Matokeo chanyA+ online




Sunday, December 2, 2018

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI PAMOJA NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA WAFUNGUA KITUO CHA KUTOA HUDUMA KWA PAMOJA MPAKANI NAMANGA







FacebookTwitterGoogle+Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiwa wameshikana mkono wakati wakimwagia maji mti mara baada ya kuupanda wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipanda mti mara baada ya mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipata maelezo ya kituo hicho cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipungia wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano pembezoni mwa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakifurahi nyimbo zilizokuwa zikipigwa na bendi ya polisi katika hafla ya ufunguzi wa vituo hivyo vya mpakani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakizungumza jambo jijini Arusha kabla ya kupanda gari kuelekea Namanga mpani mwa Tanzania na Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi funguo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea funguo kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na watoto wawili kutoka Kenya waliofika kumpokea katika kituo cha kutoa huduma kwa pamoja kwa upande wa Kenya.
Baadhi ya Wananchi wa Kenya na Tanzania waliohudhuria katika hafla ya ufunguzi wa Vituo hivyo Mpakani Namanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea upande wa mpaka wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa kituo cha kutoa huduma kwa pamoja kwa upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na   Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea kupanda gari moja kutoka Arusha mjini kuelekea Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wanachi wa Kenya na Tanzania katika eneo la Mpakani Namanga mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia wanachi wa Kenya na Tanzania katika eneo la Mpakani Namanga mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa kupiga picha za pamoja mara baada ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Oldonyo Sambu Wilayani Arumeru wakati akitokea Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Oldonyo Sambu Wilayani Arumeru wakati akitokea Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya. 
PICHA NA IKULU 

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI MKUTANO MKUU WA 20 WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA.NOVEMBA 30,2018






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museven kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018

Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika kikao chao cha ndani kabla ya kuanza kwa mkutano mkuu wa 20 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha(AICC) .Novemba 30,2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya Kikao hicho cha 20 cha Wakuu wanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wa Uganda mara baada ya kikao cha cha Ndani cha cha 20 cha Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kikao cha cha Ndani cha 20 cha Wakuu wanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kikao cha cha Ndani cha 20 cha Wakuu wanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungungumza jambo katika kikao chao na Wakuu wanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kushoto ni Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kikao chao pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Ikulu ndogo ya Arusha. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kikao chao pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika Ikulu ndogo ya Arusha. 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. Picha na Ikulu
PICHA NA IKULU

Thursday, November 29, 2018

KASI YA SERIKALI YA JPM KWENYE KOROSHO; SASA VIWANDA VYAAMKA.

