Matokeo chanyA+ online




Wednesday, June 10, 2020

MANISPAAYA SUMBAWANGA YANG’ARA KIMAPATO HUKU WAKIPATA HATI SAFI KWA MIAKA MITATU

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeendelea kung’aa kwa kuvuka malengo ya makusanyo ya mapato katika kipindi cha miaka miwli mfululizo huku ikiendelea kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo hali inayapopelekea halmashauri hiyo kupata fursa ya mikopo kwaajili ya miradi maalum ya kimkakati kwaajili ya kuongeza mapato ya halmashauri.

Wakati akitoa salamu zake katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo kuhusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alisema kuwa Halmashauri hiyo imeshindwa kuitumia fursa ya kupata mikopo nafuu kutoka OR – TAMISEMI ili kupata miradi ya kimkakati kwaajili ya kuongeza mapato ya halmashauri.


“Mmepata hati safi au inayoridhisha mwaka 2017/2018, mwaka 2018/2019 na mwaka 2019/2020 na mkiangalia kwenye makabrasha pale, hoja za CAG zilikuwa ni zile ambazo kwa lugha ya ‘Chemistry’ tungesema ni ‘Dilute’ yaani zile ambazo sio sumbufu, ndio ambazo zimebaki, hongereni sana, lakini pia waheshimiwa madiwani, mmekuwa na mshikamano sana na maelewano, hapa kuna madiwani mchanganyiko wa vyama tofauti lakini mmeweka pembeni vyama vyenu, itikadi zenu za kisiasa kule mkawa kitu kimoja kuisimamia halmashauri ya manispaa ya sumbawanga, hasa katika masuala ya kimaendeleo” Alisema.

Aidha, Mh. Wangabo alisifu juhudi za Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jacob Mtalitinya kwa kuisimamia vizuri halmashauri hiyo na kuongeza kuwa mambo yote yanayofanyika katika baraza la madiwani na kamati zake za kudumu yanategemea sana utekelezaji wa Mkurugenzi huyo ambaye pia hutekeleza maazimio ya mabaraza ya madiwani pamoja na kamati zake.

Pamoja na sifa hizo Mh. Wangabo alitoa masaa 24 kwa Mkurugenzi huyo kuhakikisha anawalipa madiwani deni la shilingi 33,243,194/= waliyokuwa wamekopa benki na kupaswa kurejesha kwani dhamana ya kurejesha ipo kwa Mkurugenzi ambaye anashughulika na posho za madiwani hao na namna wanavyokatwa katika benki walizokopa na hivyo Mkurugenzi asipolipa deni hilo litahamia kwa madiwani na hivyo kupata usumbufu kutoka kwa watu wa mabenki.

Kwa upande mwingine alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule kwa kutumia vyombo vyake ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rukwa (TAKUKURU) kuwachukulia hatua wadaiwa wote wa makusanyo ya halmashauri yapatayo shilingi 12,477,968/= kurudisha fedha hizo ndani ya siku sab ana wasipofanya hivyo wafikishwe mahakamani.

Mwaka wa Fedha 2018/2019 Makisio yalikuwa ni shilingi 2,212,104,000/= na kiasi kilichokusanywa kilikuwa shilingi 3,040,733,596.82/=  sawa na Asilimia 138, na kwa Mwaka huu wa fedha 2019/2020 Makisio ni Shilingi 2,432,510,000/= na hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2020 jumla ya shilingi 2,739,895,134.00  zimekusanywa sawa na Asilimia 113.

 

MWENYEKITI WA CCM DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR RAIS SHEIN MUDA MFUPI KABLA YA KUANZA KIKAO CHA KAMATI KUU


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM upande wa Zanzibar Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein muda mfupi kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Chamwino mkoani Dodoma

Tuesday, June 9, 2020

MATUKIO YA PICHA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA BUNGENI JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mwigulu Nchemba, Bungeni jijini Dodoma, Juni, 8, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, Bungeni jijini Dodoma, Juni, 8, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMJULIA HALI FREEMAN MBOWE HOSPITALI YA NTYUKA JIJINI DODOMA



