Matokeo chanyA+ online




Tuesday, February 7, 2023

SERIKALI imefungua milango ya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Marekani kupitia Sekta Binafsi ili kuchochea biashara kupitia uwekezaji ikiwa ni utekelezaji wa mazungumzo kati ya Marais wa nchi hizo mbili yaliyofanyika hivi karibuni mjini Washington DC.

Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Biashara wa Marekani Bi. Marisa Lago, akipokea zawadi ya moja ya vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania (Mlima Kilimanjaro), kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), jijini Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akielezea jitihada za Serikali kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa mapato, wakati wa Mkutano na Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Biashara wa Marekani, Bi. Marisa Lago, jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).



Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Biashara wa Marekani Bi. Marisa Lago, akiipongeza Serikali kwa jitihada za kuimarisha uchumi, wakati wa Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba, akifurahia jambo na Naibu wake, Bi. Amina Khamis Shaabani, kabla ya Mkutano kati Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Biashara wa Marekani, Bi. Marisa Lago (hawapo pichani), jijini Dodoma.

Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Biashara wa Marekani, Bi. Marisa Lago, katika ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kushoto), na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji(Mb) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Biashara wa Marekani, Bi. Marisa Lago (wa tatu kulia), jijini Dodoma. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba (kulia), Naibu wake, Bi. Amina Khamis Shaabani (wa pili kushoto) na Afisa Mwandamizi wa Biashara katika Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Ken Walsh, jijini Dodoma


 

No comments:

Post a Comment