Friday, May 26, 2023
Tuesday, May 23, 2023
NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA UWAJIBAKAJI UNAOZINGATIA SHERIA SEKTA YA ARDHI
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika tarehe 22 Mei 2023 mkoani Dodoma. |
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akizungumza wakati wa kikoa cha Baraza la Wafanyakazi wa wizara yake tarehe 22 Mei 2023 mkoani Dodoma |
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda akizungumza katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake tarehe 22 Mei 2023 jijini Dodoma. |
Naibu waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema watumishi wa sekta ya ardhi nchini wanao wajibu katika utendaji kazi na dhana nzima ya kuongeza ufanisi na tija kwa kuzingatia sheria.
"Tunahitaji nidhamu na miongozo mbalimbali ili kutoa huduma stahiki kwa watanzania.
Pinda aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleio ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema hayo tarehe 22 Mei 2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendekeo ya Makazi.
Aidha, amesema mwajiri naye anao wajibu wa kuweka mazingira mazuri mahali pa kazi sambamba na kuwaheshimu watumishi na kuwaendeleza ili kuwezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akigeukia suala la urasimishaji makazi holela, Naibu Waziri Pinda alisema mpango wa urasimishaji unafikia kikomo mwaka huu wa 2023 na makazi holela yanaendelea kushamiri huku miji ikikua kwa kasi.
Kwa mujibu wa Pinda aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, kazi ya Baraza la Wafanyakazi ni kutumia mkutano huo wa Baraza kuishauri serikali juu ya mkakati mpya wa kuondoa makazi holela.
Amelitaka Baraza la Wafanyakazi kujadili kwa kina makadirio ya mipango ya matumizi kwa mwaka 2023/2024 na kuweka mipango inayotekelezeka.
Pamoja na mambo mengine ametaka kuwekwa mikakati madhubuti kwenye masuala ya makusanyo ya kodi ya ardhi ambapo amesema wizara imekusanya bil 129 sawa asilimia 51.6 ya lengo jambo alilolieleza halikubalikia.
Ameelekeza kila mkoa kuongeza kasi ya makusanyo ili kutimiza lengo lililowekwa na kuchukua hatua kwa wadaiwa wote sugu kutokana na muda wa msamaha wa rais kupita.
UHUSIANO WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI UKO IMARA
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiongea na watumishi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi.Fatma Hamad Rajab.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini uko imara na unaendelea kukua siku hadi siku katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya Utamaduni.
Balozi Milanzi amesema hayo Mei 22, 2023 jijini Pritoria nchini Afrika Kusini wakati akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo ambao walifika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini humo kujitambulisha kuwa watakuwa kwenye ziara ya mafunzo yenye lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu na Afrika Kusini katika masuala ya Utamaduni na Sanaa.
“Ugeni huu sasa ni wa pande mbili za Muungano hasa kwenye eneo hili muhimu la Utamaduni. Utamaduni ni dhana pana zaidi, kuna suala la lugha, vyakula, mavazi. Mimi nimependa sana mwelekeo huu wa Serikali na wizara zetu za Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, sasa zinafanya vizuri kwenye masuala ya michezo, masuala na Utamaduni, karibuni sana hapa Afrika Kusini” amesema Balozi Milanzi.
Uhusiano huo mwema umedhihirishwa kwa mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili ambapo baadhi ya wajumbe kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wapo Afrika Kusini kwa ziara ya mafunzo yenye lengo la kubadilishana uzoefu katika kuendesha sekta za Wizara hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa msafara ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Fatma Hamad Rajab amesema kuwa nchi zetu zinahitaji kushirikiana ili kutunza urithi wake kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Aidha, mafunzo hayo pamoja na mambo mengine yanalenga kubadilishana ujuzi na kuboresha namna ya kuendesha Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika ili kuhifadhi, kulinda na kuendeleza historia ya nchi hizo mbili za Tanzania na Afrika Kusini.
Monday, May 22, 2023
DK.MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA QATAR KUJA ZANZIBAR
Katika ziara yake Rais Dk. Mwinyi leo asubuhi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Qatar Mhe. Muhamed Bin Ahmed Al-Kuwari na wadau kutoka sekta binafsi ya Viwanda.
Dk. Mwinyi aliwakaribisha wafanyabiashara hao wakubwa kuwekeza zanzibar kutokana na fursa zilizopo pia aligusia eneo jipya la uwekezaji ambalo ni utalii wa kumbi za mikutano.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ZIPA Shariff Ali Shariff alieleza umuhimu wa kukutana kwa Mabaraza ya uwekezaji ya Zanzibar na Qatar ili kuimarisha uhusiano zaidi.