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye amelazwa katika hospitali ya Ntyuka jijini Dodoma, kwa matibabu Juni 9, 2020. Mbowe anatibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu ambao bado hawajajulikana wakati akiingia nyumbani kwake jijini Dodoma usiku wa kuamkia leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI HASUNGA ATANGAZA MIFUMO MITATU UUZAJI WA KAHAWA, WANUNUZI BINAFSI RUKSA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza mikakati ya serikali kwenye zao la Kahawa wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya Kahawa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe uliofanyika katika ukumbi wa kanisa la Moravian Sala-Ichenjezya leo tarehe 9 Juni 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wadau wa sekta ya Kahawa wakifuatilia hotoba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza mikakati ya serikali kwenye zao la Kahawa wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya Kahawa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe uliofanyika katika ukumbi wa kanisa la Moravian Sala-Ichenjezya leo tarehe 9 Juni 2020.
Sehemu ya wadau wa sekta ya Kahawa wakifuatilia hotoba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza mikakati ya serikali kwenye zao la Kahawa wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya Kahawa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe uliofanyika katika ukumbi wa kanisa la Moravian Sala-Ichenjezya leo tarehe 9 Juni 2020.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Ili kukabiliana na changamoto ya uuzaji wa mazao mbalimbali ya wakulima nchini katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona serikali imetangaza na mifumo mitatu ya uuzaji wa kahawa.

Mifumo hiyo ni uuzaji wa kahawa kwa soko la moja kwa moja (Direct Selling), Mfumo wa kuuza kupitia minada ambapo vyama vya ushirika vitakusanya mazao kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani na mfumo wa tatu ni wakulima kuingia makubaliano na wamiliki wa viwanda vya ndani ya nchi vya uchakataji wa kahawa ili kuwauzia kahawa yao.

Serikali imewataka wakulima kutumia fursa hiyo ya uuzaji wa kahawa kwenye maeneo watakayoona kuna wanunuzi wenye bei nzuri lakini wauzaji hao wasiende moja kwa moja kwa wakulima badala yake wanunue kahawa kupitia kwenye vyama vya Ushirika.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 9 Juni 2020 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya Kahawa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe uliofanyika katika ukumbi wa kanisa la Moravian Sala-Ichenjezya.

Amesema kuwa serikali haiwezi kuzuia wanunuzi binafsi kwani biashara ya mazao na bidhaa zingine ni muhimu kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za nchi hivyo hivyo ushindani ni muhimu ili kuimarisha bei ya mazao ya wakulima.

Waziri Hasunga amesema kuwa serikali inazo taarifa za kutosha juu ya Afisa Ushirika wa Wilaya ya Mbozi Ndg Fredy Katoto kuihujumu serikali kwa kutotekeleza maagizo yanayotolewa na viongozi mbalimbali hivyo serikali itamchukulia hatua kali za kisheria mtumishi huyo kwani anawapotosha wakulima.

“Mtumishi wa Umma ambaye umeajiriwa unawadanganya wakulima, na wewe ndiye umekuwa tatizo kwenye kilimo chetu mnakaa huko mnapanga namna ya kulipa lakini hamlipi kwa maelekezo ya serikali taarifa tunazo, Kuna wakulima mpaka sasa hivi hawajalipwa fedha zao kwa sababu ya Katoto huyu nitamshughulikia” Alikaririwa Waziri Hasunga

Mhe Hasunga ameongeza kuwa hakuna Marais wawili katika nchi hii badala yake kuna Rais mmoja wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ambaye akitoa maagizo watumishi wengine wote wanapaswa kufuatwa na hawatakiwi kutoa maagizo mengine yoyote zaidi ya utekelezaji.

“Mimi ndio nimepewa mamlaka (Instument) inayoniambia natakiwa kutoa maelekezo ya namna ya kukisimamia kilimo nchini, Vyama vya Ushirika ni wanunuzi kama wanunuzi wengine kazi yenu ni kukusanya na kutafuta soko la mazao hivyo sitarajii kutoa maelekezo halafu kuna mtu ayapinge tena Mtumishi wa Umma” Amesema Mhe Hasunga

Katika usimamizi madhubuti wa sekta ya Ushirika nchini, Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga amesema kuwa ili kudhibiti wizi na ubadhilifu kwenye vyama vya Ushirika unaojitokeza mara kwa mara serikali imeamua kuja na mkakati wa kuwaajiri Mameneja wa vyama hivyo ili kusimamia na kudhibiti mali na fedha zote za wakulima.

Akizungumza kwa niaba ya wanunuzi binafsi wa kahawa Ndg Tikson Nzuda amesema kuwa wanunuzi hao wana fedha za kutosha za kununua kahawa yote ya wakulima hivyo wameiomba serikali kuwapatia leseni haraka iwezekanavyo ili waingie sokoni.

