Friday, March 31, 2023
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango wakati akiwaaga wananchi mbalimbali waliojitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam mara baada ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania tarehe 31 Machi 2023.
Thursday, March 30, 2023
Wednesday, March 29, 2023
Rais Mhe. Samia akutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Katoliki la Marekani (Catholic Relief Services) Bw. Sean Callahan Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Katoliki la Marekani (Catholic Relief Services) Bw. Sean Callahan pamoja na Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padri Charles Kitima mara baada ya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Katoliki la Marekani (Catholic Relief Services) Bw. Sean Callahan pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam
|
SUA KUJA NA MAPENDEKEZO YA SERA BORA ZA BIASHARA YA MAZAO YA KILIMO NA NYAMA PORI NCHINI
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Uchumi Kilimo na stadi za Biashara Dkt. Zena Mpenda akifungua warsha ya Wadau wa Mradi wa TRADE HUB kujadili matokeo ya utafiti.
Na Amina Hezron,Morogoro
WADAU wa zao la Soya kahawa miwa na nyama pori wametakiwa kushiriki
kikamilifu kwenye kutoa mapendekezo na
maoni yao kwenye Mradi wa Utafiti wa Biashara,Maendeleo na Mazingira (TRADE
Hub) ili matokeo yatakayopatikana yaweze kuinua tija ya mazao hayo nchini.
Hayo yameelezwa na Kaimu Rasi wa Ndaki ya Uchumi Kilimo na stadi za
Biashara Dkt. Zena Mpendu aliyemuwakilisha Rasi wa Ndaki hiyo Dkt Damas Philip
katika warsha iliyoandaliwa na mradi huo
ili kuwasilisha matokeo ya awali ya utafiti wao kwa wadau ili kupata maoni
yao juu ya namna bora ya kufanya
biashara ya haki na endelevu.
Amewataka wadau hao kuzingatia kuwa tasnia hizo zinagusa kwa namna moja ama
nyingine maisha na maendeleo ya wadau mbalimbali pamoja na uchumi na maendeleo
ya nchi kwa ujumla hivyo watumie fursa hiyo kwa makini kutoa maoni yao ya namna
bora ya kuboresha biashara katika tasnia
hizo zote za Nyama pori na Mazao ya kilimo.
“Ni vizuri tunaposikiliza hizi mada zinazotolewa tuangalie inaelezea kweli
ile hali halisi kwenye maeneo yetu ili tuweze kuboresha yale ambayo tumeyaona
lakini pia tuweze sasa kuangalia mapendekezo yanayotoka tuone hayo mapendekezo
yatafanyika yanawezekana ili tukitoka hapa tuwe na mapendekezo ambayo ni bora
zaidi”, alisema Dkt. Zena.
Dkt. Zena ameeleza kuwa Serikali imekuwa ikiboresha mara kwa mara Sheria,
taratibu na Kanuni kuhakikisha kwamba biashara hizo hazisababishi ongezeko la
uharibifu wa mazingira na upotevu wa baionuai hivyo ni muhimu kama wadau wa
biashara kuhakikisha wanaingia kwenye mikataba ya kijani kwenye biashaa zao ili
kuwe na biashara endelevu kwaajili ya watu na ulimwengu pia.
Akieleza malengo ya warsha hiyo Mratibu wa Utafiti na Machapisho SUA Prof.
Japhet Kashaigili amesema kuwa ni kuwasilisha kwa wadau matokeo ya tafiti
kadhaa ambazo mradi huo umeyapata ili wapate nafasi ya kuyajua, kuyajadili na
kutoa mapendekezo ili kuona ni namna gani yanaweza kuchangia kwenye maendeleo
ya jamii na Taifa kwa ujumla.
“Lengo lingine la pili la warsha yetu hii na mradi ni kutengeneza mpango au
njia itakayotupeleka nchi mahali fulani kuptia ufanyaji wa biashara yenye haki
na endelevu nchini Tanzania lakini pia bidhaa zetu ziweze kuhimili ushindani
kwenye masoko ya kimataifa na kukuza uchumi”, alifafanua Prof. Kashaigili.
Aidha amesema dhumuni kubwa linalobeba mradi huo ni kuhakikisha biashara ya
mazao na nyama pori inakuwa ni injini ya ukuaji wa uchumi jumuishi,Kuondoa
umasikini na kama mbinu ya kutekeeleza maendeleo endelevu kama ilivyosisitizwa
kwenye Mpango wa maendeleo endelevu bila kuchangia uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa mradi huo Prof. Reuben Kadigi amesema warsha hiyo
ya wadau ni muhimu sana katika kupata maoni na mapendekezo ambayo yatawasaidia
watafiti kuweza kutengeneza andiko la sera ambalo litawasilishwa Serikalini ili
kusaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa.
“Kila mchango wa mdau unaotolewa andika mahali kila ushauri andika ili
mwisho wa siku tupate kitu kizuri kifupi cha kuwasilisha serikalini baada ya
kufanya uchambuzi wa kina kulingana na matokeo tuliyoyapata maana mwisho wa
siku hatuwezi kupeleka kwa watunga sera kitu kinacholeweka nawaweze kukifanyia
kazi kwa ustawi wa biashara nchini”, alieleza Prof. Kadigi.
