Wadau mbalimbali nchini Israel wamepongeza jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza na kuienzi Lugha ya Kiswahili.
Pongezi hizo zimetolewa na wadau hao wakati wa Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika tarehe katika Makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo tarehe 07Julai 2022 Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Alex Gabriel Kalua amesema kuwa ametumia maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani kukukutana na kujadiliana na wadau mbalimbali kuhusu namna bora ya kukuza na kuendeleza Lugha hiyo adhimu. Aidha, Mhe. Balozi Kalua ambaye alijumuika na viongozi kutoka Serikali ya Israel, wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Tanzania, Watanzania wanaoishi nchini humo na wageni mbalimbali, alitumia maadhimisho hayo kugawa vitabu vya kujifunzia Kiswahili kikiwemo cha “Jifunze Kiswahili, Hazina ya Afrika: Kitabu cha Kwanza”, pamoja na kushiriki chakula cha Kitanzania na wadau hao. Kadhalika, Mhe. Balozi Kalua alitoa hotuba yake kwa lugha ya Kiswahili ambayo ilitafsiriwa kwa Kiebrania. Naye Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, Bibi Amit Gil Bayaz ambaye ni miongoni mwa viongozi kutoka Serikali ya Israel walioshiriki aliipongeza Tanzania kwa maadhimisho hayo. Maadhimisho hayo yalihitishwa kwa Wadau mbalimbali kushiriki chakula na vinywaji vya kitanzania ambapo walieleza kufurahishwa na ukarimu wa watanzanaia na kufurahia vinywaji na chakula cha kitanzania kilichoandaliwa kwa ajili yao. |
Mhe. Balozi Kalua akimkabidhi kitabu cha kujifunza Kiswahili, Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki, Bibi Amit Gil Bayaz. |
Wawakilishi kutoka Jeshi la Israel walioshiriki maadhimisho ya siku ya Kiswahili wakiwa na Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini, Israel, Brig. Jen. Mziray |
Wadau mbalimbali wakionesha vitabu vya kujifunza Kiswahili walivyokabidhiwa |
No comments:
Post a Comment