Ameongeza kuwa wanunuzi binafsi tayari wamekopa fedha kwenye Taasisi mbalimbali za kifedha zikiwemo benki lakini mpaka sasa hawajapewa kibali jambo ambalo ni hatari kwao katika mikopo hiyo.


Monday, June 8, 2020

MRADI WA MAJI LONGIDO WAMALIZA TATIZO - DK. MHINA


Tanki la maji lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido, ambalo linakusanya maji kutoka Mto Simba uliopo wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.


“Tangu Longido kuwa Wilaya mwaka 2007 haijawahi kuwa na huduma maji yanayotiririka kwenye nyumba za watu, yamekuwepo maji ya visima miaka yote, nampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitupatia fedha kiasi cha shilingi bilioni 15. 89 ambazo zimetekeleza mradi maarufu unaoitwa mto Simba, ambapo maji yanatoka Mlima Kilimanjaro sehemu ya umbali wa kilomita 63 hadi kufika hapa Longido”.

Hayo yanasemwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Longido, Dkt. Jumaa Mhina wakati akizungumza na Afisa Habari kutoka Idara ya Habari – MAELEZO na mwandishi wa makala hii, Immaculate Makilika alipokuwa ziarani huko mkoani Arusha hivi karibuni.

Dkt. Mhina anaendelea kusema kuwa maji yanapofika Longido kutoka Mlima Kilimanjaro yanahifadhiwa kwenye tanki kubwa na kusambazwa ndani ya mji wa Longido kwenye mtandao wa Km 44.7 kisha yanaenda katika Kata ya Engikaret umbali wa km 31kwa hiyo huu ni mradi mkubwa kuwahi kutokea na wa kihistoria.

“Hivi sasa tunavyozungumza, wananchi wanachota maji ya bomba kwenye nyumba zao, hiyo ilikuwa miujiza hakuna mtu ambaye aliamini kuwa jambo hili linaweza kutokea, lakini jambo hili limetokea”, anasisiza Dkt. Mhina.

Ni dhahiri kuwa mradi ulilenga kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji katika Mji wa Longido kutoka asilimia 15 ambayo ni sawa na wakazi 2,510 hadi kufikia asilimia 100 sawa na wakazi 16,712 kwa sasa. Kiasi hicho cha maji kimetosheleza mahitaji kwa asilimia 100 hadi kufikia idadi ya wakazi 26,145 kwa mwaka 2024.

Bi.Winnie Sangau mkazi wa Longido, anasema hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji, kwani iliwalazimu kwenda kuchota maji sehemu yenye umbali mrefu ambapo ni kwenye kituo kikubwa kilichokuwa kikitoa huduma ya maji mara moja tu kwa wiki tena ambayo hukatika saa nane alasiri, baada ya mradi wa mto Simba kuanza kutoa huduma ya maji hali hiyo imebaki historia ambayo hawatakaa kuisahau maishani mwao kwani yalikuwa mateso makubwa kwa akina mama ambao ndio walionekana na ndoo za maji kila uchao wakihaha kutafuta maji kama swala aliyenusurika kujeruhiwa na nyoka mkubwa!

“Ahaa! hivi sasa upatikanaji wa huduma ya maji ni rahisi, tunapata maji kwenye nyumba zetu na ambao hawajavuta mabomba katika nyumba zao wanachota kwenye vituo vilivyopo karibu na makazi ya watu na maji yanatoka kila siku, kwa kweli tunamshukuru sana Rais Magufuli kwani amebadilisha maisha yetu wakazi wa Longido”, anaongeza Sangau.

Mradi huu wenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha mita za ujazo 2,160 kwa siku wakati mahitaji ni mita za ujazo 1,462, umefungua fursa mpya za biashara katika wilaya hiyo muhimu ya Longido ambapo kwa upande wa kaskazini inapakana na nchi jirani ya Kenya, na hivyo suala la maji ni nyenzo muhimu kwa matumizi mbalimbali hasa wakati huu ambao ulimwengu unapamba na virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu huku wengine wakisema hii ni “vita ya tatu ya dunia”.

Akielezea namna ambavyo mradi huo wa maji ya mto Simba umebadilisha maisha ya wanalongido, mwalimu mstaafu, Bw.Charles Msangi anasema “Kwa sasa maji yanapatikana wakati wote usipohitaji unafunga, na hivyo sipati shida ya huduma ya maji hapa kwenye biashara yangu ya nyumba ya kulala wageni, namshukuru sana Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa kutukubalia huu mradi amefanya kitu kikubwa sana ambacho watu wa Longido hatutasahau. 
 