Kwa upande wake Dkt. Charles Malaki aliyemuwakilisha Kaimu Rasi wa Ndaki
hiyo amewashukuru wadau waliojitokeza katika warsha hiyo na amewataka kutoa
maoni na mapendekezo ya kuboresha matokeo ya tafiti hizo ili kuisaidia Serikali
baadae kupata sera bora zitakazosaidia kuwa na uendelevu katika biashara ambayo
inajali Mazingira,Nyama pori pamoja na watu.
Mradi wa Utafiti wa Biashara,Maendelo na Mazingira (TRADE Hub)ni mradi wa miaka mitano unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na washirika wengine kutoka katika nchi kumi na tano za Afrika, Asia, Uingereza na Brazil kuanzia Februari 2019 hadi Machi 2024.
Monday, March 13, 2023
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUU WA WILAYA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mtumba kufungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya tarehe 13 Machi 2023
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akihutubia Wakuu wa Wilaya wanaoshiriki Mafunzo ya Uongozi wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mtumba tarehe 13 Machi 2023.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa TAMISEMI Angellah Kairuki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya wanaoshiriki mafunzo ya uongozi mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mtumba tarehe 13 Machi 2023.
Saturday, March 11, 2023
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amuapisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Wednesday, March 8, 2023
Tuesday, March 7, 2023
WANAWAKE TANESCO, SUWASA SINGIDA WAPANDA MITI KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Wanawake watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida wakionesha furaha yao kabla ya kwenda kupanda miti kwenye chanzo cha maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida ikiwa ni shamra shamra kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, kesho Machi 08,2023.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WANAWAKE watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) na wenzao wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani Machi 08, 2023, wamepanda miti katika chanzo za maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya
Singida ikiwa ni moja ya kazi ya upandaji miti ili kuimarisha uoto wa asili
utakaosaidia upatikanaji wa mvua na hivyo kuimarisha vyanzo vya maji kwa ajili
ya kuzalisha umeme mwingi.
Mbali na upandaji miti wanawake hao wa TANESCO wametoa msaada wa unga, mafuta ya kula, sabuni na vitu vingine kwa watoto yatima wa Kituo cha Upendo Home for Street Children, ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ambayo duniani kote yatafanyika kesho.
Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Machi 7, 2023 kwa kuwashirikisha wakuu wa idara wa taasisi hizo mbili za Serikali mkoani hapa.
Akizungumza katika zoezi hilo la upandaji miti Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo, Lulu Silungwe alisema TANESCO imekuwa ikitegemea mvua inayotokana na miti kwa ajili ya kusambaza huduma ya umeme hivyo zoezi hilo la upandaji wa miti litasaidia kukabiliana na athari za kimazingira na mvua kuwa nyingi.
“Tumekutana hapa leo na wenzetu kutoka SUWASA kwa ajili ya kupanda miti chanzo cha maji Mwankoko chini ya kauli mbiyu yetu isemayo Panda Miti, Mvua Ndi, Umeme Ndindindi ikiwa ni moja ya kazi yetu kuelekea maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo ni kesho” alisema Silungwe.
Alisema mbali ya kupanda miti pia watawatembelea watoto Yatima wanaolelewa Kituo cha Upendo Home for Street Children, kwa ajili ya kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwa ni kazi yao nyingine kuelekea maadhimisho hayo.
Neema Ntandu ambaye ni mfanyakazi wa shirika hilo alisema wamepanda miti 150 ya aina mbalimbali na kuwa watahakikisha inakuwa na kuimarisha chanzo hicho cha maji cha Mwankoko.
Mwenyekiti wa Wanawake wa Shirika hilo Mkoa wa Singida, Asiatu Mnanura akizungumza wakati wa kutoa msaada kwa watoto wa kituo hicho alisema wamefurahi kuwatembelea ukizingatia kuwa wao ni wazazi hivyo waliona vizuri jambo hilo liwe ni sehemu ya moja ya kazi yao kuelekea maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa SUWASA, Fatina Mbaga alisema ni wajibu kwa kila mwana Singida kupanda miti kwa wingi ili kuhifadhi mazingira jambo litakalosaidi kuhifadhi mazingira na kuwepo kwa mvua nyingi na hivyo kuwa na maji ya kutosha.
Mratibu wa kituo hicho Afesso Ogenga alishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa kituo hicho kinawapokea watoto kutoka mitaani na majumbani lakini ni baada ya kufanyika utaratibu wa kuwatambua na kujua historia zao kwa kushirikiana na watu wa ustawi wa jamii.
Wanawake watumishi wa Tanesco Mkoa wa Singida wakifanya maandamano kuelekea katika zoezi hilo la kupanda miti.
Mratibu wa Kituo cha Home for Street Children, Afesso Ogenga akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo.Wanawake watumishi wa Suwasa Mkoa wa Singida wakipanda ngazi kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda kupanda miti.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Suwasa, Fatina Mbaga, akizungumzia kuhusu zoezi hilo la upandaji miti.