Matokeo chanyA+ online




Wednesday, November 22, 2023

Hakutakuwa na watoto watakao tembea umbali mrefu kufuata elimu

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inajenga shule mpya nchini ili kutatua changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu na kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani.

Dkt. Msonde amesema hayo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mputa inayojengwa kupitia fedha za mradi wa SEQUIP Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

“Serikali haijengi shule kwasababu ya kujifurahisha au kumridhisha mtu bali inajenga shule kwa lengo la kuwawezesha watoto wasitembee umbali mrefu kufuata elimu, lengo la Mhe. Rais kujenga shule ni kuwawezesha watoto wa kitanzania wanaoingia sekondari kumaliza masomo bila kisingizio cha umbali ili waondoke na ujuzi na umahiri wa kujiletea maendeleo yao pamoja na kuleta maendeleo ya jamii zao na taifa kwa ujumla,” amesema.

Ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwa kuchagua eneo zuri la kujenga Shule ya Sekondari ya Mputa na kuongeza kuwa, ujenzi wake ukikamilika vizuri inaweza kuongezwa hadhi ya kuwa na kidato cha tano na cha sita.

Awali, akitoa taarifa ya ujenzi huo, Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari Mputa, Godlove Chumi amesema ujenzi umefikia asilimia 71 na hadi sasa Sh.Milioni 379.9 zimetumika kati ya Sh.milioni 560.5 zilizopelekwa kupitia mradi wa SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya.

:Tamisemi

Saturday, November 18, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa wito wa kulinda na kuhifadhi mazingira ya Ziwa Tanganyika na rasilimali zake.


Ziwa Tanganyika ni moja ya maziwa makubwa ya Afrika ya Kati likienea mpakani mwa TanzaniaJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoBurundi na Zambia.

Ni ziwa kubwa la pili duniani kwa wingi wa maji matamu baada ya Ziwa Baikal (Siberia) kwa kuzingatia kiasi cha maji ndani yake na kina (hadi mita 1,470).

Kwa kulinganisha eneo lake (km² 32,893) ni la pili tu baada ya Viktoria Nyanza katika Afrika.

Maji yake hutoka kuelekea mto Kongo ha hatimaye katika Bahari Atlantiki.






Dkt. Jafo alitoa wito huo wakati wa Mkutano wa 11 wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika uliofanyika Zambia. Alisisitiza kuwa ziwa hilo ni zaidi ya kapu la chakula na nyumbani kwa watu milioni 13, na hivyo ni jukumu letu kulinda rasilimali zake.

Mkutano huo ulitumika kutoa mwongozo kuelekea matumizi endelevu ya rasilimali za ziwa na kushuhudia tukio la kutia saini Itifaki ya Maendeleo ya Ufugaji wa Majini katika Ziwa Tanganyika na bonde lake. Dkt. Jafo pia alishukuru wadau wa maendeleo kwa juhudi zao katika usimamizi endelevu wa ziwa hilo.

Katika kufunga mkutano, Dkt. Jafo alimpongeza Mhe. Mhandisi Dkt. Collins Nzovu wa Zambia kwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza Kuu la Mawaziri. Mkutano ulijadili masuala muhimu kama vile uwezekano wa kuwajumuisha Makatibu Wakuu katika Vyombo vya Sheria vya LTA, Itifaki ya Maendeleo ya Kilimo cha Majini kwa Ziwa Tanganyika, utafiti wa bioanuwai, na hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali. Washiriki walipokea pia taarifa kuhusu michango ya kitaifa na mpango wa kazi wa mwaka pamoja na bajeti ya LTA ya mwaka 2024.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi nne wanachama wa ziwa hilo, na ujumbe wa Tanzania uliokuwa na Naibu Katibu Mkuu (Muungano), Mkurugenzi wa Mazingira, na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Kundi la 04/20-Shahada ya Sayansi ya Kijeshi.








