Saturday, January 28, 2023
Monday, January 23, 2023
SIASA ZA KIISTARABU ZA RAISI SAMIA NA KUMBUKUMBU YA TUKIO LA " DINNER TABLE BARGAIN 1790 " NCHINI MAREKANI
Na Kassim Mpingi Rufiji-Pwani
Bila Shaka Taifa Linaunganishwa Na Siasa Za Umoja,Mshikamano,Kusameheana Na Kujenga Nchi Kwa Pamoja(4R).
Vyama Pinzani Baada Miaka Saba Vinaingia Tena Mtaani Kufanya Mikutano Na Kufurahi Matunda Ya Siasa Safi Na Za Kiistarabu Za Raisi Samia .
Aina Hii Ya Siasa Anayofanya Raisi Samia Imenifanya Nikumbuke Tukio Muhimu Katika Historia Ya Siasa Za Kiistarabu Duniani Lililotokea Nchini Marekani Mwaka 1790 Lijulikanalo Kama " Dinner Table Bargain " Au " Great Compromise Of 1790 "
Ilikuwa Usiku Wa June 20, 1790 Wakati Mikutano Ya " Congress " Inafanyika Jijini Newyork .Thomas Jefferson Wakati Huo Akiwa Secretary Of The State( Baadae Raisi Wa Tatu Wa Marekani) Alipoamua Kuwaalika Chakula Cha Usiku Watu Wawili Alexander Hamilton Wakati Huo Akiwa Secretary Of Treasure Na James Madison Mwakilishi Wa Jimbo La Virginia( Baadae Raisi Wa Nne Wa Marekani).
Mualiko Huu Ulisukumwa Na Tofauti Kubwa Na Uhasama Uliokuwa Wakati Huo Katika Ujenzi Wa Taifa La Marekani .
Tofauti Kubwa Iliyopelekea Kugawanyika Kwa Taifa Lao Ni Hoja Ya Hamilton Na Wenzake Kuwa Serikali Ya Shirikisho (F.G) Ibebe Madeni Ya Majimbo Yatokanayo Na Vita Vya Mapinduzi .Hoja Hii Ililigawa "Congress" Majimbo Ya Kaskani Yaliunga Mkono Hoja Hii Kwa Vile Madeni Yao Yalikuwa Ni Makubwa Na Wasingeweza Kuyalipa Huku Majimbo Ya Kusini Akiwemo Madison Wakipinga Kwa Kuwa Wao Walishalipa Madeni Yao.
Na Hoja Ya Pili Ilikuwa Wapi Yawe Makao Makuu Ya Taifa Lao La Marekani .
Ni Majadiliani Katika Kikao Hiki "Dinner Table Bargain Of 1790" Kilichoitishwa Na Jafferson Ndicho Kilicholeta Suluhu Hasa Baada Ya Madison Kukubali Hoja Ya Hamilton Na Kushawishi Majimbo Ya Kusini Kuunga Mkono Hoja Na Kwa Pamoja Kulijenga Taifa Lao Ambalo Leo Ni Moja Ya Mataifa Makubwa Na Yenye Nguvu Duniani.
Na Ni Katika Kikao Hii Ndio Maamuzi Ya Kuwa Makao Makuu Ya Taifa Lao Kuwa Newyork Yalifikiwa |
Ndio Maana Tunasema Wakati Huu Nchi Inaunganishwa Na Siasa Za Kiistarabu Za Samia Kupitia Sera Yake Ya "4R" Ni Vyema Kukumbuka Moja Ya Tukio Muhimu Katika Historia Ya Siasa Za Kiistarabu Ulimwenguni.
" The Great Compromise of 1790
Saturday, January 21, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Syngenta Crop Protection AG, Davos nchini Uswizi
Monday, January 9, 2023
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amuapisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Ndugu Griffin Venance Mwakapeje, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya Hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya Hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023. |