Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (Law Reforms Commission of Tanzania –
LRCT) ni injini ya Sekta ya Sheria nchini ambayo imeundwa na Serikali na
kukasimiwa majukumu ya kurekebisha sheria nchini ili kuhakikisha uwepo wa haki
na maendeleo ya taifa kwa wananchi ambapo ni vema kutekeleza majukumu kwa
kuzingatia maadili, sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma
Hayo yameelezwa na Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Waziri wa Katiba na Sheria
wakati akifungua mkutano wa kikao kazi cha mafunzo baina ya viongozi wa Wizara
na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania yanayofanyika kwa siku
tatu kuanzia leo kwenye ukumbi wa Ofisi za Bunge, Dar es Salaam
Waziri Dkt. Ndumbaro amesema kuwa LRCT ni injini ya kurekebisha sheria nchini
hivyo amewataka watumishi kutambua kuwa wamebahatika kupewa jukumu la
kufanya kazi kwenye Tume na amewahimiza kuzingatia maadili, sheria, taratibu na
kanuni za utumishi wa umma kwa vitendo, kwa kujitoa sadaka na kutumikia cheo
alichopewa ili kuwapatia wananchi huduma stahiki
“Hii ni taasisi ya umma, na siyo ya kwenu binafsi, lazima msimame kwenye sheria,
taratibu na kanuni na siyo kutoka nje ya sheria, taratibu na kanuni kwa kuwa sisi
wote ni watumishi wa umma na hakuna mwenye hati miliki ni muhimu mfanye kazi
kwa kuzingatia uzalendo, tuchape kazi kwa bidii, tuheshimu mamlaka ili kuifanya
Tume ing’ae, iendelee kuwa na thamani na kukubalika”, amesisitiza Mhe. Dkt.
Ndumbaro
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Mary Makondo amesema kuwa viongozi na
watumishi wa Tume watapatiwa mafunzo kuhusu maadili kwa watumishi wa umma;
utawala bora; na kutokomeza rushwa katika utumishi wa umma; ambapo lengo la
Wizara kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha mafunzo hayo yanawawezesha
kutekeleza majukumu yao kisheria kwa ajili ya haki na maendeleo ya taifa letu ili
kuwa na uwajibikaji kwa kuzingatia maadili ya watumishi wa umma na mafunzo
hayo yanatolewa na Ofisi ya Rais – Ikulu; Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora; TAKUKURU; na Sekretariati ya Viongozi ya Maadili ya
Umma
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Tume, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mhe. Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Januari Msofe amesema kuwa Tume imezingatia
maelekezo ya Waziri Dkt. Ndumbaro hususani masuala ya maadili kwa kuwa maadili
ni kila kitu, maadili ni popote iwe nyumbani, kazini na mbele ya jamii hivyo
pamoja na mafunzo yaliyotolewa leo viongozi na watumishi wametambua kuwa ni
muhimu kuendelea kujifunza ili kuweza kutekeleza vema majukumu na kuhudumia
wananchi
Naye Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Casmir Kyuki ameishukuru Wizara kwa
kuendeleza utaratibu wa kusimamia Tume hiyo na anaamini kupitia mafunzo hayo
watumishi watatoka na mwamko mpya wa kutekeleza majukumu
No comments:
Post a Comment