Wednesday, November 15, 2023

BWAWA LA NYERERE NI ZIWA JIPYA ULIMWENGUNI



Linakuwa Eneo la tisa kwa ukubwa Ulimwenguni, la nne kwa ukubwa barani Afrika, na kubwa zaidi Mashariki mwa Afrika. Kwa urefu wa kilomita 100 (maili 62), upana wa kilomita za mraba 1,200 (maili za mraba 460), Likizuiwa naukuta wa konkriti wenye urefu wa mita 134 [futi 440] likiwa na kiasi cha maji cha mita za ujazo bilioni 34. linakuwa ziwa jipya kuzalishw ulimwenguni  hiki cha kuzalisha umeme, Julius Nyerere Hydropower Station. Bwawa la Mteremko wa Stiegler,..Sisi ni Tanzania..na haya ndio matokeochanya+

 

 

Wagojwa 32,867 watibiwa moyo JKCI kwa kipindi cha miezi mitatu


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.



Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Daktari bingwa wa usingizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhe. Balozi Ulisubisya Mpoki akielezea maendeleo ya Taasisi hiyo tangu kuanzishwa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akichangia mada wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Afisa Manunuzi na Ugavi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Victor Kapama akielezea mchakato wa manunuzi unavyotakiwa kufuatwa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akijibu hoja zilizohusu idara yake wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Na: JKCI

********************************************************************************************************

Wagonjwa 32,867 watu wazima 30,616 na watoto 2,251 wenye matatizo mbalimbali ya moyo wamepata huduma ya matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miezi mitatu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akisoma taarifa ya kazi zilizofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 katika mwaka wa fedha wa 2023/24 katika kikao cha wafanyakazi wa JKCI kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema wagonjwa waliolazwa walikuwa 1,131 kati ya hao watu wazima walikuwa 1030 na watoto 101.

“Kupitia mtambo wa Cathlab ambayo ni maabara inayotumia mionzi maalumu kwaajili ya uchunguzi wa matatizo na tiba za magonjwa ya moyo wagonjwa 638 watu wazima 630 na watoto nane  walipata huduma za uchunguzi, kuzibuliwa mishipa ya damu ya moyo iliyoziba pamoja na kupandikizwa vifaa visaidizi vya moyo”, .

Wagonjwa 129 ambao ni watoto na watu wazima walifanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kubadilishwa valvu, kupandikizwa mishipa ya damu ya moyo (Coronary artery bypass grafting – CABG), kukarabati mishipa ya damu ya moyo iliyotanuka au kuchanika, kuziba matundu ya moyo, kutoa uvimbe katika kifua au mapafu, kupandikiza na kuzibua mishipa ya damu ya miguu.

Dkt. Kisenge alisema kwa kipindi hicho cha miezi mitatu waliona wagonjwa 61 kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Visiwa vya Comoro, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nje ya Africa ambazo ni nchi za Canada, Ufaransa na India.

“Tulifanya vipimo 14,864  vya jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) na mfumo wa umeme wa moyo (ECG), X-Ray 3,815 zilifanyika,  vipimo vya maabara 7,966 na ultrasound 1,881 zilifanyika pia dawa zilitolewa kwa wagonjwa 30,249”, alisema Dkt. Kisenge. 

Mkurugenzi huyo Mtendaji aliwakumbusha wafanyakazi wa JKCI kumtanguliza Mungu mbele katika kazi zao za kila siku huku wakiiombea taasisi hiyo ili iweze kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaowatibu. 

Dkt. Kisenge alisema kutokana na huduma bora inayotolewa katika Taasisi hiyo imekuwa kivutio cha wagonjwa wengi kutoka ndani na nje ya nchi kutaka kutibiwa hapo na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuimarisha huduma za matibabu ya moyo nchini.

Kwa upande wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo waliohudhuria mkutano huo waliishukuru menejimenti ya JKCI kwa kuwaongoza vizuri na kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata maslahi yao kwa wakati.

“Kuna watu wengi wanaohitaji kupata huduma za matibabu ya moyo tunazozitoa, ni jukumu letu kama Taasisi kutangaza huduma zetu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili tuweze kuwafikia wananchi wengi zaidi”, alisema Jilala John ambaye ni Afisa Uuguzi katika Taasisi hiyo.