KOROSHO-7
Korosho ikiwa tayari kwa kusafirisha
  • Tanzania ni mmoja wa wazalishaji wakuu zaidi wa korosho katika Afrika, mauzo ya karosho ya Tanzania huchangia asilimia kumi na tano ya fedha za kigeni.
  • Tanzania ni mkulima wa 8 mkubwa zaidi duniani na wa 4 katika Afrika.
  • Takwimu iliyotolewa mwaka 2012 na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Tanznaia imekuwa imefanya vizuri katika uzalishaji wa zao la korosho tangu kabla ya uhuru, hata hivyo, udhibiti mbaya na ukosefu wa malipo ya kuaminika kwa wakulima wamesababisha uzalishaji wa korosho kutokuongezeka.
  • Kwa kawaida mmea hupandwa katika mikoa ya kusini ya pwani, Mtwara, Kilwa na Dar-es-Salaam. Uuzaji wa korosho huendeshwa na Bodi ya Korosho ya Tanzania, kwa njia ya ushirika mbalimbali wa wakulima.
  • Zaidi ya asilimia tisini ya mauzo ya nje ni nchini India, Ukosefu wa makampuni ya ubanguaji wa wa korosho ha Tanzania, umezipa faida kubwa nchi za kigeni kwa kuzalisha maelfu ya kazi kupitia korosho zinazotoka Tanzania.
  • Serikali imekuwa ikijitahidi kupata wawekezaji wenye uwezo wa kufufua sekta ya ubanguaji wa korosho bila ya manufaa.
KOROSHO-3
Wafanyakazi wa kiwanda cha TERRA CASHEW PROCESSING TANZANIA LTD kilichopo Kibaha Mkoani Pwani wakibagua korosho.
  • Historia 
  • Historia ya pato la kitaifa la zao la korosho, uliongezeka mwaka wa 1973, wakati pato la jumla lilizidi tani 145,000.
  • Sekta ya korosho ilianguka karibu miaka ya 1980. Uzalishaji wa kila mwaka ulikuwa umeanguka chini ya tani 20,000 mwaka 1986. Hii ilikuwa hasa kutokana na hatua mbalimbali za serikali katika mchakato wa mavuno na masoko.
  • Programu ya Ujamaa ilifanya mabadiliko ya kilimo kutoka na mazao ya biashara na kuanzisha mazao mbadala.
  • Zaidi ya hayo, kuhamishwa kwa wingi wa watu na kukusanywa katika vijiji vya ujamaa wakati wa miaka ya 1980 iliwawezesha wakulima wengi kuacha sehemu kubwa na maeneo ya mazao ya biashara kama korosho.
  • Kupungua kwa viwanda vya usindikaji wa mbegu pia vilichangia matatizo makubwa ya sekta ya korosho kwani taasisi hizi za serikali zilipotezwa na kushindwa kusimamiwa.
  • Mageuzi ya kiuchumi yalianza kuchukua kasi baada ya kufufua sekta ya usafirishaji wa bidhaa ghafi. Kumekuwa na ahueni ya ajabu tangu miaka 10 kutoka mwaka wa 1990-1999, uzalishaji wa korosho umeongezeka kutoka tani 29,000 hadi tani 120,000.
KOROSHO-4
Wafanyakazi wa kiwanda cha Terra Cashew kilichopo Kibaha Mkoani Pwani wakibagua korosho.
  • Hii ilisababisha pato la zaidi ya dola za Kimarekani milioni 100 Tanzania,
  • Mafaniko haya yalitokana na kuimarishwa kwa sheria za awali zilizotolewa na serikali ambazo zimezuia uuzaji wa korosho ghafi.
  • Lengo likiwa ni kuimarisha Shilingi ya Tanzania iliyoanguka dhidi ya dola kwa kuuza nje zaidi na kufaya uwekezaji mpya katika sekta binafsi iliyoongeza mapato ya wakulima.
  • Wakulima pia walianza kulipwa kwa muda na kuongezeka kwa pato kubwa lilikuwa kizuizi kikubwa kilichowazuia wakulima wadogo hapo awali.
KOROSHO-2
Korosho ikiwa imepakiwa vizuri tayari kwa kusafirisha
  • Kupanda Zaidi ya asilimia themanini na tano ya wakulima ni wakulima wadogo wadogo na wana wastani wa ukulima wa hekta 1. Wakulima wengi ni wazee na wanategemea kazi ya mikono badala ya mashine.
  • Vijana wengi kutoka maeneo ya vijijini wanapendelea kuhamia maeneo ya mijini kwasababu kilimo cha korosho hakijawekewa mazingira mazuri ya kuwavutia.
