Matokeo chanyA+ online




Thursday, April 5, 2018

WAFANYABIASHARA WADOGO WAANZA KUPEWA VITAMBULISHO VYA TRA

WAFANYABIASHARA WADOGO WAANZA KUPEWA VITAMBULISHO VYA TRA


UZINDUZI WA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA
WAFANYABIASHARA WADOGO

27 Machi, 2018 - Dar es Salaam.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), 
imezindua rasmi utoaji wa vitambulisho vya
Wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta 
isiyo rasmi ikiwa ni pamoja na Wamachinga.

Utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara 
hao unatokana na marekebisho ya Sheria ya 
Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 yaliyofanywa na 
 Kikao cha Bunge la Bajeti la Mwaka wa 
Fedha 2017/2018 ambapo moja ya marekebisho
 hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho 
maalum wafanyabiashara wadogo walio kwenye 
sekta isiyo rasmi.

Zoezi hili linatekelezwa na Mamlaka ya Mapato 
Tanzania  kwa kushirikiana na Mamlaka ya
 Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Tawala za Mikoa na
 Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa Usajili, 
Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na Idara ya Uhamiaji.

TRA kwa kushirikiana na wadau husika hapo juu, 
ilianza kutekeleza jukumu hilo kwa kuutambua Umoja wa 
Wamachinga wa Kariakoo jijini Dar es Salaam na 
kufanikiwa kuwapatia vitambulisho vya Taifa na 
Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) 
ambapo leo hii baadhi yao wamepatiwa vitambulisho 
maalum vya wafanyabiashara wadogo kama ishara ya
 uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho hivyo.

Baada ya mafanikio haya, zoezi la kutambua vikundi 
mbalimbali vya wafanyabiashara wadogo na kuwapatia 
kitambulisho cha Taifa na Namba ya Utambulisho wa 
Mlipa kodi linaendelea kufanyika nchi nzima.

Aidha, Ili wafanyabiashara wadogo waweze kupata 
vitambulisho hivyo maalum wanatakiwa:-
  • Kujiunga katika vikundi maalum vinavyotambuliwa 
    kisheria na Serikali,
  • Kuwa na Kitambulisho cha Taifa,
  • Kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi ya
     kikundi alichojiunga nacho na
  • Kuchangia shilingi 10,000/=.
Vitambulisho hivyo maalum kwa wafanyabiashara 
wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi vitadumu na 
kutumika kwa kipindi cha miaka mitatu (3) 
na vitakuwa na maelezo ya 
mfanyabiashara husika kama vile:-
Jina na picha ya mfanyabiashara,
  • Jina la eneo analofanyia biashara,
  • Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi na
  • Sahihi ya mfanyabiashara.

Imetolewa na:
Charles E. Kichere
KAMISHNA MKUU
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Pamoja naye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (mwenye miwani) na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Kodi, Dina Kaka jinsi ya kuandaa risiti ya kitambulisho cha Mfanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi Mfanyabiashara Mshamu Nakukwa kitambulisho wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018.  
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo.  
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kulia (kwake) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, Kamshna wa Kodi za Ndani, elijah Mwandumbya na Naibu Kamishana wa Kodi za ndani, Abdul Zuberi. 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Pamoja naye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (mwenye miwani) na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi Mwenyekiti wa Wafanyabiashara (Machinga) Steven Lusinde kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. (Imeandaliwa na ROBERT OKANDA BLOGS)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na baadhi ya wafanyabiashara wakati uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) kwa wafanyabiashara (Machinga) Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto (kwake) ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. 
Sehemu ya wafanyabiashara (Machinga) wakishiriki katika uzinduzi huo.  
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Kodi Msaidizi, Mordekai Kibona jinsi ya kuandaa kitambulisho cha Mfanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara (Machinga) Steven Lusinde akiongea kushukuru TRA na Serikali kwa ujumla kwa kuwatambu na kuahidi kutoa ushirikiano kwa serikali kwani imedhihirisha inawajali na kuthamini mchango wao kwa maendeleo ya nchi. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo, viongozi wa Machinga, Manispaa ya Ilala na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo, viongozi wa Machinga na Manispaa ya Ilala. 

Le gouvernement de la Tanzanie veut que l'exercice de l'impôt soit simp...

"Le gouvernement de la Tanzanie veut que l'exercice de l'impôt soit simplifié et effectué de manière civile. Nous nous attendons à ce que tout le monde sache que payer les taxes appropriées est un devoir noble de tout citoyen respectueux des lois. "" "Le président de la République-Unie de Tanzanie J. P. Magufuli. Mars 2018.