Pia alielezea fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar zaidi kwa upande wa utalii kwani ujenzi wa hoteli kubwa za kifahari unahitajika kutokana na soko la utalii kuongezeka.
Fursa nyingine alizowakaribisha kuwekeza ni ukodishaji wa visiwa vidogo.
Halikadhalika aliwafahamisha kwa undani fursa zilizopo katika sera ya uchumi wa Buluu ambayo imewagusa zaidi wawekezaji hao hasa suala la uchimbaji wa gesi na mafuta.
Eneo jingine ni shamba la Makurunge Bagamoyo ambalo ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar linalofaa kwa utalii na hata kilimo.
📆 22 Mei 2023
📍Doha, Qatar
Monday, May 15, 2023
KELELE NA MITETEMO INAUWA WATOTO NJITI 12,000 KWA MWAKA ULAYA PEKE YAKE
Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kelele kuwa ni mojawapo ya
kisababishi cha madhara katika maisha ya binadamu. Aidha, kwa mujibu wa “European Environmental Agency” (EEA, 2018) kelele zimeainishwa kuwa mojawapo ya visababishi vya vifo vya mapema vya watoto “Pre-mature death” ambapo takwimu zinaonyesha takribani watoto 12,000 hufariki kila Mwaka katika Bara la Ulaya”. Katika nchi yetu changamoto ya kelele zinazozidi viwango vilivyoainishwa na TBS zinatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia. Kwa siku za hivi karibuni, kelele zimeongezeka kwenye maeneo ya kazi na hivyo kusababisha matatizo ya kiafya ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza umakini katika mafunzo, ajali na kupungua uwezo wa kusikilizana. Vyanzo vikuu vya kelele hizi ni kumbi za starehe hasa biashara za vileo (baa), vyombo ya usafiri na usafirishaji (kama magari, ndege na treni), matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwanda vikubwa na vidogo (Karakana za kuchomelea, ufyatuaji matofali, mashine za kusaga na kukoboa nafaka), majenereta, matangazo ya biashara mitaani, shughuli za ujenzi, nyumba za ibada n.k. |
SHERIA NA SERA ZINAZOONGOZA UDHIBITI WA
KELELE NA MITETEMO
Udhibiti wa kelele na mitetemo nchini unasimamiwa na Sheria mbalimbali
zikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 pamoja na
Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa Kelele na Mitetemo) za
Mwaka 2015; Sheria ya Usalama Kazini ya Mwaka 2003; Sheria ya Afya ya
Jamii ya Mwaka 2009; Sheria ya Jumuiya [Sura ya 337 Marejeo ya 2002];
Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa [Sura 204 Marejeo ya 2002] na Kanuni za
Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018; Sheria ya Ardhi [sura 113 Marejeo ya
Mwaka 2019] na Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 pamoja na Kanuni
zake za Mwaka 2018.
Sheria na Kanuni hizi zimeelekeza shughuli zote zenye madhara zifanyike
mbali na makazi ya watu na hivyo shughuli zenye kelele kufanyika mbali na
makazi ya watu ili kupunguza madhara kwa afya ya binadamu na mazingira.
BARAZA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA (NEMC)
Katika kuhakikisha kelele na mitetemo zitokanazo na shughuli mbalimbali
zinadhibitiwa, Baraza litafanya yafuatayo:
a. Kuendelea na ukaguzi wa maeneo ya biashara na kutoa
maelekezo mbalimbali ikiwemo Amri na Ilani za kudhibiti kelele.
b. Kuanisha na kutangaza maeneo ambayo kelele haziruhusiwi
(Noise Control Zone).
c. Kusimamia uanishaji wa ramani za maeneo yenye kelele
zilizopitiliza na kuandaa Mkakati wa udhibiti.
Mwongozo wa Kitaifa wa Udhibiti Kelele na Mitetemo
d. Kufanya tafiti za mara kwa mara kubaini hali ya uchafuzi wa
mazingira utokanao na kelele na mitetemo.
e. Kutoa elimu kwa jamii na maafisa mazingira kuhusu majukumu
yao katika udhibiti wa kelele na mitetemo.
f. Kupokea taarifa za malalamiko yanayohusu kelele na mitetemo.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan aongoza Viongozi pamoja na Waombolezaji kuaga Mwili wa Marehemu Bernard Kamilius Membe, Karimjee Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2023
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2023
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na waombolezaji kabla ya kuwaongoza kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernard Kamilius Membe katika viwanja vya Karimjee tarehe 14 Mei, 2023.
|