  • Ukosefu wa uwekezaji mpya katika mashamba ya korosho umesababisha miti minngi kuwa na mkubwa na kashamba mengi ni ya kale sana na yamekuwa yakipunguza mavuno zaidi kila mwaka.
  • Uzalishaji kuu iko katika sehemu ya kusini mwa Tanzania na Mtwara kuchangia asilimia 70 ya pato la kitaifa mwaka 2011. Sehemu nyingine kubwa ni Lindi (18%) na Pwani (8%). Kuna baadhi ya mashamba madogo na mashamba kote Tanznaia Ruvuma (4%), Tanga (1%), Iringa na Dodoma.
  • Tanzania ina faida ya ushindani kwenye soko la kimataifa, hata hivyo, tanzania imejipanga kuimarisha rasilimali hii ya Korosho.
  • Wakati wa mavuno korosho ya Tanznaia inauzwa wakati bei za soko ni za juu. Aidha, Tanzania ina korosho kubwa zaidi na ina maeneo makubwa ya kulima Korosho
  • Mwaka 2010 shamba la wastani lilizalishwa zaidi ya tani 1 kwa hekta. Mnamo Julai 2014, waziri mkuu wa zamani wa Tanzania, Mizengo Pinda, alisema kuwa serikali itatumia $ 72,000,000 na kufufua mimea aina nne ya uzalishaji kusini mwa Tanznaia.
  • Mimea iliyowekwa kwa ajili ya ukuzwaji iko katika miji ya Newala, Masasi, Lindi na Nachingwea. Mimea mpya itaongeza uwezo wa uzalishaji wa korosho nchini Tanzania kwa tani 29,500.
  • Takwimu za kuuzwa korosho za Tanzania ni nchi ya India (83%) Marekani (5%) United Arab Emirates (4%) Kenya (2%) Nyingine (6% )
KOROSHO-1 Faida za ajabu 15 za Korosho ya Tanzania
  • Korosho ya Tanzania huimarisha na kukupa moyo wenye afya, ujasiri, nguvu na kuimarisha misuli ya moyo kukuepusha na kupanuka kwa moyo,
  • Korosho ya Tanzania ina msaada mkubwa katika kuundwa kwa seli nyekundu za damu,
  • Korosho ya Tanzania inakupa afya bora ya mfupa na mdomo.
  • Pia Korosho ya Tanzania huina msaada mkubwa kuepukana na ugonjwa wa kisukari, upungufu wa damu, na vidonda vya tumbo. Kwa kutoa ulinzi wa antioxidant, pia huhamasisha mfumo bora wa kinga ya mwili.
  • Korosho ya Tanzania inalishe bora sana na inakupa nguvu na protini na madini muhimu ikiwa ni pamoja na shaba, kalsiamu, magnesiamu, chuma, fosforasi, potasiamu, zinki na Sodiamu ingawa iko kwa kiasi kidogo.
  • Korosho ya Tanzania pia ina vitamini C, vitamini B1 (thiamin), vitamini B2 (riboflavin), vitamini B3 (niacin), vitamini B6, folate, vitamini E (alpha-tocopherol), na vitamini K (phylloquinone).Korosho ya Tanzania ni chanzo cha asidi ya oleic na hutoa kiasi kikubwa cha mafuta yenye kiasi kidogo cha polyunsaturated bila cholesterol hatari ikiwa itztumiwa ipasavyo.
  • Korosho ya Tanzania ya huzuia Magonjwa ya Moyo, Korosho ya Tanzania ni nzuri kwa moyo na husaidia kupunguza cholesterol mbaya (cholesterol LDL) ikiwa Korosho ya Tanzania itatumiwa kwa kiasi sahihi inakinga hata ugonjwa wa kisukari. Cholesterol LDL inaweza kuongezeka kutokana na matumizi ya mafuta mengi yaliyojaa, na kusababisha tishio kubwa kwa watu wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo kama vile atherosclerosis au ugumu wa mishipa.
  • Uchunguzi umeonyesha kwamba mafuta ya Korosho ya Tanzania hupunguza viwango vya cholesterol HDL, hupunguza viwango vya triglyceride, na pia hupunguza shinikizo la damu. Korosho ya Tanzania ni chanzo kizuri cha magnesiamu, ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa,
  • Korosho ya Tanzania inahusika katika kazi za kimetaboliki, huathiri shughuli za insulini na hudhibiti viwango vya sukari katika damu.
