Thursday, April 27, 2023
Wednesday, April 26, 2023
Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera, mwenye matatizo ya ngozi
Tuesday, April 25, 2023
KLINIKI YA AGA KHAN, MKOA WA MJINI MAGHARIBI.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amesema Shirika la maaendeleo la Aga Khan (AKDN) limekuwa likijitahidi kuimarisha afya na ustawi wa jamii ulimwenguni kote pamoja na Zanzibar. Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 25 Aprili 2023 katika uzinduzi wa kituo cha afya cha Kliniki cha Aga Khan ambacho kitatoa huduma za dharura, huduma za kibingwa pia wagonjwa watapata huduma za afya zilizounganishwa dijitali na Hospitali ya Aga Khan iliyopo Dar es Salaam. Serikali ya Zanzibar inatambua umuhimu wa huduma bora za afya hivyo sekta hiyo imepata mageuzi makubwa ambayo yanajumuisha huduma za afya kwa ngazi ya shehia, wilaya hadi mkoa kupitia Hospitali za rufaa ikiwa na jumla ya vituo vya afya 172 ambavyo vipo katika wilaya 11 Zanzibar. Naye Binti Mfalme Zahra Aga Khan alisema uwekezaji kupitia Shirika la maendeleo la Aga Khan kupitia miundombinu ya huduma za afya ya Zanzibar inaonyesha dhamira yake ya kuendelea kuboresha afya na ustawi wa jamii ulimwenguni kote.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Balozi wa Muungano wa Umoja wa Falme za Kiarabu Nchini Tanzania (UAE), Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa (UAE) Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi alipofika Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 25 Aprili 2023.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa (UAE) Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi alipofika Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 25 April 2023.
|
Saturday, April 22, 2023
RAIS SAMIA AHUTUBIA BARAZA LA EID EL-FITR KITAIFA LILILOFANYIKA JNICC JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Baraza la Eid El-Fitr ambalo Kitaifa limefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2023. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kwenye Baraza la Eid El-Fitr ambalo Kitaifa limefanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2023. |
Tuesday, April 18, 2023
JK AKUTANA NA WANARIADHA GABRIEL GEAY NA WENCE TARIMO MJINI BOSTON, MAREKANI
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar na kushoto ni mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya jezi toka kwa mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo wakati alipoonana na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha mwanariadha Gabriel Geay mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kitabu mwanariadha Gabriel Geay mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar wakiwa na Watanzania waishio Marekani pamoja na wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo na kushoto ni mtoto wa Bongo Zozo. |
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo aliyeongozana na mwanariadha Gabriel Geay alipokutana nao mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon. |
KAMATI KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI YAANZA KAZI RASMI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Kamati ya Kutathmini Utendaji wa Wizara alipokutana nayo jijini Dodoma tarehe 18 Aprili 2023 kama ishara ya kuanza rasmi kwa kazi ya Kamati hiyo. Kamati hiyo ambayo iliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 28 Machi, 2023 inao wajumbe saba (7) na inaongozwa na Balozi Msatafu, Mhe. Hassan Simba Yahya (wa kwanza kushoto) |
Kikao na Kamati kikiendelea |
Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianio wa Afrika Mashariki, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax |
Mjumbe wa Kamati, Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akiwa kwenye Kikao kati ya Kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax. Kushoto ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati hiyo |
Wajumbe wengine wa Kamati ambao ni Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kulia) na Balozi Peter Kalaghe wakati wa kikao kati ya kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax |
Mjumbe wa Kamati, Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka (kulia) akiwa na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati (kushoto) |
Wajumbe wengine wa Kamati ambao ni Balozi Tuvako Manongi (kushoto) na Mhe. Balozi George Madafa wakati wa kikao kati ya Kamati na Mhe. Waziri Tax |
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati wakifuatilia kikao |
Kikao kikiendelea |
Mhe. Dkt. Tax (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Simba (wa pili kushoto mstari wa kwanza) pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo |
Mhe. Dkt. Tax (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja
na Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Simba (wa pili kushoto
mstari wa kwanza), Wajumbe wa Kamati pamoja na Sekretarieti ya Kamati hiyo |