Matokeo chanyA+ online




Saturday, March 10, 2018

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN MAGUFULI AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHATO MKOANI GEITA.MACHI 9,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.March 9,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali wa Chato waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.March 9,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali wa Chato waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.March 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mkuu mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel mara baada ya kuwasili katika sherehe za ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.March 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kuwasili katika sherehe za ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.March 9,2018.
Wananchi mbalimbali wa Chato wakifurahia katika ufunguzi huo Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.March 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay mara baada ya Benki hiyo kuchangia mfuko wa Elimu wa mkoa wa Geita kwa kutoa kiasi cha Shilingi milioni 50 kabla ya ufunguzi wa Tawi hilo la Benki.March 9,2018.
Mcheza ngoma za asili wa kikundi kutoka Chato akionesha umahiri wake wa kucheza ngoma katika sherehe za ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wakati kikundi cha ngoma za asili kutoka Chato(hakionekani pichani) kilipokuwa kikitumbuiza katika viwanja wa Tawi la Benki ya CRDB kabla ya ufunguzi.March 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwa kupiga makofi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji wakati msanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Chato alipokuwa akitoa burudani ya ngoma hiyo.
Mmoja wa wacheza ngoma wa kikundi cha Ngoma za asili cha Chato akimwagiwa Rangi kabla ya kuonesha umahiri wake wa kucheza ngoma hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Denmark hapa nchini Einar Hebogard Jensen wakati akielekea kwenda kufungua Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.March 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji wakati wakipiga picha ya pamoja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati msanii wa Msechu Bendi Peter Msechu alipokuwa akiimba mara baada ya kufungua tawi hilo la Benki.March 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay, Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei kabla ya ufunguzi wa tawi hilo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Chato mara baada ya kutoka kwenye ufunguzi wa tawi hilo la benki ya CRDB lilopo Chato mkoani Geita.March 9,2018.

Monday, February 26, 2018

TAASISI ZA MTANDAO WA WANAWAKE WAKUTANA KUJADILI UTUNGWAJI WA SHARIA MPYA YA VYAMA VYA SIASA ITAKAYOLENGA UJENZI WA USAWA WA JINSIA.


Mkutano Huo Ulioandaliwa Na Tanzania Women Cross Platform (Ulingo) Umehudhuriwa Na Mabaraza/Jumuiya Za Wanawake Kutoka Vyama Mbali Mbali Vya Siasa, Viongozi Wa Barazaa Vyama Vya Siasa, Tanzania Center For Democracy, Mtandao Wa Wanawake Wa Kikatiba Na Uongozi, Women Fund Tanzania, Tanzania Women Parliamentary Group Pamoja Na Umoja Wa Wanawake Wawakilishi Zanzibar

Baadhi Ya Maridhiano Ya Mkutano Ilikuwa Ni Pamoja Na;
1. Kutaka Sheria Mpya Kutoa Maelekezo Kwa Katiba Za Vyama Vya Siasa Kutambua Nafasi Za Usawa Wa Jinsi Katika Nafasi Na Vikao Muhimu.

2. Kutaka Sheria Mpya Iwatambue Kikatiba Nafasi Za Usawa Kwa Wanawake (Kuwe Na Deliberate Clause)

3. Wajumbe Wameomba Vyama Vya Siasa Vipunguziwe Nguvu Ili Kuwa Na Taasisi Imara Ambazo Sio Za Kisiasa

4. Wajumbe Pia Wamelaani Vikali Matumizi Ya Lugha Zisizo Na Staha Zinazoendelea Katika Majukwaa Ya Kisiasa Na Kusema Kwamba Huo Sio Utamaduni Wetu Wa Siasa

Mgeni rasmi wa mkutano huo Mhe Naibu Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar amepokea mapendekezo na maridhiano ambayo yatafikishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kama maoni katika kuandaa sheria mpya ya vyama vya siasa.

Pamoja na wajumbe wengine muhimu waliohudhuria akiwemo Mhe John Cheyo, Mhe John Shibuda, Mhe Suzan Lymo, pamoja na wengine wengi wamekubaliana kuandaa kikao kupitia ULINGO ili kukutana na viongozi wote wa vyama vya siasa katika kueleza maoni yao.
















Wednesday, February 21, 2018

ZIARA  YA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN MKOANI SIMIYU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma maneno yalioandikwa kwenye jiwe la msingi mara baada ya kufungua jengo la upasuaji kwenye hospitali ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais akimsabahi Mtoto Mchanga pamoja na Mama yake Bi. Mariam Patrik mkazi wa Nyashimba ambaye amejifungua katika wodi ya wazazi ya hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Simiyu mara baada ya kufungua jengo la Upasuaji lililopewa jina la Samia Suluhu Hassan Operating Theatre.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe pamoja na viongozi wa mkoa wa Simiyu kama ishara ya ufunguzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima lenye vyumba 43 vya kufanyia kazi.


MAKAMU WA RAIS  MKOANI SIMIYU