Matokeo chanyA+ online




Wednesday, December 18, 2019

WARATIBU WA MTUHA WATAKIWA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA TAKWIMU SAHIHI


Waratibu wa Mfumo wa Taarifa za Utoaji wa Huduma za Afya (MTUHA) nchi wametakiwa kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi za sekta ya afya  katika maeneo yao ya kazi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali.Dkt. Saitole Laizer akifungua kikao kazi cha waratibu wa mfumo wa taarifa wa ufuatiliaji wa huduma za afya wa mikoa na halmashauri unaofanyika chuo cha mipango jijini Dodoma 
Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali ambaye pia ni mkurugenzi wa mafunzo na rasiliamali watu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Saitole Laizer wakati akifungua  kikao kazi cha waratibu MTUHA wa mikoa na halmashauri Tanzania kinachofanyika jijina hapa.

Dkt. Saitole amesema kuwa Wizara imeboresha mfumo wa takwimu kulingana na mahitaji  ya sasa na zinaingizwa na kuchanganuliwa kwa kutumia program maalum ya kompyuta katika ngazi ya wilaya ijulikanayo  kama ‘District health information software-DHIS 2’, hivyo ana imani  watasimamia na kuratibu kwa umakini.
Waratibu hao wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani)  wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho.kinachofanyika chuo cha mipango Dodoma

Waratibu wa mfumo wa taarifa wa ufuatiliaji wa huduma za afya wakiwa kwenye makundi wakiandaa mpango kabambe wa utekelezaji
“Matarajio ya wizara ni kuwa takwimu  zinazopatikana kutoka katika program hii zitakuwa sahihi  na mtatengeneza  orodha ya kielekroniki ya vituo vya kutolea huduma  za afya  ili kusaidia  katika mipango na kutoa maamuzi katika Sekta ya Afya”.

Vile vile Dkt. Saitole aliwataka waratibu hao kuweka mipango kabambe ili kuhakikisha mrejesho wa zoezi la uhakiki  wa ubora wa takwimu za afya  uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali pamoja  na kutoa mafunzo ya mrejesho katika meza maalum zitakazoandaliwa ili kutoa msaada wa watumishi ambao wanahitaji kujifunza,kupata ufafanuzi au kuuliza na kupata majibu ya masuala ya MTUHA yanayowasumbua  katika maeneo ya kazi .
Mwenyekiti wa waratibu hao Dkt. Ally Msoke akitoa neno la shukrani wakati wa ifunguzi wa mkutano huo

Kaimu mkurugenzi msaidizi ufuatiliaji na tathimini kutoka wizara ya afya Tumainiel Macha  akiongea kwenye kikao kazi hicho

Picha ya pamoja ya watumishi kutoka wizara ya afya na OR-TAMISEMI na mgeni rasmi


Hata hivyo aliwataka waratibu hao kuhakikisha  halmashauri zinatenga fedha kwa ajili ya  MTUHA katika mpango kabambe wa  halmashauri(CCHP) na timu za  za afya za mikoa na halmashauri na Wadau wa Maendeleo wanashiriki kikamilifu katika kuimarisha  upatikanaji wa takwimu sahihi za Sekta ya Afya.

Mfumo wa taarifa za utoaji wa huduma za afya nchini umesaidia kuwezesha sekta ya afya kupata takwimu sahihi na kwa wakati zinazowezesha kufanya maamuzi sahihi katika kupanga na kutekeleza malengo yake ili hatimaye kufikisha huduma bora kwa wananchi kutoka asilimia 43 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 85 mwaka 2019. Na. Catherine Sungura, Dodoma

MIFUMO IKOLOJIA BORA INASAIDIA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI – BALOZI SOKOINE


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Faraja Ngereageza akiongea wakati akimkaribishaMgeni Rasmi kufungua warsha hiyo ya mafunzo kuhusu kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwakutumia mifumo ya ikolojia iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma
 
Mifumo ikolojia yenye afya ndio inaweza kutupatia huduma za uhakika kama chakula, maji safi na salama, kutuepusha na magonjwa, mafuriko, uharibifu wa ardhi na wakati huo huo kutuwezesha kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu kuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine ambaye alikua mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya mafunzo kuhusu kuhimili mabadiliko ya tabia Nchi kwa kutumia mifumo yaikolojia iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma.
 
