Matokeo chanyA+ online




Friday, February 17, 2023

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA LONGPING YA CHINA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akifanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Longping
Agriscience LTD wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Liang
Shi, mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 17
Februari 2023.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya
Longping Agriscience LTD wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
hiyo Liang Shi pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde mara
baada ya mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo tarehe 17
Februari 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Longping
Agriscience LTD Liang Shi mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Ikulu Jijini
Dar es salaam leo tarehe 17 Februari 2023.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango leo tarehe 17 Februari 2023 amekutana na kufanya
mazungumzo na viongozi wa Kampuni inayojishughulisha na Kilimo kutoka
nchini China ya Longping Agriscience LTD wakiongozwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Bwana Liang Shi, Mazungumzo yaliofanyika Ikulu
Jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais ameipongeza kampuni hiyo kwa
nia yake ya dhati ya kuwekeza katika kilimo hapa nchini kwa kutambua
uhusiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na China. Amesema Tanzania
inaendelea na jitihada za kuimarisha sekta ya kilimo ikiwemo kuanzisha
programu ya kilimo biashara (Building Better Tomorrow) yenye lengo la
kuwasaidia vijana kushiriki katika sekta hiyo kikamilifu na kuchochochea
ukuaji wake kufikia lengo la asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
Makamu wa Rais amesema ushirikiano huo utaongeza mafanikio zaidi katika
kuifanya Tanzania kuwa nchi tegemeo kwa chakula Barani Afrika kwa
kuzingatia uwepo wa ardhi nzuri ya kilimo pamoja na jiographia ya kuvutia.
Aidha ameongeza kwamba malengo ya kampuni hiyo katika kuweka mnyororo
wa thamani kuanzia uzalishaji wa mbegu hadi uzalishaji mazao na uongezaji
thamani wa mazao hayo viwandani, utaweza kuongeza tija katika kilimo hapa
nchini.
Halikadhalika amewasisitiza kutumia ubunifu, utafiti, ulinzi wa mimea na
matumizi ya teknolojia rafiki ili kuongeza uzalishaji. Pia kutoa mafunzo na
vitendea kazi kwa wakulima na kutumia vema ardhi watakayopata kwa
maendeleo endelevu.
Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Longping Agriscience LTD
bwana Liang Shi amesema Tanzania ni nchi nzuri yenye ardhi ya rutuba
iliobarikiwa kuwa na idadi ya watu ya kutosha pamoja na jiographia
itakayosaidia uzalishaji wa mazao wa uhakika utakaopelekea Tanzania kuwa
tegemeo la chakula kwa Afrika na Dunia kwa ujumla.
Amesema kampuni hiyo imelenga kuanzisha mashamba ya darasa, kuwasaidia
wakulima wazawa kwa mafunzo ya vitendo, kuanzisha vituo vya mauzo
vitakavyoweka uwazi wa bei za mazao katika maeneo mbalimbali nchini.

 




No comments:

Post a Comment