  • Ukosefu wa magnesiamu hubadilisha kimetaboliki ya kalsiamu na homoni zinazohusika na udhibiti wake. Uwepo wa kiasi cha chini sana cha sukari na hakuna cholesterol hatari katika Korosho ya Tanzania huwafanya kuwa salama wagonjwa wa kisukari! Hii husaidia hata kupunguza kiwango cha ugonjwa wa kisukari cha aina 2.
  • Utafiti umeonyesha kwamba utajiri wa antioxidants unaopatikana katika Korosho ya Tanzania kama asidi anacardic, kadianols, na kadiols, huwafanya wagonjwa wenye uvimbe wa kansa kuwa na nafuu na hata kuponya.
  • Korosho ya Tanzania hutoa fosforasi, ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya afya ya meno na mifupa. Fosforasi pia husaidia katika protin, hutunza ngozi na kiasi cha wanga na mafuta Korosho ya Tanzania ni chanzo cha chuma na chakula ambacho ni muhimu kwa kubeba oksijeni na kuzunguka mwilini, ina msaada mkubwa katika utendaji wa enzymes na mfumo wa kinga ya mwili.
  • Ukosefu wa chuma katika chakula unaweza kusababisha uchovu, anemia, na upungufu wa damu.
  • Korosho ya Tanzania ina zinc, ambayo ina jukumu muhimu katika kuimarisha mfumo wa kinga dhidi ya maambukizi ya microbial, protini, na uponyaji wa majeraha. Ni muhimu sana wakati wa ujauzito kwa ajili ya ukuaji wa mtoto na miaka ya maendeleo ya utoto kudumisha hali imara ya mwili wa watoto.
  • Korosho ya Tanzania huongezwa kwenye mboga mbalimbali na zisizo za mboga na vitu vingi vya chakula kama vile biskuti, na ice cream.
  • Mti wa Korosho ya Tanzania una hazina kubwa ya ya dawa.
  • Mafuta ya Korosho ya Tanzania ni kemikali muhimu kwa ajili ya kuhifadhia vyombo vya chuma kuepukana na kupata kutu.
  • Bibo la Korosho ya Tanzania ni bidhaa iliyopatikana wakati wa usindikaji na ni nyenzo zenye manufaa kwa matumizi ya viwandani Ni malighafi ambayo hutumiwa katika maandalizi ya madawa ya kulevya, kuulia wadudu, kutengeneza rangi, plastiki, resini, na kupambana na wadudu walao mbao.
  • Ganda la Korosho ya Tanzania lina asidi anacardiki katika inatumika kama antibiotic na hutumiwa katika kutibu jino, husaidia kurasisisha kupumua, kutibu ukoma, hutibu vidonda na matende (elephantiasis).
  • Jani la mti wa Korosho ya Tanzania linatumika kama dawa kwa ajili ya kutibu kuhara na msokoto tumboni.
  • Vilevile majani ya Korosho ya Tanzania hutumiwa kupunguza sukari katika damu na viwango vya shinikizo la damu.
  • Gome la mti wa Korosho ya Tanzania hutumiwa kuoshea mdomo na kutibu vidonda vya mdomo na kama dawa ya koo na homa.
  • Majani ya mti wa Korosho ya Tanzania, huchemshwa na maji, hutumikia kupambana na homa, kutibu uchungu wa uzazi na kutuliza maumivu ndani ya mwili.
  • Maji kutoka katika majani ya korosho ya Tanzania yakichanganywa na chumvi yanautajiri wa vitamini C na yanauwezo wa kupandisha kinga ya mwili.
  • Ganda la korosho ya Tanzania linatumika sana katika sekta ya vipodozi kutokana na uwepo wa antioxidants na hutumiwa katika maandalizi ya creams mbalimbali na shampoo ya kuoshea nyele.
  • Ganda la Korosho ya Tanzania lina asidi aina ya anacardiki inayosaidia kufungua mishipa ya damu kwenda kwenye ubongo ambayo ni antioxidant na husaidia kupunguza madhara ya rangi ya ngozi na kuzeeka pia kuondokana na kansa ya seli za mwili.
  • Matunda ya mti wa Korosho ya Tanzania hutumiwa kutibu mapunye kwa watoto wachanga na vidonda mdomoni.
  • Mafuta yaliyotokana na mbegu za Korosho ya Tanzania hutumiwa sana kwa kuponya visigino vilivyopasuka (magaga).
  • Mbegu za Korosho ya Tanzania vina vimelea
  • Vya kupambana na sumu na hutumiwa kwa kutibu kuumwa na nyoka.