Monday, March 19, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Sehemu ya Viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Viongozi wa wa taasisi mbali mbali katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Ujumbe wa Umoja wa nchi za Ulaya (EU) katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) .Geoffrey Mwambe,  alipowasili kushiriki katika  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Kulia kwake ni   Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel 
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  alipowasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. 
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu  na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  akijiandaa kufungua  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  
 Sehemu ya Mawaziri, Wabunge na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Mhandisi Raymond Mbilinyi  akisoma risala yake katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  akisoma muhtasari wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Maonda akitambulishwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Viongozi wa wa taasisi mbali mbali na wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
Makatibu wakuu wakitambulishwa lishwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Viongozi wa taasisi mbalimbalui wakitambulishwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
  Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
  Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
  Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018 
  Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiipongezwa baada ya kuongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  
 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendesha  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  
  Viongozi wa taasisi mbalimbalui wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
  Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu  na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  akijiandaa kufungua  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.  
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
 Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018
Wafanyabiashara wakitoa changamoto zao wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. Pic ha na IKULU

Wednesday, March 14, 2018

USAJILI WA WATAALAM WA MAFUTA,GESI WAENDELEA KUFANYWA NA TaESA


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TaESA Boniface Chandaruba


*Ni kwa ajili ya kupata kazi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta Tanzania-Uganda

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania(TaESA) umetangaza kuanza kwa mchakato wa utambuzi wa Watanzania wenye taaluma na ujuzi katika sekta ya mafuta na gesi ambapo mwisho wa usajili ni Machi 30 mwaka huu.

Mchakato wa utambuzi huo ni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga nchini.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Boniface Chandaruba amesema kuwa ili kuhakikisha Watanzania wengi wananuifaka na fursa za ajira zitokanazo na mradi wa bomba la mafuta TaESA imepewa jukumu la kuhamasisha wote wenye taaluma na ujuzi nchini katika sekta ya mafuta na gesi wajitokeze.

“Hivyo tunaomba Watanzania wenye sifa kuja kujisajili TaESA ili waweze kuingizwa kwenye kanzidata ya Wakala kwa lengo la kuiwezesha Serikali kubaini idadi halisi ya walio na sifa zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi wa ujenzi wa bomba hilo.

“Usajili huu unafanyika bure ,hivyo tunasisitiza hakuna gharama yoyote itakayotozwa kwa Mtanzania yeyote atakayehitaji kusajiliwa.Maelezo ya kina kuhusu aina ya fursa za ajira zinazotegemewa kutolewa yanapatikana katika tovuti ya Wakala ya www.taesa.go.tz,”amesema .

Chandaruba amesema mchakato wa usajili unafanyika kwa kujaza fomu maalum ambazo zinapatikana kupitia tovuti ya Wakala au kwa kufika kwenye ofisi zao za kanda zilizopo Dar es Salaam,Arusha, Dodoma na Mwanza.Pia amesema fumu hizo zinapatikana kwa barua pepe eacop@taesa.go.tz na kwamba mchakato wa usajili unatarajia kumalizika Machi 30 mwaka huu.

Ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia Watanzania wote kuwa watumishi wa TaESA ni wanazingatia maadili ,hivyo hakuna rushwa ya aina yoyote kwa mtanzania ambaye anataka kujisajili.Kuhusu idadi ya ajira ambazo zitapatikana kwenye mradi huo, Chandaruba amesema unategemewa kuzalisha ajira 10,000 wakati wa ujenzi na ajira zaidi ya 1000 wakati wa uendeshaji wake.

Amesema kuwa mradi wa ujenzi wa bomba hilo la kusafirisha mafuta ni moja ya mradi mkubwa kutekelezwa hapa nchini na unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 3.5 sawa na Sh.trilioni 8.“Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,445 ambapo ujenzi wa kilometa 1,115 za bomba utafanyika nhini Tanzania.Jumla ya Wilaya 24 na vijiji 184 hapa nchini vinategemewa kupitiwa na bomba hilo katika mikoa nane,”amesema.

Ametaja mikoa hiyo ni Kagera, Geita, Shinyanga,Tabora,Singida,Dodoma,Manyara na Tanga.Amefafanua licha ya bomba kupita kwenye maeneo hayo lakini ajira zitatolewa kwa Watanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Alipoulizwa kama ndio wanatangaza sasa au walishatangaza siku za nyuma kuhusu watanzania kujisajili , amejibu kuwa ujenzi wa bomba hilo umekuwa ukizungumzwa kwa nyakati tofauti na hivyo kila eneo limekuwa likitangaza, lakini wao ambao ndio wakala wa ajira nao wanayo nafasi ya kuufahamisha umma.

Hivyo siku 16 ambazo zimebaki zinatosha watu kujisajili hasa kwa kuzingatia teknolokia ya habari na mawasiliano imerahisisha na kufafanua tayari wananchi walishaanza kujaza fomu na kuzipeleka kwenye wilaya na mikoa na sasa wanaotuma maombi hayo watajua wenye jukumu hilo ni TaESA.

Kuhusu TaESA amesema walianza kutoa huduma mwaka 2008 ambapo moja ya majukumu yake ni kukusanya,kuchambua na kusambaza taarifa za soko la ajira, pia kuendesha mafunzo kwa watafuta kazi ili kuwajengea uwezo na mbinu za kutafuta kazi na kuajirika.

Amezungumzia changamoto ya soko la ajira duniani, na kutumia nafasi hiyo kuwashauri wasomi nchini kuwa kutumia elimu ambayo wameipata kujiajiri na hatimaye nao kutoa ajira kwa wengine na kuongeza jukumu la Serikali ni kuandaa mazingira mazuri ya kuwawezesha Watanzania kujiajiri.

Amesema kwa mwaka idadi ya wasomi wanaohitimi vyuo vikuu ni 600,000, hivyo kwa idadi hiyo unaweza kuona soko la ajira serikali halitoshi, hivyo ni vema jamii ikaanza kubadili fikra kwa kutambua badala ya kusubiri ajira serikalini wakatumia elimu wanayoipata kujiajiri.