Matokeo chanyA+ online




Tuesday, January 2, 2024

 Maandalizi Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa Yakamilika, Kufanyika Ukumbi wa JNICC


Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji, Francis K. Mutungi akitoa ufafanuzi wakati wa Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kilichoketi leo tarehe 2 Januari 2024 jijini Dar es Salaam. Kikao hicho cha maandalizi ya mwisho kuelekea Mkutano Maalum wa wadau wa Demokrasia na Vyama vingi vya siasa nchini utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia kesho tarehe 3 – 4 Januari 2024 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC). Picha na ORPP



Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa anayeshughulia Usajili na Ufuatiliaji, Sisty Nyahoza akitoa maelezo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu hatua ya maandalizi ya mwisho kuelekea Mkutano Maalum wa wadau wa Demokrasia na Vyama vingi vya siasa leo tarehe 2 Januari 2024 jijini Dar es Salaam. Mkutano huo  utafanyika kwa siku mbili kuanzia kesho tarehe 3 – 4 Januari 2024 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)

Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya baraza hilo, Ndg. Doyo Hassan Doyo akichangia mada wakati wa Kikao cha kutathmini maandalizi ya mwisho ya Mkutano Maalum wa wadau wa Demokrasia na Vyama vingi vya siasa leo tarehe 2 Januari 2024 jijini Dar es Salaam. Mkutano huo  utafanyika kwa siku mbili kuanzia kesho tarehe 3 – 4 Januari 2024 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)

Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi na Fedha ya baraza hilo, Salum Mwalimu akichangia mada wakati wa kikao cha kutathmini maandalizi ya mwisho ya Mkutano Maalum wa wadau wa Demokrasia na Vyama vingi vya siasa leo tarehe 2 Januari 2024 jijini Dar es Salaam. Mkutano huo  utafanyika kwa siku mbili kuanzia kesho tarehe 3 – 4 Januari 2024 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)



No comments:

Post a Comment