Wafugaji huko nyuma walipata shida sana kwani walikuwa wakienda kunywesha mifugo siku nzima na mara nyingine ng’ombe hulala huko huko , lakini kwa sasa hawaendi tena huko kwani watu wengi wana mabomba katika nyumba zao na sehemu za kunyweshea zimewekwa karibu na makazi ya watu”.

Halikadhalika miujiza ya Longido haikuishia kwenye maji tu, bali hata kwenye mifugo na ukusanyaji wa mapato, hali iliyobadilisha maisha ya wakazi wengi ambao ni wa jamii ya kimasai.

Awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa mnada wa mifugo ulipata fedha za utekelezaji kupitia ufadhali wa programu ya kuendeleza Miundombinu ya Masoko, Ongezeko la Thamani na Huduma za Fedha Vijijini (MIVARF) kwa asilimia 95 na Halmashauri ya Wilaya ya Longido ilichangia asilimia 5 ya gharama za mradi kwa awamu ya kwanza.

Utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya mnada wa mifugo ulianza rasmi Novemba 2016 na kugharimu shilingi 782,743,085.59/= ambapo MIVARF imechangia 95% sawa na shilingi 743,605,931.30 na Halmashauri ilichangia asilimia 5 sawa na shilingi 39,137,154.30.

Katika awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu ya mnada huu, Wizara ya Mifugo na Kazi hii ilitoa jumla ya shilingi 150,000,000/= ili kukamilisha ujenzi wake kazi. Hivyo jumla kuu ya gharama za mradi (awamu ya kwanza na awamu ya pili) ni shilingi 932,743,085.59.

Licha ya mradi huo kuwa na manufaa mbalimbali kama vile kuongeza uzalishaji wa mifugo na mazao ya mifugo kutokana na uwepo wa soko la uhakika la mifugo, kuboresha na kuinua kipato cha wananchi wa Wilaya ya Longido kwa kuuza mifugo ndani ya Tanzania na nchi jirani.

Faida nyingine ni ajira kwa vijana na wanawake, kurahisisha upatikanaji wa mifugo kwa ajili ya kiwanda cha nyama kinachojengwa upande wa pili wa eneo la mnada ambacho kitasindika mbuzi au kondoo 2,000 na ng’ombe 500 kwa siku, ikiwa ni pamoja na na kijiji cha Eworendeke kunufaika na mapato asilimia 10 kutoka eneo la mradi.

Dkt. Mhina anasema kuwa kwa mara ya kwanza katika nchi hii, Serikali imepata mapato makubwa kupitia mnada wa kuuza mifugo kwenda nchi jirani ya Kenya.

“Katika mnada huo tuna mifugo takribani 3,000 hadi 6,000 kulingana na msimu inavuka kwenda nchi ya Kenya, na mifugo hiyo imekuwa ikivuka bila Serikali kupata ushuru wa aina yoyote yaani export permit kwa miaka yote, lakini tulivyoanzisha mnada huu kwa kipindi cha mwaka huu pekee tayari Serikali imekusanya shilingi bilioni 1.2, na hivyo kiasi ambacho halmashauri inapata kwa mwaka kutokana na mnada huu ni shilingi milioni 400 na hivyo kuongeza mapato ya halmashauri ambapo inatusaidia kupeleka fedha katika miradi ya maendeleo pamoja na kulipa stahili“ anasema Dkt. Mhina.

Dkt. Mhina anaendelea kusema kuwa ili kuongeza mnyororo wa thamani licha ya kuwa na soko la kimataifa la mifugo, wilaya yake tayari imepata muwekezaji anayejenga kiwanda kikubwa kuchakata nyama katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambacho ambacho ujenzi wake utakamilika mwezi Julai mwaka huu.

Aidha, anaongeza, “Tunaamini kuwa kiwanda hicho kitakapoanza kufanya kazi, kitakuza uchumi wa wilaya yetu, na watu watafuga kwa tija, tumeshaongea na benki mbalimbali pamoja na vikundi zaidi ya 100 vya wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo na hivi sasa tumeanzisha SACCOS ya kununua na kuuza mifugo ili kiwanda kitakapoanza kazi watanzania wasibaki kuwa watazamaji“

Mmoja wa wawekezaji wa kiwanda hicho cha Eliya Food Overseas Ltd, Alshabir Mohamed anasema kuwa gharama za mradi huu ni jumla ya Dola za Kimarekani 5,000,000.

Ujenzi wa kiwanda hicho umefikia asilimia 80, na wanatarajia kiwanda hicho kuanza kazi ifikapo mwezi Julai mwaka huu, ambapo watapeleka nyama yao kwenye hoteli mbalimbali za hapa nchini pamoja na kusafirisha nje ya nchi.

“Kiwanda hiki kitatumia kila kitu kinachotoka kwa mnyama ili kutengeneza malighafi mbalimbali, ngozi zote zitapelekwa katika kiwanda cha ngozi Mororgoro, pia tutatengeneza chakula cha mifugo, mafuta yanayotoka kwenye wanyama yatatumika kutengeneza sabuni. Aidha, tutaajiri watu 3,000 ambao wengi wao watakuwa vijana“, anasema Mohamed.

Hakika mapinduzi yanayoendelea katika Wilaya ya Longido, ni dhahiri kuwa Serikali imedhamiria kuboresha maisha ya watanzania na kufikia azma yake ya nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025, sambamba na Tanzania ya viwanda.

MALIMA AIPONGEZA HALMASHAURI YA BUNDA KWA HATI SAFI


 Immaculate Makilika- MAELEZO

Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima, ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka wa fedha 2016/2017.

Akizungumza hivi karibuni wakati  wa uwasilishaji wa hoja za Mkaguzi na Mdhibiti  Mkuu wa  Hesabu za Selikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima  aliipongeza  Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kupata  hati safi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka wa fedha  2016/2017, 2017/2018 na 2018/2019.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima

“Halmashauri hii ni ya mfano katika mkoa wa Mara na ninawaomba msibweteke kwa vile mmepata mafanikio haya, bali muongeze bidii” alisema mkuu wa mkoa Malima

Aidha, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali katika  mkoa wa Mara, Patrick Lugisi alisema kuwa mafanikio hayo ni matokeo mazuri ya kazi wanayofanya watumishi wa Halmashauri ya mji wa Bunda.

“Ushirikiano na uwajibikaji  wa Menejimenti  ndio umepelekea Halmashauri hii  kuwa na hoja chache na kuwa na ufanisi, niziombe Halmashauri zingine kuiga mfano huu” alisema Lugisi.

Halmashauri ya mji wa Bunda ilianzishwa Mwaka 2015 na ilianza kutekeleza majukumu  yake Mwaka 2016. Hati safi kwa halmashauri hii imekuwa chachu ya kuongeza tija kwa watendaji wote na hivyo kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma bora zinazotolewa  katika sekta za afya, elimu, maji,miundombinu na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Sunday, June 7, 2020

TUNA USHIRIKIANO MZURI NA SERIKALI KWENYE UTEKELEZAJI WA HAKI ZA BIANADAMU - JAJI MSTAAFU MWAIMU


Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Ibrahim Mzee Ibrahim(wa kwanza kushoto)  akizungumza na ugeni wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora walipomtembelea  ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari na kufanya kikao kifupi kuhusu masuala ya haki za binadamu, kulia ni  Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu na Makamu Mwenyekiti, Mohamedi Khamis Hamadi.


Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema kuwa ushirikiano baina ya Tume hiyo na Serikali ni Muhimu ili kutekeleza majukumu ya kuwapatia wananchi haki inayohitajika katika masuala mbalimbali ya jamii.

Akizungumza katika Ziara aliyoifanya Ofisi ya Mkurugenzi wa  Mashtaka iliyopo Mjini Unguja, Zanzibari Jaji Mwaimu alisema kuwa tume ya haki za binadamu ni chombo cha serikali ambacho kipo kisheri kwa ajili ya wananchi kikilenga ukuzaji na ulindaji wa haki  kwa pande zote mbili.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu , Mohamedi Khamis Hamadi akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi,  ya Zanzibari ( hayupo pichani), kuhusu haki za binadamu walipomtembelea ofisini kwake Mjini Ungua, Zanzibari Juni 5, 2020., kulia ni Kamishna Mkazi wa Haki za binadamu na Utawala bora  kwa upande wa Zanzibari, Khatibu Mwinyichande na kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu

“Tume ni chombo cha Serikali ambacho kipo kisheria na majukumu yake ni kukuza na kulinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa Serikali na wananchi, tunafanya kazi ya kuisaidia Serikali maana yake pande zote mbili viongozi na wananchi kwa kushughulikia malalamiko  mbalimbali ya pande hizo”, Alisema Jaji Mwaimu.

Alisema kuwa lengo kuu la ziara ya kupita kila ofisi inayohusiana na masuala ya utekelezaji wa haki za binadamu ni kujenga mahusiano bora katika kitumiza azma ya kuiwezesha Serikali kujua mahali ambapo kuna ukiukwaji wa haki za binadamu ili iweze kutatua jambo hilo kwa haraka zaidi.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu.Mathew Mwaimu akizungumza na watendaji wa juu wa tume hiyo na Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Ibrahim Mzee Ibrahim, wakati wa kikao kifupi kuhusu haki za binadamu kilichofanyika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Mjini Unguja Zanzibari Juni 5, 2020.

Naye, Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Ibrahim Mzee Ibrahim alisema kuwa ataendelea kutoa ushirikiano kwa ofisi ya Tume hiyo kwa kuwa utekelezaji wa majuku yake unaendana na uwepo wa haki za binadamu.

“Majukumu ya ofisi yetu tunayoyafanya kila siku, mara nyingi yanahusiana sana na haki za binadamu kwa sababu mtu akikutwa na jinai yeyote moja kwa moja lazima haki yake iangaliwe na hukumu itolewa kwa kuzingatia sheria na haki za binadamu, kwa hiyo ushirikiano wetu na ofisi ya tume unahitajika sana na mimi nasema tutaendelea kutoa ushirikiano kwa ofisi yako”,  alisema  Ibrahim Mzee.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu.Mathew Mwaimu akikabidhi Mpango Mkakati wa tume hiyo  wa  2018/2023 kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibari baada ya kufanya mazungumzo mafupi kuhusu haki za binadamu, kikao hicho kilifanyika Ofisi za Mkurugenzi wa Mashtaka zilizoko Mjini Unguja, Zanzibari Juni 5, 2020


Aliongeza kuwa tume hiyo imepewa jukumu kubwa la kutekeleza na kuleta haki za binadamu, kwani imekuwa msaada mkubwa kwa Serikali na wananchi katika kulinda na kuweka hali sawa kwa malalamiko mbalimbali.


Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu.Mathew Mwaimu na Mkurugenzi wa Mashitaka Ibrahim Mzee Ibrahim pamoja na watendaji wa Tume hiyo baada ya kikao kifupi kuhusu haki za binadamu kilichofanyika katika Ofisi za Mkurugenzi wa Mashtaka Mjini Unguja Zanzibari Juni 5, 2020.

“Tume mumepewa jukumu zito, lakini naamini jukumu limefika kwenye mikono salama kwani mnakwenda vizuri na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano, na mumeleta heshima kwa tume hii na sasa inafanya kazi kwa manufaa makubwa ya wananchi na Serikali yao”, Alifafanua Ibrahim Mzee.

Kwa Upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mohamedi Khamis Hamadi alisema kuwa tume imeendelea kushirikiana vizuri na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibari katika kuleta haki kwa wananchi na aliomba kuwepo na mashirikiano mbalimbali yakiwemo ya mafunzo kwa watumishi wa ofisi hizo mbili.


 

MSIMU WA PAMBA MWAKA 2020/2021 KUZINDULIWA JUNI 15 - WAZIRI HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifungua mkutano wa maalumu wa wadau wa tasnia ya Pamba uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Benki kuu Jijini Mwanza,  tarehe 7 Juni 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Serikali imetangaza kwamba msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2020/2021 utazinduliwa tarehe 15 Juni 2020.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameyasema hayo tarehe 7 Juni 2020 wakati akizungumza kwenye mkutano maalumu wa wadau wa tasnia ya Pamba uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Benki kuu Jijini Mwanza.

Hasunga amebainisha kuwa msimu wa Pamba utazinduliwa wakati ambapo serikali imejiweka kando kutopanga bei elekezi katika zao hilo pamoja na mazao mengine badala yake bei za mazao zitatokana na soko.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Juma Homera (Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga wakifuatilia mkutano wa maalumu wa wadau wa tasnia ya Pamba uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Benki kuu Jijini Mwanza, tarehe 7 Juni 2020.

Amesema kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha kuwa inasimamia uzalishaji bora wa mazao kadhalika kusimamia upatikanaji wa masoko ya mazao ili kuwa na bei nzuri yenye manufaa kwa wakulima.

