Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 14 kujenga shule mpya za sekondari
11 na vituo vya afya 12 mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Mkoa
umefanikiwa kujenga shule hizo mpya katika Halmashauri zote nane za
Mkoa wa Ruvuma kwa gharama ya shilingi Bilioni 7.7.
“Ujenzi huu unajumuisha shule ya Mkoa ya Wasichana inayojengwa eneo
la Migelegele Kata ya Lwinga katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
kwa gharama ya shilingi bilioni nne’’,alisema Kanali Thomas.
Hata hivyo amesema Mkoa umefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa
792 elimu msingi na sekondari yakijumuisha madawati, viti na meza kwa
gharama ya Shilingi Bilioni 14.93
Kwa mujibu wa Kanali Thomas,Mkoa umefanikiwa kujenga mabweni
matano ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa gharama ya
shilingi Milioni 640 na kwamba Mkoa ulipokea fedha kiasi shilingi milioni
400 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara 23 za Shule za Sekondari kupitia
fedha za Tozo na Serikali Kuu.
Akizungumzia kuhusu sekta ya Afya na Ustawi wa Jamii,Kanali Thomas
amesema Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kujenga Vituo vya Afya 12
kupitia fedha za Tozo na Serikali Kuu kwa gharama ya zaidi ya shilingi
bilioni 7.8.
Ameongeza kuwa Mkoa umefanikiwa kujenga nyumba tisa za watumishi
wa Afya kwa gharama ya shilingi Milioni 856 na kwamba Mkoa
umefanikiwa kujenga majengo matatu ya huduma za dharura (EMD) Kwa
gharama ya Shilingi Milioni 900.
Kulingana na Kanali Thomas Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kujenga jengo
moja la wagonjwa mahututi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa
gharama ya shilingi milioni 250 na kujenga zahanati 21 kwa gharama ya
zaidi ya shilingi bilioni moja.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma unaendelea na ujenzi wa Hospitali
tano za Wilaya ya Nyasa, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Halmashauri
ya Madaba na Halmashauri ya Songea kwa gharama ya Shilingi bilioni 3.4
Amesema serikali pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa awamu ya kwanza katika eneo la Mwengemshindo Manispaa ya
Songea kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7.
Amesema ujenzi wa hospitali hiyo unahusisha jengo la wagonjwa wa nje
(OPD), jengo la mionzi na nyumba ya mtumishi na kuongeza kuwa hali ya
upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea
huduma za afya upatikanaji umeongezeka na kufikia asilimia 96.
No comments:
Post a Comment