Matokeo chanyA+ online




Friday, February 17, 2023

POPO (FRIUT BATS) KIVUTIO KINGINE KATIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA MAJIMAJI SONGEA

 

Moja ya popo wakubwa dunaini wanaolinga na kunguru ambao wanafika ndani ya Makumbusho hayo  kuanzia mwishoni mwa mwezi Novemba kila mwaka na kuzaliana kisha huondoka mwishoni mwa mwezi Februari.Inaaminika popo hao wabatoka nchini Nigeria




Licha ya kuwepo historia hizo,makumbusho ya Taifa ya Majimaji
imepata aina nyingine ya kivutio cha utalii baada ya kubainika
katika makumbusho hayo kuna aina ya spishi ya popo wakubwa
duniani ambao asili yake ni nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,popo hao wa aina yake kila
mwaka kuanzia Oktoba wanafika katika Makumbusho hayo na
kuweka makazi kwenye eneo la miti mikubwa iliyopo katika
kaburi la pamoja ambalo wamezikwa mashujaa 67.
“Hawa popo wanaokadiriwa kuwa kati ya 6000 hadi 10,000
wakifika hapa wanaishi kuanzia Oktoba hadi Februari kila
mwaka,kutokana na uzito wa popo hawa baadhi ya matawi ya miti
mikavu inaanguka na miti mingine inainama kutokana na
uzito’’,anasisitiza Nyamusya.
Hata hivyo utafiti unaonesha kuwa popo wakubwa kuliko wote
duniani wanapatikana hapa nchini katika visiwa vya Pemba na
Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mtafiti Ng’oko Innocent, popo
wanaopatikana katika visiwa hivyo wanafahamika kwa jina la
flying fox bat au fruit bat ambao wanatajwa kuwa ndiyo popo
wakubwa kuliko wote duniani hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa
watalii.
Ukubwa wa popo hao unakadiliwa kufikia gramu  400 hadi 650 na
kwamba wana mabawa yenye urefu wa  mita 1.6 wakiwa na
sura inayofanana na mnyama aina ya mbweha.

Anasema Popo hao ambao baadhi yao wapo katika msitu wa
bandari ya Wete Pemba wana rangi ya chungwa sehemu ya
tumbo na wana masikio,pua na mabawa meusi ambapo  mara
nyingi ukiwa katika kisiwa hicho popo hao wanapatikana kwenye
misitu mikubwa yenye asili ya matunda.
Kisayansi popo wana faida  kubwa ikiwemo ya kusambaza misitu
kutokana na kula matunda ya aina mbalimbali na kuchavusha
maua na kwamba popo hupendelea misitu yenye mvua.
Popo hujamiana kati ya Januari hadi Juni ambapo jike huzaa
mtoto mmoja kwa mwaka.Inakadiriwa popo wana uwezo wa
kuishi kati ya miaka 15 hadi 30 ingawa  baadhi yao hufikisha
hadi miaka 40.














No comments:

Post a Comment