Mgeni Rasmi katika warsha hiyo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki waliohudhuria warsha hiyo ya mafunzo kuhusu kuhimili mabadiliko ya tabia Nchi kwa kutumia mifumo ya ikolojia iliyoandaliwa na Ofisiya Makamu wa Rais na kufanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango Dodoma.
 
Alisema kuwa Kukosekana kwa huduma hizo kutapelekea kushindwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia (Sustainable Development Goals). Hivyo mradi huu umekuja wakati muafaka wakati pia Serikali ikiendelea kukuza uchumi katika njia endelevu.

“Kama mnavyo fahamu mabadiliko ya tabianchi yameleta athari mbalimbali kwenye mazingira yetu hapa nchini. Kati ya madhara hayo ni kuharibika kwa kanda za Ikolojia Kilimo (Agro Ecolojical Zones) ambazo kwa mujibuwa tafiti kanda hizi ziko saba. Tafiti zinaonyesha kwamba ni rahisi kuhimili (Adaptation) kuliko kukabili (Mitigation)”. Alifafanua Balozi Sokoine.
 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine ambaye ni mgeni Rasmiakiongea wakati wa ufunguzi wa Warsha ya mafunzo kuhusu kuhimili mabadiliko ya tabianchikwa kutumia mifumo ya ikolojia iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanyika katikaukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Meneja wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini Bwana George Kafumu akitoa maelezo mafupi kuhusiana na mradi huo pamoja na lengo warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanyika jijini Dodoma.


Akimkaribisha Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Bwana Faraja Ngerageza alisema kuwa warsha hiyo itawawezesha washiriki kufahamu zaidi kuhusiana na kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia mifumo ya ikolojia iliyopo vijijini.

Warsha hiyo ya mafunzo ya siku tatu imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia mifumo ya ikolojia vijini (EBARR). Mradi huu unatekelezwa na Ofisi yaMakamu wa Rais. Warsha hiyoimehudhuriwa na Washiriki kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, inafanyika katika ukumbi wa Mikutano wa chuo cha Mipango jijini Dodoma.
 
 
 

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MRADI WA VISIMA VIREFU PAMOJA NA UJENZI WA MADARASA SHULE YA MSINGI CHATO A-B MKOANI GEITA



Sehemu ya Madarasa ya Shule ya Msingi Chato A-Bkama yanavyoonekana mara baada ya ujenzi wake kukamilika.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akifungua moja ya mradi wa Kisima kirefu kilichojengwa katika Shule ya Msingi Chato A-B kwa ufadhili wa Emirates Red Crescent-UAE kwa usimamizi na Utekelezaji wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chato A-B Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waChato katika sherehe za Ufunguzi wa Madarasa yaliyojengwa kwa mchango wake Mhe. Rais Dkt. Magufuli pamoja na mradi wa Visima virefu vya Maji vilivyojengwa na Emirates Red Crescent-UAE kwa usimamizi na Utekelezaji wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini
Tanzania zilizofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chato A-B Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Msingi Chato A-B mara baada ya kufungua Madarasa pamoja na Ofisi zilizojengwa kwa Mchango wake mwenyewe katika shule hiyo ambayo alisoma elimu yake ya Msingi.
PICHA NA IKULU

WAZIRI KAIRUKI AIPONGEZA TIRDO KUSAIDIA WAWEKEZAJI WADOGO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki (kushoto) akitazama bidhaa ya nyama inavyochakatwa na kuwa soseji inayozalishwa na Kiwanda cha ORI Meat Product Ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019) na kujionea uzalishaji. Katikati ni Meneja Uzalishaji wa ORI Meat Product Ltd, Mitesh Dhokie.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki amelipongeza Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kwa kuweka msukumo na mkakati endelevu wa kuwaendeleza na kuwasaidia wafanyabiashara na wawekezaji wadogo nchini.

Akizungumza na Uongozi na Wafanyakazi wa Kiwanda cha kuchakata nyama cha ORI Meat Product Ltd leo Jumatano (Desemba 18, 2019), Waziri Kairuki alisema TIRDO imeendelea kutekeleza vyema majukumu kupitia shabaha iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika ujenzi wa viwanda unaochochea katika kukuza mnyororo wa thamani na kuleta tija iliyokusudiwa.
 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kariuki akizungumza jambo na Viongozi wa Kiwanda cha ORI Meta Product Ltd kinachochakata bidhaa ya nyama na kuwa soseji wakati alipofanya ziara yake katika Kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019). Kushoto ni Meneja Uzalishaji wa Kiwanda hicho, Mitesh Dhokie na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji, Goodluck Hussein.
Aliongeza kuwa msukumo uliowekwa na Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) ni kuhakikisha kuwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wanakuwa na fursa kuwa katika kukuza uchumi kwa kuwawezesha kujenga viwanda vidogo vidogo na kuchakata bidhaa zenye ubora.

‘’Niwapongeze TIRDO kwa kutambua wajibu wenu katika masuala ya utafiti na viwanda lakini pia kutoa eneo lenu lenye ukubwa square (mraba) mita 600-700 na ghorofa moja na kukodisha kwa kiwanda cha ORI na kwa msukumo huu tutaweza kuwasaidia wajasiriamali, wafanyabiashara na wenye viwanda vidogo kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa’’ alisema Waziri Kairuki. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki (kushoto) akitazama bidhaa ya nyama inavyochakatwa na kuwa soseji inayozalishwa na Kiwanda cha ORI Meat Product Ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019) na kujionea uzalishaji. Katikati ni Meneja Uzalishaji wa ORI Meat Product Ltd, Mitesh Dhokie.
 

Aidha Waziri Kairuki aliitaka TIRDO kuhakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu ili kuwafanya wafanyabiashara, wawekezaji na wajasiriamali wadogo wanaendelea kupata maeneo makubwa zaidi kupitia miradi yake hatua itakayowawezesha kuweza kuongeza mnyororo wa thamani ya uzalishaji na hivyo kuleta tija kwa taifa.

Waziri Kairuki pia aliipongeza Kampuni ya ORI Meat Product Ltd kutokana na juhudi na ubunifu mkubwa walioufanya katika kuchakata bidhaa za nyama kupitia soseji za ng’ombe na kuku, na kuongeza kuwa Ofisi yake itawasiliana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuona namna bora mauzo na uzalishaji wa bidhaa za kampuni hiyo.
 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kariuki akionja bidhaa ya nyama iliyochakatwa na kuwa soseji soseji inayozalishwa na Kiwanda cha ORI Meat Product Ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019) na kujionea uzalishaji. Kushoto ni Mfanyakazi wa Kiwanda hicho, Martha Gwali na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Goodluck Hussein.
 

‘’Ndani ya muda mfupi wa kipindi cha mwaka mmoja vijana hawa wa Kitanzania wameweza kuwekeza mtaji wa Tsh Bilioni 1.1, walianza na wafanyakazi 50 lakini sasa wapo 64 lakini pia wameweza kuongeza mnyororo wa thamani kupitia label (alama), vifungashio vya plastiki, wazalishaji wa kuku ambapo wajasiriamali wanaweza kuuza kuku katika kiwanda hiki’’ alisema Waziri Kairuki.

Akifafanua zaidi Waziri Kairuki aliitaka Kampuni hiyo kuendelea kupanua shughuli zake ikiwemo kuimarisha mtandao wa masoko ya ndani na nje ya nchi, ikiwemo soko la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na kuzalisha bidhaa zenye viwango na ubora unaostahiki.
 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki akitazama bidhaa ya nyama iliyochakatwa na kuwa soseji inayozalishwa na Kiwanda cha ORI Meat Product Ltd kilichopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo Jumatano (Desemba 18, 2019) na kujionea uzalishaji. Kushoto ni Mfanyakazi wa Kiwanda hicho, Martha Gwali.  (PICHA NA MAELEZO)

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO, Humphery Ndossi Ofisi yake imeendelea kufanya kazi na wawekezaji wa ndani kwa kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara zao, na miongoni mwao ni Kiwanda cha ORI Meat ambapo wamekuwa wakitoa msaada mbalimbali ikiwemo upimaji wa ubora wa bidhaa za kiwanda hicho.

Aliongeza kuwa TIRDO imeendelea kusimamia wajibu wa msingi wa majukumu yake kwa kuwasisitiza wafanyabiashara kuzingatia ubora wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini ili kuweza kuliepusha taifa na mlundikano wa bidhaa bandia na zisizo na ubora na kuzuia matumizi yake ili kulinda afya za wananchi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ORI Meat Product Ltd, Goodluck Hussein alisema Ofisi yake imeendelea kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Serikali na imeweza kuuza pakiti 1200-1500 kwa mwaka, jambo ambalo lilikuwa gumu kwa miaka ya nyuma kutokana na uwepo wa bidhaa nyingi za nyama kutoka nje ya nchi.
 

RAIS MAGUFULI AFUNGUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA CHATO PAMOJA NA KUZINDUA UJENZI WA KITUO CHA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wapili kutoka kulia waliokaa, Spika wa Bunge Job Ndugai watano kutoka kulia waliokaa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma wanne kutoka kushoto waliokaa pamoja na viongozi wengine wa Mkoa pamoja na viongozi wa Kidini mara baada ya kufungua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Chato.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Agustine Mahiga kuashiria ufunguzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma mara baada ya kufungua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato lililopo Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua eneo la Mapokezi katika jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Chato lililopo eneo la Mlimani Chato mkoani Geita mara baada ya kulifungua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Chato mara ya kufungua jengo la Mahakama la Wilaya ya Chato.
Moja ya Vyumba vya Mahakama hiyo ya Wilaya yaChato kama inavyoonekana pichani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa Kituo cha Jeshi la Zimamoto la Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Sehemu ya Jengo la Kituo cha Jeshi la Zimamoto naUokoaji cha Wilaya ya Chato kilichowekewa Jiwe la Msingi leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. PICHA NA IKULU 
 

RAIS DKT MGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA MSIKITI MKUU WA CHATO WA MASJID AL HUDA MJINI CHATO LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir akiangalia mchoro wa utakaavyoonekana Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda alipowasili kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti huo utaokuwa na uwezo wa kukaa waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje, ukiwa unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/- 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akisalimia wananchi akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe Job Ndugai wa Taasisi
ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir pamoja na viongozi wengine wa dini na serikali wa Mkoa wa Geita kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato leo. Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua
waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/=.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe Job Ndugai akisalimia wananchi akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir pamoja na
viongozi wengine wa dini na serikali wa Mkoa wa Geita kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato leo. Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/=.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir pamoja na viongozi wengine wa dini wa Mkoa wa Geita akifunua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato leo. Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/=
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato leo. Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/=
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri Mhe Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation Sheikh Shariff Abdulqadir pamoja na viongozi wengine wa dini wa Mkoa
wa Geita wakipata picha ya kumbukumbu baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti Mkuu wa wilaya ya Chato wa Al Huda mjini Chato leo. Msikiti huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa ndani na 6000 kwa nje kwa wakati mmoja, unajengwa kwa
ufadhili wa Taasisi ya Al-Hikma Foundation kwa thamani ya Shilingi 1.6bn/=
 

WACHIMBAJI GEITA WATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI SALAMA YA KEMIKALI

Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason (aliyesimama) akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wachimbaji na wachenjuaji wa madini ya dhahabu katika Mkoa wa Geita yaliyoanza leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita. Kushoto ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko na wengine kutoka kulia ni Meneja wa Maabara ya Kanda ya Ziwa, Bonaventura Masambu (wa pili kulia) na Meneja wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Redempta Samwel.
Na; Mwandishi wetu- Geita

MIRADI YA UJENZI IFANYWE NA WAKANDARASI WA NDANI - NAIBU WAZIRI MASAUNI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipowasili katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania tayari kwa hafla ya ufungaji Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza  Desemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam.



Na Abubakari Akida

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema Miradi yote ya Ujenzi itakayokuwa inatekelezwa ndani ya vyombo vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi sasa itafanywa na wakandarasi kutoka Jeshi la Magereza na Polisi ili kuweza kutumia vikosi kazi hivyo ambavyo vimesheheni wataalamu wa kada hiyo huku agizo hilo likienda sambamba na maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano kubana matumizi na kuokoa fedha nyingi za walipa kodi zilizokuwa zikipotea.

Masauni ameyasema hayo wakati akihutubia katika Sherehe za Kufunga Mafunzo ya Maafisa Ngazi ya Juu yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga jijini Dar es Salaam huku akiwaasa wahitimu hao kwenda kusimamia maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano katika maeneo yao ya kazi.

“Natumia fursa hii kutoa maelekezo kwa taaasisi zote zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi ni marufuku miradi ya ujenzi wa vyombo vilivyopo chini ya wizara kutafuta mjenzi au mkandarasi kutoka nje ya vyombo vyetu hii,inatakiwa tuanze kuvitumia vikosi hivi ili tuvijengee imani huko nje na imani yangu inaniambia uwezo huo tunao na tunaweza,Shirika la Uzalishaji mali lazima likiboreshe kikosi hicho cha ujenzi cha magereza ili mwakani kiweze kutoa gawio kwa serikali”

Akizungumza katika sherehe hiyo Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP Faustine Kasike alisema jeshi la magereza limeshaingia katika mkakati wa kujitosheleza kwa chakula ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli na tayari magereza kumi ya kimkakati yashaanza kutoa matunda huku akiweka wazi mkakati wa kuongeza vitendea kazi katika magereza hayo kumi ya kimkakati.

“Jeshi la Magereza sasa limejipanga kufanya maboresho makubwa ya kiutendaji na kiuendesahji ili kuweza kuendana na kasi ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli,moja ya sehemu inayofanyiwa maboresho ni sehemu ya mafunzo ili tuweze kuwa na ufanisi na kasi,kwahiyo kozi unayoifunga leo imeandaliwa kwa mtazamo huo na tuna hakika wahitimu hawa watakua chachu ya mabadiliko hayo” alisema Kamishna Kasike

Akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Wahitimu,mmoja wa wahitimu amesema mafunzo hayo yamewapa uweledi hasa katika kipindi hiki chakuchangia uchumi wa nchi ikiwemo kujitosheleza kwa chakula kwa Jeshi la Magereza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali ya Awamu ya Tano huku wakiahidi kutumia elimu waliyoipata kulibadilisha jeshi katika maeneo ya kazi watakayopangiwa.

Jumla ya wahitimu 115 wamehitimu mafunzo hayo ya Maafisa Ngazi ya Juu ambapo watapangiwa sehemu mbalimbali za kazi ili kwenda kuboresha utendaji katika maeneo hayo.Chanzo MichuziBlog

MAKAMU WA RAIS SAMIA ATEMBELEA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wazee wa Kijiji cha Moga Mpitile Wilaya ya Kaskazini (A) Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati alipotembelea kijiji hicho leo Disemba 18,2019.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wanafunzi wa Madrasa Mpitile katika Kijiji cha Moga Mpitile Wilaya ya Kaskazini (A) Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati alipotembelea kijiji hicho leo Disemba 18,2019.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO MHANDISI MATHEW MTIGUMWE ASHANGAZWA HALMASHAURI KUTOZA USHURU WA MAZAO YA MBEGU


Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe

Na Innocent Natai, TPRI, Arusha

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameshangazwa na kuwepo kwa baadhi ya halmashauri zinazotoza ushuru wa mazao ya mbegu,kitendo ambacho ni kinyume na maelekezo ya serikali na kinarudisha nyuma jitihada za serikali za kuhakikisha nchi inaongeza uzalishaji wa mbegu na kuacha kununua mbegu kutoka nje ya nchi.

Mtigumwe ameyasema hayo tarehe 17 Disemba 2019 wakati wa kikao cha utekelezaji wa tasnia ya mbegu hapa Nchini, ikiwemo kupitisha aina mpya za mbegu bora za mazao, kupitia changamoto za uzalishaji wa mbegu hapa nchini, Kilicho jumuisha ujumbe kutoka TARI (Tanzania Agricultural Research Institute), Ofisi ya hatimiliki za wagunduzi wa mbegu, Idara ya mazao, na Taasisi ya udhibiti ubora wa mbegu (TOSCI).

Wengine ni Chama cha Wafanyabiashara wa Mbegu Tanzania, Mwakilishi  kutoka Vyuo vikuu vya Kilimo, Maendeleo ya Mazao, Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), na Wakala wa mbegu za kilimo (ASA) uliofanyikia katika ukumbi wa mikutano TPRI Makao Makuu Arusha.

Amesema halmashauri kutoza ushuru kwenye mazao ya mbegu ni kosa kwani maelekezo ya serikali kuhusu suala hilo yalishatolewa na mbegu za kilimo ni tofauti na mzao ya chakula na biashara yanayo zalishwa, hivyo kufanya hivyo kunakwamisha adhma ya serikali ya kuhakikisha uzalishaji wa mbegu unaongezeka na taifa kuacha kununua mbegu kutoka nje.

Amesema serikali imejipanga kuhakikisha suala hilo linafanikiwa kwa kipindi kifupi ikiwemo kuwaondolea vikwazo wazalishaji wa mbegu na kuwatatulia kero mbalimbali zinazowafanya washindwe kuzalisha kwa wingi na  kuwataka wazalishaji wa mbegu kutoa nje kufanyia uzalishaji wa mbegu zao hapa nchini na kuacha ule utaratibu wa awali wa kuzalishia nje na kuja kuuza hapa nchini.

Aidha, amezitaka taasisi zote zinazohusiana na tasnia ya Mbegu kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ili kusaidia mkakati wa kitaifa wa uzalishaji mbegu  unatimia ikiwemo kuhakikisha wanatoa elimu kwa wakulima ya kutambua mbegu bora,mbegu zisizo bora,kanuni za mbegu bora ikiwemo kuacha kurudia mbegu kwa muda mrefu.

Ameitaka Taasisi ya Kudhiti Ubora wa Mbegu (TOSC) kuhakikisha inaongeza kasi ya ukaguzi na kubaini wauzaji na wasambazaji wa mbegu zisizo bora na feki au bandia na watakao bainika kuchukuliwa hatua ili kuwahakikishi wakulima usalama wa kilimo chao na kufanya tasnia ya  kukua na taifa kujitosheleza kwa mbegu zilizo bora. 

Kakao hicho kimeazimia kwa pamoja kupitisha aina mpya za mbegu bora za mazao takribani 40 ambazo ni za mazao ya Mahindi aina 10, Mpunga aina 2, Ulezi aina 1, Pamba aina 3, Mhogo aina 9, Alizeti aina 9 na Viazi vitamu aina 6.


WIZARA YA KILIMO YAJA NA MKAKATI KABAMBE WA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA MPUNGA-MHE HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) wakifatilia hotuba ya mhgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. 
Katibu Mkuu wa Wiziri ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa taarifa ya Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) wakati wa hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali imesema kuwa imekusudia kuimarisha utoshelevu wa chakula nchini, ili kuchangia utoshelevu wa chakula katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SADC), na kuwa  kinara wa soko la mchele katika Jumuiya za Kikanda.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 16 Disemba 2019 wakati akizindua Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (NRDS II) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St Gaspar Jijini Dodoma.

Ili kufikia azma hiyo, Waziri Hasunga amesema kuwa serikali imeweka kipaumbele katika malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora za mpunga ambazo zinastahimili ukame na kuhamasisha matumizi ya teknolojia bora za uzalishaji zitakazo himili mabadiliko ya tabia nchi na Kupunguza gharama za uzalishaji na kuweka mifumo bora ya udhibiti ili mchele wetu uweze kushindana kwa bei na ubora na michele inayotoka nje ya nchi.

Malengo mengine ni Kuimarisha mifumo ya uzalishaji na masoko hususani kwa wakulima wadogo ili kukifanya kilimo cha zao la mpunga kuwa endelevu na kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi; na Kuongeza eneo la kulima zao la mpunga katika maeneo ya umwagiliaji na yanayotegemea mvua.

Pamoja na mikakati hiyo muhimu kabisa ya kuimarisha zao la mpunga Pia amesema kuwa serikali imekusudia kuimarisha na kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na kuwajengea uwezo wakulima kuhusu usimamizi wa miundo mbinu hiyo.

Ili kufikia malengo hayo Waziri Hasunga amesema kuwa Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na wadau wa zao la Mpunga nchini itahakikisha inasimamia inaongeza eneo la uzalishaji wa mpunga kutoka hekta milioni 1.1 za mwaka 2018 hadi hekta milioni 2.2 ifikapo mwaka 2030; Kuongeza tija ya uzalishaji wa mpunga kutoka wastani wa tani 2.2 kwa hekta hadi kufikia wastani wa tani 4.4 kwa hekta ifikapo mwaka 2030; Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na kuhamasisha teknolojia za umwagiliaji zinazotumia maji kwa ufanisi na Kuongeza thamani ya zao la mpunga kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2030 ikiwa ni pamoja na kupunguza upotevu kabla na baada ya mavuno.

Kadhalika kuimarisha mifumo ya masoko na kilimo biashara; Kuongeza upatikanaji wa mbegu bora za mpunga pamoja na kuimarisha mifumo ya mbegu; Kuongeza upatikanaji wa mbolea kwa kuanzisha Viwanda vya kuzalisha na kuchanganya mbolea nchini ikiwa ni pamoja na mifumo ya masoko na usambazaji; na Kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, kuongeza thamani na kuboresha mifumo ya masoko na upatikanaji wa mitaji.

Waziri Hasunga amnetumia mkutano huo kuyasihi makampuni ya kimataifa ya JICA, HELVETAS, IRRI, RIKOLTO, BRiTEN, AGRICOM na Wadau wengine kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Mkakati huo ambao umeainisha viashiria chanya vya kuendeleza zao la mpunga; na hatimaye kuifanya nchi kuwa mzalishaji na soko kuu la mchele katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika.

Alisema kuwa pamoja na kukamilika kwa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mkakati wa Kuendeleza Zao la Mpunga (NRDS I) na kuonesha mafanikio makubwa, ni dhahiri kuwa bado kunahitajika kuongeza tija na uzalishaji zaidi. Hivyo hiyo ndio sababu iliyopelekea Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo kuandaa Mkakati wa Kuendeleza Zao la Mpunga Awamu ya Pili (National Rice Development Strategy Phase II - NRDS II) utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi (10) kuanzia Mwaka 2019/20 hadi Mwaka 2029/30.

Lengo kuu la Mkakati huo ni kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga, kuimarisha usalama wa chakula na lishe, pato la wakulima na Taifa kwa ujumla ifikapo Mwaka 2030.

Ameongeza kuwa Uandaaji wa Mkakati huo ni matokeo ya Mkutano Mkuu wa Coaliation for African Rice Development (CARD) uliofanyika Jijini Tokyo, Japani Mwezi Oktoba, 2018 ambao ulikuwa na malengo makuu mawili ambayo ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa CARD awamu ya kwanza kipindi cha mwaka 2008 hadi 2018 na kuona namna gani awamu ya pili ya Mkakati huo itakavyotekelezwa kwa kipindi cha  Mwaka 2019 hadi 2030.


Tuesday, December 17, 2019

Makala ya MGUU KWA MGUU Umuhimu wa Ofisi ya Afisa Mtendaji

WAZIRI HASUNGA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MAAFISA UGANI NA CHAMA CHA WAGANI NCHINI


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) uliofanyika Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) uliofanyika Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) uliofanyika Jijini Dodoma, tarehe 16 Disemba 2019. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali imekiagiza Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) kutumika kama chombo cha kuishauri Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za ugani hapa nchini pamoja na kuwa ni kiungo cha kuwaunganisha watoa huduma za ugani na wadau mbalimbali hapa Nchini.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa kauli hiyo tarehe 16 Disemba 2019 wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka (Annual General Meeting - AGM) wa Chama cha Wagani Tanzania (Tanzania Society of Agricultural Extension and Education - TSAEE) uliofanyika Jijini Dodoma.

Amekitaka chama hicho kusimamia weledi wa Maafisa ugani katika kutekeleza majukumu yao; pia kwa lengo la kuimarisha uhai wa chama amewataka wajumbe wa chama hicho kukutana mara kwa mara ili kujadili mafanikio na changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za ugani nchini na kutoa ushauri kwa Serikali namna ya kutatua changamoto hizo.

Pia amewataka Wajumbe, kwa kushirikiana na Viongozi wa Chama hicho kuongeza ubunifu katika kutafuta vyanzo vya mapato kwa ajili ya kuimarisha na kuendesha Chama huku akiwasisitiza kuwa wakati wa uchaguzi wahakikishe wanachagua viongozi makini watakao simamia na kuongoza Chama hicho ili kiwe imara na endelevu.

Kwa upande wa Maafisa Ugani, ili kuweza kuimarisha utendaji wa majukumu yao ya kila siku na hatimaye kuinua sekta ya kilimo nchini, Waziri Hasunga ameagiza kila Afisa Ugani kuwa na Daftari la Kilimo ambalo atalitumia kuweka kumbukumbu zote za muhimu kila atakapoenda kuwahudumia Wakulima.

Amesema kuwa pamoja na taarifa nyingine za msingi, Daftari hilo lioneshe orodha ya wakulima anaowahudumia, ukubwa wa mashamba yao na aina ya mazao wanayolima.

Ameongeza kuwa Afisa Ugani ni lazima awe na Mpango kazi utakaoonesha ni nini hasa amepanga kufanya kwa wakulima, ikiwa ni pamoja na kuainisha ratiba ya kazi kwa kipindi husika huku akitaka kila Afisa Ugani kuwa na mashamba ya mfano au mashamba darasa ambayo atayatumia kuwafundishia Wakulima katika Kata/Kijiji/Mtaa wake.

Kadhalika ameagiza kuwa Afisa Ugani ni lazima awe na Mwongozo wa kusimamia Huduma za ugani na kuhakikisha anausimamia ipasavyo pamoja na kufahamu kanuni au mbinu bora za kilimo cha mazao makuu yote yanayolimwa katika eneo lake.

Waziri Hasunga amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itaendelea kushughulikia changamoto kwa kutoa msukumo wa kutosha kwa ajili ya uendelezaji wa sekta hizo muhimu hususani kupitia Utekelezaji wa Programu mbalimbali ikiwemo Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II). 

Aidha, Amesema kuwa serikali pia itaendelea kushirikiana na Wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya Nchi ambao wanaonesha dhamira ya dhati ya kuungana na serikali katika kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati kupitia shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.