Korosho ni zao ambalo chimbuko lake ni Portuguese na baadae karne ya 16
ndipo lilipo fika afrika katika nchi ya msumbiji na baadae likafika
nchini Kenya na Tanzania.
kwa hapa Tanzania korosho hulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya
kusini Mtwara, lindi, na maeneo kama Mafia, bagamoyo na Rufiji.
Korosho ni chakula maalumu cha kutafunwa chenye ladha nzuri na hutafunwa
huku ikiwa imewekwa chokoleti juu yake, lakini sababu ya gharama yake
kubwa korosho haijazoeleka sana kwenye maduka mengi ya vitu vitamu.
Korosho pia hupatikana mara nyingi kwenye mapishi ya thai na China,
huliwa nzimanzima na kusagwa na kuliwa kama unga hasa kama kiungo.
Huko
Malaysia majani huliwa mabichi kama saladi na Brazili korosho hupatikana
kwa wingi mno. Maeneo yote wageni hupata kununua korosho zikiuzwa
barabarani kwenye paketi ndogo ambazo zimefungwa ndani yake na chumvi
kiasi.
No comments:
Post a Comment