Friday, October 12, 2018

Kongamano la pili la sekta ya Sanaa na Ubunifu Afrika Mashariki lafanyika Dar

Kongamano la Pili  la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji  (2nd Mashariki Creative Economy Impact Investment Conference) lenye kauli  mbiu ‘Haki Ubunifu ni mali, Nikopeshe’ llilokuwa la siku mbili Oktoba 11-12, 2018 limemalizika  huku wadau na Wabunifu mbalimbali kutoka Tanzania na Nchi za Afrika Mashariki wakipata kujadili changamoto katika sekta hiyo.
Awali akifungua kongamano hilo Oktoba 11,2018 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya uwekezaji Bwana Aritiside Mbwasi  ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Mhe. Charles Mwijage  amesema Sekta ya ubunifu ina umuhimu wake hivyo wadau wanatakiwa kuwaangalia kwa jicho la pili katika kuwasaidia wabunifu  ili kuendeleza mitaji yao  kwani ina umuhimu wake kwa sababu ndio inaleta biashara, huduma, bidhaa na teknolojia mpya.
Amefafanua kuwa, ni  jinsi gani ubunifu unaongeza ufanisi kwa namna ya kipekee  na ubunifu  huo unavyofanya kazi na kuachana na kazi za mazoea.
“Wabunifu wetu wanamawazo mengi.   Kwa mfano watumiaji wa Electroniki Media (digital) labda anaandaa program ya watoto  namna ya kusoma ‘online’  huo ni ubunifu.  Sasa changamoto  taasisi za kifedha wao wanaangalia  zaidi namna ada yao inavyoweza kurudi, lakini wazo au ubunifu huo aliofanya huyo msanii je Benki pengine wasiuone
..biashara inaweza kulipa kwa hiyo ni moja ya changamoto wanayokutana nayo wabunifu wengi nchini na kwingine kote hapa Duniani” ameeleza Aritiside Mbwasi.
Kwa hatua hiyo amebainisha kuwa, sekta hiyo inaumuhimu wake na mijadala ya kongamano hilo itakuja na hitimisho la kuwasaidia wabunifu namna ya kupata mitaji.
Aidha, amesema moja ya pendekezo pengine ambalo wadau hao wanatakiwa kuangalia ni namna ya kushirikiana na wawekezaji  wengine ambao tayari wao wana fedha  ama mtaji ili kuingia ubia wa kuungana kwenye shea.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Maendeleo ya Afrika Mashariki  la  (Culture and Development  East Africa - CDEA),  Bi Ayeta Anne Wangusa amesema kongamano hilo lililoandaliwa kwa kushirikiano na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na kuwezeshwa  kwa msaada wa wadau wa OSIEA na British Council,  wanategemea wadau washiriki watakuja na majibu juu ya wabunifu kupata mikopo kutoka kwa wadau wenye mitaji.
Naye Mtaalmu na mtafiti wa kimaitafa  wa viwanda vya ubunifu,  Dkt. Keith Nurse, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la Dunia la Uchumi, kwenye  tasisi ya Sir Arthur Lewis Institute for Social and Economic Studies ndani ya chuo kikuu cha West Indies, amesema kuwa wabunifu wengi Duniani wamekuwa na matamanio ya maendeleo makubwa lichaya kukosa fursa tarajiwa kwa wakati.
 
Aidha, Dkt. Nurse ametoa mifano jinisi haki ubunifu imetumika kama dhamana ya kukopesha wabunifu kutoka nchi zilizoendelea na nchi  zinazoendelea.
Kongamano limeendesha mijadala mbalimbali kutoka kwa  watalum wa sheria, fedha, haki miliki na haki ubunifu, kutoka Afrika Mashariki.
Aidha, wadau mbalimbali wanaoshughulikia masuala ya haki miliki kutoka serekalini na  mashirika kama CISAC, wajumbe kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wizara zinahohusika na haki miliki toka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki,
Benki ya Maendeleo  Afrika Mashariki, Benki za kiuchuni, wawekezaji wa Afrika mashariki, mawakili wa haki miliki, vyombo vya hakimiliki vya Afrika Mashariki na wasanii mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wameudhuria kongamano hilo.
Mwisho.

Thursday, September 20, 2018

BARABARA MPYA ZA LAMI ZA MITAA YA MIKOCHENI NA MSASANI ZAONGEZA KASI YA KUKUZA UCHUMI JIJINI DSM.






