Mkutano Huo Ulioandaliwa Na Tanzania Women Cross Platform (Ulingo) Umehudhuriwa Na Mabaraza/Jumuiya Za Wanawake Kutoka Vyama Mbali Mbali Vya Siasa, Viongozi Wa Barazaa Vyama Vya Siasa, Tanzania Center For Democracy, Mtandao Wa Wanawake Wa Kikatiba Na Uongozi, Women Fund Tanzania, Tanzania Women Parliamentary Group Pamoja Na Umoja Wa Wanawake Wawakilishi Zanzibar
Baadhi Ya Maridhiano Ya Mkutano Ilikuwa Ni Pamoja Na;
1. Kutaka Sheria Mpya Kutoa Maelekezo Kwa Katiba Za Vyama Vya Siasa Kutambua Nafasi Za Usawa Wa Jinsi Katika Nafasi Na Vikao Muhimu.
2. Kutaka Sheria Mpya Iwatambue Kikatiba Nafasi Za Usawa Kwa Wanawake (Kuwe Na Deliberate Clause)
3. Wajumbe Wameomba Vyama Vya Siasa Vipunguziwe Nguvu Ili Kuwa Na Taasisi Imara Ambazo Sio Za Kisiasa
4. Wajumbe Pia Wamelaani Vikali Matumizi Ya Lugha Zisizo Na Staha Zinazoendelea Katika Majukwaa Ya Kisiasa Na Kusema Kwamba Huo Sio Utamaduni Wetu Wa Siasa
Mgeni rasmi wa mkutano huo Mhe Naibu Spika wa Baraza la
wawakilishi Zanzibar amepokea mapendekezo na maridhiano ambayo yatafikishwa kwa
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kama maoni katika kuandaa sheria mpya ya
vyama vya siasa.
Pamoja na wajumbe wengine muhimu waliohudhuria akiwemo Mhe
John Cheyo, Mhe John Shibuda, Mhe Suzan Lymo, pamoja na wengine wengi
wamekubaliana kuandaa kikao kupitia ULINGO ili kukutana na viongozi wote wa
vyama vya siasa katika kueleza maoni yao.
1. Kutaka Sheria Mpya Kutoa Maelekezo Kwa Katiba Za Vyama Vya Siasa Kutambua Nafasi Za Usawa Wa Jinsi Katika Nafasi Na Vikao Muhimu.
2. Kutaka Sheria Mpya Iwatambue Kikatiba Nafasi Za Usawa Kwa Wanawake (Kuwe Na Deliberate Clause)
3. Wajumbe Wameomba Vyama Vya Siasa Vipunguziwe Nguvu Ili Kuwa Na Taasisi Imara Ambazo Sio Za Kisiasa
4. Wajumbe Pia Wamelaani Vikali Matumizi Ya Lugha Zisizo Na Staha Zinazoendelea Katika Majukwaa Ya Kisiasa Na Kusema Kwamba Huo Sio Utamaduni Wetu Wa Siasa
No comments:
Post a Comment