Amesema kuwa kutokana na usimamizi madhubuti wa serikali kupitia Wizara ya Kilimo, uzalishaji wa pamba umeongezeka kutoka tani 122,178 msimu wa ununuzi wa 2015/2016 hadi tani 348,910 msimu wa 2019/2020.

Waziri Hasunga ameeleza kuwa zao la pamba ni mhimili wa uchumi wa wananchi wengi katika mikoa 17 na Wilaya 56 zinazozalisha zao hilo.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akisisitiza jambo kuhusu zao la Pamba wakati wa mkutano wa maalumu wa wadau wa tasnia ya Pamba uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Benki kuu Jijini Mwanza,  tarehe 7 Juni 2020.

Kiwango   kikubwa cha uzalishaji kwa miaka ya karibuni kilifikiwa katika msimu wa ununuzi wa 2011/12 ambapo kiasi cha tani 357,133 za pamba zilizalishwa. Kutokea hapo, uzalishaji umekuwa ukishuka mwaka hadi mwaka ambapo katika msimu wa kilimo wa 2015/16 uzalishaji ulikuwa tani 122,178 kiasi ambacho ni kidogo kuwahi kuzalishwa nchini.
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipoingia madarakani, hatua kadhaa za makusudi zimechukuliwa na Wizara ya Kilimo ili kulinusuru zao la pamba ambapo malengo ya Wizara kwa sasa ni kuzalisha tani 1,000,000 za pamba ifikapo mwaka 2022/2023.

Sehemu ya wadau wa tasnia ya Pamba wakifuatilia mkutano wa maalumu wa wadau wa tasnia ya Pamba uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Benki kuu Jijini Mwanza,  tarehe 7 Juni 2020.

Amezitaja Hatua zilizochukuliwa na serikali kuwa ni pamoja na kuhamisha makao makuu ya Bodi ya Pamba kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza ili kuwa karibu na maeneo yanayolima pamba na kuwahudumia wakulima kwa karibu zaidi. Kutokana na hatua hiyo, ufanisi wa utendaji na huduma kwa wakulima umeongezeka.
Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza Zao la Pamba kurejeshwa Bodi ya Pamba ili kuimarisha usimamizi wa fedha zinazokusanywa na utoaji wa huduma kwa wakulima kwa lengo la kuboresha kilimo cha Pamba.
Hatua nyingine ni kuanzishwa kwa mfumo rasmi wa kuzalisha mbegu bora za kupanda. Kwa mara ya kwanza wakulima wote wa pamba kuanzia msimu wa kilimo wa 2018/19 wamepanda mbegu zilizothibitishwa (certified seeds). Aidha, mbegu mpya ya UKM08 yenye uwiano mkubwa wa pamba nyuzi wa asilimia 38-42 ukilinganisha na mbegu aina ya UK91 iliyokuwa na asilimia 32-35 ndiyo inayopandwa na wakulima. Kwa kuwa nyuzi zina thamani kubwa kuliko mbegu, UKM08 inampatia mkulima mapato makubwa zaidi kwa kuongeza bei anayolipwa.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akifungua mkutano wa maalumu wa wadau wa tasnia ya Pamba uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Benki kuu Jijini Mwanza, tarehe 7 Juni 2020. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mwanza


Waziri Hasunga amesema kuwa mafanikio ya zao la Pamba yamechagizwa na kubadilisha mfumo wa upuliziaji wa viuadudu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Kuimarisha upatikanaji na usambazaji wa pembejeo kwa wakulima kwa kuwapatia mbegu bora za kupanda, viuadudu, vinyunyizi na molasisi pasipo kulipa fedha taslimu na wakulima kulipa pembejeo hizo kwa kukatwa shilingi 100 kwa kila kilo moja ya pamba katika mjengeko wa bei.
Kadhalika ni pamoja na kubadili mfumo wa ununuzi wa pamba kwa kuwaondoa mawakala wa kampuni binafsi na badala yake kutumia Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS). Kwa kuchukua hatua hii, ubora wa pamba umeongezeka kutoka asilimia 22 msimu ununuzi wa 2017/18 hadi asilimia 65 msimu wa 2019/2020. 
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) amesema kuwa msimu wa ununuzi wa zao la Pamba 2019/2020 haukuwa rahisi lakini kwa kiasi umekuwa na mafanikio makubwa ambapo amewashukuru wakuu wa Mikoa ya uzalishaji kwa usimamizi madhubuti wa zao la Pamba jambo lililopelekea kuongezeka kwa uzalishaji na tija. 
Pia amewapongeza wafanyabiashara/wanunuzi wa Pamba, Sekta mbalimbali za fedha zikiwemo Benki N.k kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa pamba ya wakulima inanunuliwa. 
Ameongeza kuwa serikali iliamua kuwalipa wakulima wa Pamba kupitia Account zao za Benki hivyo jumla ya Account 128,000 za wakulima wa Pamba zimefunguliwa huku zoezi hilo likiendelea.
Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stela Manyanya akitoa salamu za Wizara hiyo amesema kuwa wanunuzi/wafanyabiashara wanapaswa kujipanga zaidi baada ya serikali kutekeleza wajibu wake ili kuhakikisha kuwa msimu wa zao la Pamba utakapoanza wakulima waweze kupata bei nzuri na yenye tija. 

Thursday, June 4, 2020

WAZIRI WA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA APOKEA VIFAA VYA KUKABILIANA NA CORONA KUTOKA AFRICAB


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe uzindua ugawaji wa mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya Africab kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam kwa lengo la  kupambana na maambukizi ya Corona. Aliyeambata naye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na Wakurugenzi watendaji wa Kampuni ya Africab.


Katika kuendelea kukabiliana na virusi vya Corona nchini, SerikaIi kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imepokea msaada wa matanki 100 kutoka kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya umeme ya AFRICAB maalumu kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi na wanavyuo jijini Dar es Salaam kunawa mikono ili kukabiliana na janga la homa mapato inayosababishwa na virusi vya Corona.

Akipokea na kisha kukabidhi matanki hayo yenye thamani ya Sh. Milioni 50, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako mbali na kushukuru kwa msaada huo, amefafanua kwamba msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo vyuo na baadhi ya shule nchini zimefunguliwa na itawawezesha wanafunzi kujikinga dhidi ya ugonjwa huo wa Covid-19.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akizungumza baada ya kukata utepe kuashiria  uzinduzi wa ugawaji wa mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya Africab kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam kupambana na maambukizi ya Corona. Kulia kwani ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na Wakurugenzi watendaji wa Kampuni ya Africab.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akikagua moja ya tanki la maji kati ya mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya Africab kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam kupambana na maambukizi ya Corona.

Ameongeza kuwa msaada wa matanki hayo yenye ujao wa lita 1000 kila moja yametolewa kwa shule 10 za Sekondari za Serikali na 57 kwa shule za sekondari za binafsi na vyuo 13 ni muhimu kwa Serikali hasa wakati huu ambapo vita dhidi ya ugonjwa huo unaendelea.

Profesa Ndalichako amesema kuwa "Naiwapongeze AFRICAB msaada huu muhimu kwa ajili ya kinda afya za wanafunzi wetu, niwaombe wadau wengine muige mfano huu kwa ajili ya manufaa ya watu wote wa taifa hili,"amesema Prof.Ndalichako na kuongeza licha ya hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika napambana dhidi ya Corona, wananchi nao wanapaswa kuchukua tahadhari hizo huku wakiendelea kuchapa kazi.

Kwa upande wa Meneja Masoko wa AFRICAB David Tarimo, ametumia nafasi hiyo kueleza msaada umetolewa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na Corona na kusisitiza kuwa wao kama wadau wa maendeleo na wawekezaji wazalendo huo ni wajibu wao wa kimsingi.

 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa kampuni ya Africab baada ya kuzindua ugawaji wa mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yalitolewa na kampuni hiyo  kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam ili kupambana na maambukizi ya Corona.


Na Said Mwishehe ,Michuzi TV
"Mapambano dhidi ya Corona ni wajibu wa kila mmoja wetu na sisi AFRICAB tunatambua nini kinafanywa na Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo unaoisumbua dunia kwa sasa.Aidha mbali na msaada huo, AFRICAB itaendelea kushirikiana na Serikali katika masala mbalimbali ya kimaendeleo huku ikitarajia kujenga cha uzalishaji wa dawa za binadamu hivi karibuni " amesema.

Awali Mkurugenzi Mwenza wa kiwanda hicho Mohammed Ezz amesema kwamba anatoa shukrani za dhati kwa Rais John Magufuli kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji yanayokiwezesha kiwanda hicho kutekeleza majukumu yake ipasavyo." Tunamshukuru Rais Magufuli kwa namna ambavyo ameweka mzingira mazuri ya uwekezaji na hii imekuwa fursa kwetu kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia ubora ww viwango vinavyotakiwa."