Monday, September 17, 2018

NCHI YETU INASONGA MBELE... TUNACHAPA KAZI!



Maana #SisiNiTanzaniaMpyA+ yenye kupata Matokeo ChanyA+ 110% kwenye kila nyanja ya kukuza uchumi imara na madhubuti 








MFUGALE FLYOVER Yakamilika kwa asilimia 100


MFUGALE Flyover ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ya tarehe 17 Oktoba 2015 Ime...


Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 17 Octoba 2015 katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015, Dk Magufuli alifanya kampeni katika jimbo la Segerea, aliwaomba wakazi wa Dar es Salaam wampatie kura Oktoba 25 ili aweze kutekeleza miradi hiyo mikubwa itakayoenda sanjari na ujenzi wa barabara za juu zitakazopunguza foleni.
LEO AHADI IMETIMIA BAADA YA KUANZA RASMI KUTUMIKA KWA FLYOVER MPYA YA Eng. Patrick MFUGULE

Thursday, September 13, 2018

Tanzania ilivyoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara nchini Msumbiji


Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji (katikati), wengine kutoka kushoto ni ndugu Albert Philipo, Afisa wa Wizara kutoka Idara ya Diaspora (kushoto) na ndugu Nelson Nkini, Mwenyekiti wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Msumbiji  akikaribishwa katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 yanayojulikana kwa jina la FACIM yaliyofanyika tarehe 27 Agosti hadi 2 Septemba 2018 Maputo nchini Msumbiji. Ushiriki wa wafanyabiashara kutoka Tanzania uliratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
                                                                                                                 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Carlos Agostinho do Rosário wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 ya FACIM alipotembelea banda la Tanzania na kukaribishwa na Bi. Getrude Ngweshemi, Kaimu Meneja - Masoko ya Ndani wa TanTrade na Bw. Albert Philipo, Afisa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje ambapo alipatiwa maelezo kuhusu bidhaa za viwandani pamoja na vivutio vya utalii wa Tanzania. 
Balozi Rajabu Luhwavi akipokea maelezo kutoka kwa Afiisa wa Wizara, Bw. Albert Philipo kuhusu bidhaa za Tanzania zilizoletwa na wafanyabiashara mbambali kutoka Tanzania wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya 54 ya FACIM Maputo, Msumbiji. Wengine katika picha hiyo ni wafanyabiashara kutoka Kampuni mbalimbali nchini Tanzania.

Mheshimiwa Balozi Luhwavi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 ya FACIM mjini Maputo.
Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akiwa na Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi kushoto kwake wakikata utepe wakati wa kufungua Maonyesho ya Biashara Nampula tarehe 20 Agosti 2018. Maonesho hayo yalihusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na wenyeji wa Msumbiji. 
Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi akitoa maelezo mafupi wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara Nampula yaliyohusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania. Kwa upande wake Balozi Luhwavi, alieleza kuwa maonesho haya ni ya kimkakati kwa ajili ya kukuza na kuimarisha umoja, mshikamano na mahusiano ya kiuchumi yaliyojengwa na waasisi wetu hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; hayati Sheikh Abeid Amani Karume, aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar na hayati Samora Moises Machel, aliyekuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Msumbiji. Maonesho haya yalifungua fursa za masoko kwa bidhaa za viwanda vya Tanzania pamoja na kuendeleza juhudi za utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kukuza uchumi, hususan uchumi wa viwanda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kilele cha maonesho ya bidhaa za Tanzania mjini Nampula akiwa pamoja na Balozi Rajabu Luhwavi na Katibu Mkuu wa Jimbo la Nampula, Bi. Veronica Langa wakipata maelezo kuhusu teknolojia ya kisasa ya ufugaji samaki kutoka kampuni ya Dokaman ya nchini Tanzania.
Kutoka kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Juma Ali Juma, Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara TanTrade, Bi. Anna Bulondo wakipata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya A- Z Textile Mills inayojishughulisha na utengenezaji nguo, vifaa vya plastiki, mifuko ya kuhifadhia mazao na bidhaa nyingine.

Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi