisha  na masoko ya ndani na nje ya nchi kupitia bandari.

Aidha, amesema Serikali imetenga maenwo mbalimbali ya uwekezaji ikiwa ni ni pamoja na uwepo wa kongani za viwanda  zinazotarajiwa kuwa na viwanda  vya kuchakata mazao na kuzalisha bidhaa mbalimbali pamoja maeneo maalumu ya uzalishaji bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje hususani karibu na viwanja vya ndege.

Aidha, Prof. Kahyarara aliwahakikishia wawekezaji  kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora yanayovutia  uwekezaji na ufanyaji biashara nchini kwa kurekebisha sera na sheria mbalimbali  ikiwemo sheria ya uwekezaji,  kuondoa baadhi ya tozo na kuanzisha Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji.

Prof. Kahyarara pia ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita  kwa kutoa kipaumbele katika kukuza uchumi kwa kuchukua  hatua mbalimbali za diplomasia ya uchumi ikiwemo filamu ya Royal Tour ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bi Latifa Mohammed Khamis amesema kupitia Kongamano hilo kuna baadhi ya Makubalino ya Kibiashara yatafikiwa ili kuhakikisha Fursa walizokuja nazo wawekezaji kupitia maonesho ya Saba saba zinawahufaisha watanzania nchini.











 

No comments:

Post a Comment