RAIS DK. MWINYI; ZANZIBAR KUPUNGUZIWA GHARAMA ZA UENDESHAJI WA MIRADI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameonesha utayari wa Serikali ya Zanzibar kushirikiana na Taasisi ya Mabenki Yasiyo na Mipaka (Bankers without Boundaries) katika kuwekeza kwenye miradi ya kipaumbele ambayo italeta tija kwa nchi.
Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo leo, tarehe 14 Agosti 2024, alipokutana na Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Matteo Scollabrino, aliyefika Ikulu Zanzibar akiwa ameongozana na ujumbe wake kutoka makao makuu ya taasisi hiyo yaliyopo nchini Uingereza.
Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa Serikali inatilia mkazo sekta muhimu kama Uchumi wa Buluu, Kilimo, Nishati, Miundombinu, na Afya. Sekta hizi zimebainishwa kuwa ni kipaumbele na zinahitaji msukumo wa ziada ili kuhakikisha zinaweza kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment