Matokeo chanyA+ online




Wednesday, September 2, 2020

BILIONI 12 KULIPWA WAKULIMA WA KAHAWA MKOANI KAGERA - KATIBU MKUU KUSAYA

 




Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella ( katikati) akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto) na Katibu Mkuu Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe (kulia) leo wakati wa kikao cha kujadili ulipwaji wa madeni ya wakulima wa kahawa mkoa wa Kagera kilichofanyika Mwanza na kuhusisha viongozi wakuu wa Vyama vya Ushirika KDCU na KCU.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Mwanza kutangaza uamuzi wa kuanza kuwalipa wakulima wa kahawa wa mkoa wa Kagera fedha zao shilingi Bilioni 12 kupitia Vyama Vikuu vya KDCU na KCU.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe. Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe (kulia) wakati wa kikao kilichojadili ulipwaji wa madeni ya wakulima wa zao la kahawa kwa vyama vikuu vya ushirika KDCU na KCU utakaonza kesho .Kikao kimefanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.Picha ya pamoja kati ya Makatibu Wakuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( wa pili kushoto) akiwa kwenye kikao leo Mwanza kujadili kuanza kulipwa kwa wakulima wa Kahawa Kagera.Wengine ni Bw.Emanuel Tutupa (RAS Mwanza) katikati,Prof.Riziki Shemdoe ( Katibu Mkuu Viwanda) na Prof.Faustin Kamuzola (RAS Kagera aliyevaa kofia).



Serikali imesema wakulima waliokusanya kahawa yao kwenye vyama vya ushirika mkoani Kagera wataanza kulipwa madeni yao mapema wiki hii.

Kauli hiyo imetolewa leo (01.09.2020) Jijini Mwanza na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya wakati alipoongoza kikao cha viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, mikoa ya Mwanza na Kagera na vyama vikuu vya Ushirika KDCU na KCU kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Kusaya alisema tangu msimu wa ununuzi wa kahawa ulipofunguliwa mwezi Juni mwaka huu jumla ya shilingi Biioni 32 tayari zimelipwa kwa wakulima wa mkoa wa Kagera kutokana na kukusanya tani 62,336 za kahawa ghafi na tani 31,168 za kahawa safi kwenye vyama vikuu vya ushirika na vile vya msingi.

“Pamoja na kulipa Bilioni 32 za wakulima bado Chama Kikuu cha Ushirika KDCU kinadaiwa shilingi Bilioni 12 kutokana na kukusanya kahawa ya wakulima ,hivyo kikao chetu leo tumekubaliana KDCU waanze kulipa wakulima shilingi Bilioni 7 zilizopo tayari kuanzia kesho na zingine Bilioni 5 zitalipwa mapema wiki ijayo” alisema Kusaya

Katibu Mkuu huyo alisema deni hilo linatokana na KDCU kuendelea kukusanya kahawa ya wakulima kufuatia uwepo wa mavuno mazuri ambapo takwimu zinaonesha wanakusanya kwa siku kahawa yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.7 kutoka kwa wakulima na tayari wamenunua kilo milioni 37.3 kati ya lengo la kilo milioni 45 za kahawa msimu huu.

Kuhusu Chama Kikuu cha Kagera ( KCU) ,Katibu Mkuu Kusaya alisema wanadaiwa na wakulima shilingi Bilioni 7.1 na kuwa wamekubaliana kuanza kulipa shilingi Bilioni 2 mapema wiki huku wakiendelea na kukusanya fedha toka kwa wanunuzi waliowauzia kahawa.

“Shilingi Bilioni 2 za wakulima waliouza kahawa KCU tumekubaliana zitaanza kulipwa wiki hii Kagera na kuwa zingine Bilioni 3 zitatolewa na mnunuzi aliyeuziwa kahawa na KCU katika muda mfupi ujao” alisisitiza Kusaya.

Kusaya aliongeza kusema serikali imejipanga kikamilifu kuona wakulima wa kahawa kote nchini wanalipwa fedha zao kwani mfumo unaotumika wa vyama vikuu na AMCOS kununulia kahawa ni wa uhakika na kuwa wakulima wawe na subira kipindi kifupi fedha zitapatikana kwani wanunuzi toka nje ya nchi wameanza kuonyesha nia ya kuja Tanzania kutokana na tatizo la korona kudhibitiwa .

“Kuchelewa kwa malipo ya wakulima wa kahawa hususan mkoa wa Kagera yametokana na vyama vikuu vya ushirika kuchelewa kuuza kahawa” alisema Kusaya na kuwa serikali ipo tayari kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kutoa mikopo kwa vyama vya ushirika kununua kahawa na kulipa wakulima.



Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe alisema kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo wanaendelea kutafuta masoko ya uhakika ya mazao ya wakulima kama alivyoelekeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Prof. Shemdoe alisema kwa sasa wanunuzi na wafanyabiashara binafsi wanaruhusiwa kununua kahawa toka vyama vikuu vya ushirika au vyama vya msingi (AMCOS) lakini wahakikishe wanatoa bei nzuri na yenye ushindani wa soko.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora alisema wakulima wa kahawa msimu huu wamepata bei nzuri karibu asilimia 75 ya bei ya soko la dunia na kuwa vyama vikuu vya Ushirika (KDCU) na (KCU) kwa mkoa wa Kagera wamefanya kazi nzuri kuwezesha wakulima kulipwa bei nzuri.

Prof.Kamuzora ametoa wito kwa watanzania kuwa na tabia ya kunywa kahawa ili kusaidia upatikanaji wa soko la kahawa ndani ya nchi tofauti na ilivyo sasa kahawa asilimia 93 inayozalishwa nchini inauzwa nje ya nchi.

Mrajis wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini Dkt. Benson Ndiege alisema wanunuzi binafsi wa kahawa wanaruhusiwa kununua lakini sharti waingie mikataba na vyama vya vikuu vya ushirika au AMCOS ili kuwa na uhakika wa bei nzuri kumfikia mkulima.

Dkt. Ndiege alitoa wito kwa viongozi wa vyama vya ushirika nchini hususan mkoa wa Kagera kutoa kipaumbele cha malipo ya wakulima waliouza mapema kahawa yao kutokana na fedha zilizopatikana sasa na makubaliano yaliyofikiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu Kilimo na Viwanda .

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Kahawa Tanzania imeonesha makusanyo ya kahawa msimu wa 2020/2021 yamefikia jumla ya tani 79,245 (73%) za kahawa ghafi kati ya lengo la tani 108,000 na tani 44,695 (63 %) za kahawa safi kati ya lengo la tani 70,000.

Kahawa hiyo imekusanywa toka kwenye mikoa yote 17 inayolima zao la kahawa nchini.

Aidha bei ya kahawa kwa mkulima msimu huu imekuwa ikilipwa kwa utaratibu wa malipo ya awali kupitia vyama vyao vya ushirika ambapo mkulima analipwa kwa kilo shilingi 1,200 kahawa ya Robusta maganda (dry cherry) na shilingi 1,250 na 1,500 kahawa za Arabika maganda (parchment)

MGOMBEA URAIS KUPITIA TIKETI YA CCM, RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NZEGA MKOANI TABORA

Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Igunga mkoani Tabora katika Kampeni za Urais za CCM wakati akiwa njiani kuelekea Nzega.
Sehemu ya Wananchi wa Igunga waliohudhuria mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Shelui mkoani Singida wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Tabora.
Wananchi wa Shelui mkoani Singida wakishangilia mara baada ya Mgombea Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama wakati akielekea Igunga mkoani Tabora.

MGOMBEA MWENZA MAMA SAMIA AKISALIMIANA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA MVOMERO

 

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana Wananchi wa kijiji cha Mvomero Mkoani Morogoro alipokuwa njiani akitokea Turiani kuelekea Morogoro Mjini kuhutubia Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM Uwanja wa Jamhuri Mrorogoro leo Septemba 02,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SERIKALI YATUMIA SH.BILIONI 470.4 KUTEKELEZA MIRADI MKOANI SINGIDA


Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi (hawapo pichani) katika  mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Bombadia mjini Singida jana.


Umati wa Wananchi wa Mkoa wa Singida wakisikiliza hutuba ya mgombea huyo wa Urais
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Francis Isack akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo,  akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Yahaya Masere akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu,  akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Tatu Ntandu,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Gwau,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mussa Sima, akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.


Na Dotto Mwaibale, Singida

Serikali imetumia Sh. Bilioni 470.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Singida.

Hayo  yalisemwa na  Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli wakati akiwahutumia maelufu ya wanannchi katika mkutano wake wa pili wa kampeni wa kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa awamu ya pili uliofanyika viwanja vya Bombadia mjini hapa jana.

Magufuli alisema katika kipindi cha miaka mitano Serikali imefanikiwa kujenga vituo vya afya vilivyowezesha akinama 730 kufanyiwa upasuaji hivyo kuokoa maisha yao na watoto wao.

Alisema mbali ya vituo hivyo vya afya serikali imejenga Hospitali tatu za wilaya  katika Wilaya za Mkalama, Ikungi na Singida.

" Ndani ya  kipindi hicho viwanda zaidi ya 8,500 vimejengwa katika mkoa huu huku tukizalisha ajira milioni sita  na kama mtanipa ridhaa ya kuongoza nchi kwa mara nyingine tena tutazalisha ajira milioni 8." alisema Magufuli huku akishangiliwa.

Aidha Magufuli alisema Sh. bilioni 52.6 zimetumika kujenga miundombinu ya shule yakiwemo madarasa, maabara na miundombinu mingine huku

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida  Mandewa ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika na hiyo ni moja ya hatua ya kuboresha sekta ya afya.

Mgombea huyo wa Urais alisema kulikuwa na vijiji 2018 tu vilivyokuwa vimefikishiwa  umeme mwaka 2015 lakini katika miaka mitano ya uongozi wake vijiji 9570 vimefikiwa kati ya vijiji 12280 nchi nzima huku sh. bilioni 310 zikitumika kujenga miundombinu wezeshi na sh. bilioni 27.2 zikitumika kutekeleza miradi ya maji ipatayo 66.

Akiongelea uandikishaji wanafunzi umeongezeka kutoka milioni 1 hadi milioni 1.6 baada ya kuanza kwa mpango wa elimu bure.

Magufuli aliongeza kuwa katika kipindi hicho jumla ya sh. bilioni 17 zimetumika kujenga barabara za Singida mjini na kuziwekea taa huku ujenzi wa barabara ya Chaya Singida hadi Tabora ikibakia kilometa tu 20 kukamilika.

Alisema viituo vya afya 487 vimejengwa Tanzania nzima na bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115.

Alisema vijiji 9,570 vimefikiwa na nishati ya umeme ikilinganishwa na vijiji 2,018 vilivyokuwa na umeme mwaka 2015.

Alisena katika kipindi hicho bajeti ya Wizara ya Afya imeongezwa kutoka sh. bilioni 30 hadi bilioni 270.

" Niko hapa kwa unyenyekevu mkubwa kuomba kura za vyama vyote kwa sababu maendeleo hayana chama" alisema Magufuli.

Magufuli alisema katika kipindi hicho katika Mkoa wa Singida visima vinne virefu vimechimbwa ili kuongeza upatikanaji wa maji ambapo sh. bilioni 66 zimetumika kutekeleza miradi ya maji na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 41 hadi 54.

Alisema mbali ya kutekeleza miradi hiyo ya maji shule kongwe ikiwemo Mwenge Sekondari zimekarabatiwa ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha sekta ya elimu.

Alisema ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa sh. bilioni 850 hadi kufikia zaidi ya sh.Trilioni 1.5 huku Tozo 114 zikifutwa katika sekta ya kilimo na wafanyabiashara ndogondogo wakifutiwa kodi 54.

Alisema Serikali imeweza  kukusanya   sh Ttrioni1.5-1.9 kwa  mwezi  ukilinganisha na Bilioni  850 zilizokuwa zikiikusanywa hapo awali.

Akiendelea kuongelea mafanikio ya Seikali kwa kipindi hicho cha miaka mitano alisema kwa mujibu wa ripoti ya  "Global Peace Index" Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki, ya 6 Afrika na 52  duniani kwa amani.

Magufuli aliongeza kueleza kuwa ndani ya miaka hiyo mitano mitandao ya simu imeimarika nchi nzima huku waki jenga ukuta wa kilometa  25 eneo la Mererani ambao umesaidia  kudhibiti  wizi wa madini ya Tanzanite na upotevu wa mapato ya nchi.

Mgombea huyo alimaliza hutuba yake kwa kuwanadi wagombea wote wa nafasi ya ubunge na udiwani wa chama hicho pamoja na kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga LA Corona kutokana  na maombi tuliyofanya kama taifa na kuwa hiyo imetoa somo kubwa kwa mataifa mengi duniani kuwa Mungu anaweza.

MAJALIWA AZINDUA KAMPENI ZA CCM MKOA MANYARA

 

Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa  akimkabidhi nakala ya Ilani ya Uchaguzi, Mgombea Ubunge wa CCM wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul, baada ya kuzindua Kampeni za CCM Mkoa wa Manyara  kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati kuzindua Kampeni za CCM Mkoa wa Manyara, Septemba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipozindua Kampeni za CCM Mkoa wa Manyara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipozindua Kampeni za CCM Mkoa wa Manyara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Septemba 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, September 1, 2020

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM, RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MKOA WA SINGIDA

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa mkoa wa Singida kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bombardier uliopo Singida Mjini.



 



Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa mkoa wa Singida kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bombardier uliopo Singida Mjini.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Bombardier uliopo Singida Mjini kwa ajili ya mkutano wa Kampeni za Urais za Chama cha Mapinduzi CCM



 Sehemu ya Wananchi waliohudhuria Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Bombardier uliopo Singida Mjini.


Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana  na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa CCM Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro kwenye mkutano wa Kampeni kwa Chama cha Mapinduzi katika Viwanja vya Shele ya Sekondatri Gairo (B)  leo Sepotemba 01,2020.

 

KINANA ANOGESHA UZINDUZI WA KAMPENI ZA RIDHIWANI KIKWETE JIMBO LA CHALINZE




NA ANDREW CHALE, CHALINZE.

Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM anayewania kiti hicho kwa mara nyingine, Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua rasmi kampeni zake za Ubunge Jimbo la Chalinze huku akiwataka WanaCCM kupiga kura za kishindo kwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Ridhiwani Kikwete amesema kwa sasa WanaCCM watembee kifua mbele kwani maendeleo yameoenekana kutokana na utekelezaji wa Ilani ya CCM ikiwemo ile ya 2020-2025.

"Tumeshuhudia miundombinu bora na ya kisasa pamoja na ukuaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya, pia elimu na maendeleo ya utawala bora.

Oktoba 28, WanaCCM Chalinze, Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla tujitokeze kifua mbele kumpigia kura nyingi za ndiyo Rais Magufuli lakini pia kura za ushindi kwa Madiwani  na Wabunge wetu." alisema Ridhiwani Kikwete.

Aidha, akinadi sera na maendeleo yaliyopatikana  ndani ya jimbo hilo,  
Alisema awali wakati anaingia kwenye jimbo hilo alikuta vituo vya afya vitano lakini kwa sasa vimeongezeka na kufikia zaidi ya Nane.

"Leo hii tulipo kuna vituo vya Afya zaidi ya Nane na kuwa vikisaidia sana Wananchi wetu kupata huduma stahiki mahala pao na kuacha kwenda mbali.

Lakini pia kwa sasa tunaendelea kupanua katika ujenzi wa vituo vyetu vya afya ikiwemo kituo cha Afya Buringu, pia tunataka kujenga wodi ya akinamama kama kituo cha Miono,

Hii itaenda kituo cha afya Kibindu na vingine ilikuhakikisha Wananchi wetu hawaendi mbali kusaka huduma za afya." Alisema Ridhiwani Kikwete.

Aidha, aliongeza kuwa lengo kubwa yeye kama Mbunge na Madiwani watahakikisha Wananchi wa Chalinze wanapata huduma za afya zikiwemo za kibingwa ndani ya Chalinze.

"Miaka mitano iliyopita tumehakikisha Wananchi wanapata huduma za afya hapahapa. Katika kuhakikisha hilo tayari Hospitali imeshajengwa na ipo katika hatua ya mwanzo.

Ujenzi wake upo wa vipande vya hatua nne kwa sasa tunaingia hatua ya pili ambapo wodi ya kutoa huduma kwa akina mama nayo imeanza kujengwa

lengo mimi kama mbunge na Madiwani ni kuhakikisha hospitali ile inajengwa na kukamilishwa kwa ukamilifu ili Wananchi wetu wasiende tena Hospitali za Wilaya za jirani kama Tumbi ama Bagamoyo ili waweze kufaidika na matunda ya viongozi wao" Alieleza Ridhiwani Kikwete.

Akiongelea suala la miundombinu, tayari maji, umeme na barabara kwa kuzingatia ilani, imetekelezwa kwa kiwango kikubwa na kwa sasa amewataka wananchi wajiandae kwa mambo makubwa.

"Ilani ya CCM 2020-2025  Imeelezea juu ya utekelezaji sasa wa ujenzi wa barabara ya Afrika Mashariki inayotoka Kenya inayopita Pangani inayokuja mpaka Saadani na kwenda Mkange hadi Makurunge na Bagamoyo.

Wananchi wa Mkange mliopitiwa na barabara hii mtalipwa fidia na mjiandae sasa kwa mambo makubwa yanayokuja kwani mji unakuja kubadilishwa

Pia maisha ya watu yatabadilika na uchumi utakuwa mkubwa sana na zao la muhogo unaolimwa utakuwa na thamani kubwa sana" Alisema Ridhiwani Kikwete.

Aidha, Ridhiwani Kikwete aliwataka wote waliopita bila kupingwa kuhakikisha wanaendelea kumuombea kura nyingi za chama cha Mapinduzi CCM Rais Magufuli wakiwemo Wabunge wa vitimaalum ili kushinda ushindi wa kishindo.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hizo, Katibu Mkuu Mstaafu, Kinana alisema misingi imara iliyojengwa na viongozi wa chama hicho itaendelea kulindwa na kuimalisha ushindi imara.

"Wote ambao mliteuliwa Chama kwenye majimbo na vitimaalum hongereni sana.
Pia hongereni kwa mliopita bila kupingwa, lakini msibweteke, mpambane kutafuta kura nyingi za Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli." alieleza Kinana.

Kinana pia aliweza kuwaombea kura madiwani wote wa Jimbo la Chalinze na Bagamoyo pamoja na Mgombea wa Ubunge wa Bagamoyo,  Muharami Mkenge.

Uzinduzi huo umefanyika katika  viwanja vya Miono shule ambapo umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa CCM waliweza kushiriki kusikia sera mbalimbali za wagombea wao.


MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM, RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYONI KATIKA KAMPENI





Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Manyoni katika Kampeni za Urais wakati akiwa njiani kuelekea Singida mjini leo tarehe 1 Septemba, 2020.





NCHI YETU IKO KWENYE NAFASI YA 10 KATIKA MAENDELEO YA KIUCHUMI – RAIS MAGUFULI

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na mamia ya wananchi wakati akiwasili  wilayani Bahi mkoa wa Dodoma kwa mkutano wa kampeni wa hadhara leo Jumanne Septemba 1, 2020, ikiwa ni kituo chake cha kwanza toka azindue rasmi kampeni zake za
kugombea Urais


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na mamia ya wananchi wakati akiwasili  wilayani Bahi mkoa wa Dodoma kwa mkutano wa kampeni wa hadhara leo Jumanne Septemba 1, 2020, ikiwa ni kituo chake cha kwanza toka azindue rasmi kampeni zake za
kugombea Urais

 

Na Said  Mwishehe,Bahi-Michuzi TV

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.John Magufuli amewahkikishia wananchi wa Wilaya ya Bahi kuwa wakimchgua katika Uchaguzi Mkuu mwaka unaotarajia kufanyika Oktoba 28 atahakikisha anaendelea kuleta maendeleo kwa kasi kubwa ikiwa pamoja na kumalizia viporo vilivyobaki.

Dk.Magufuli amesema hayo leo Septemba 1, 2020 wakati akizungunza na  wananchi wa Wilaya ya Bahi alipokuwa akiomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu na wingi wa wananchi amewaambia ana deni kubwa ya kuwapelekea maendeleo na kwamba hatawasahau.

Wakati anaanza kuzungumza Dk.Magufuli amesema katika kuleta mabadiliko ya kweli katika maeneo yetu  katika mambo ya kitaifa tayari amezungumza juzi, ya kimkoa ameshazungumza na leo yuko Bahi ambako kuna mengi yamefanyika "ata hizi nyumba huko nyuma haizikuwa hivyo mmepiga hatua kubwa ndani ya miaka mitano" amesema Magufuli

"Tumejenga Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya vitatu vya Bahi, Kifukuta na Mdemu nataka  hospital imalizike haraka,ndio maana naomba mnipe kura nimalizie kiporo kilichobaki kwani imekamilika kwa asilimia 95

"Nimekuja kuomba kura nataka katika miaka mingine mitano elimu bure iendele hapa Bahi tumetumia Sh.bilioni 2.1 na tutaendelea kutoa elimu bure,ndio maana nimekuja kuomba kura kwenu.

Katika miradi ya maji tumetumia Sh.bilioni 2.9 katika maeneo ya Magage, Bahi,Mkatike, Mdem na Ngugi. Pia tumetekeleza miradi ya maji katika vijiji vya Zanka,Nondwa na Zegele na kuchimba visima vingine 11 "najua tatizo la maji bado lipo Bahi naomba mnibebeshe hii changamoto,tutaimaliza,"amesema Dk.Magufuli.

Kuhusu umeme, Dk.Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano vijiji 43 vimepata umeme kutoka vijiji vinne mwaka 2015 na kwamba kuna vijiji 16 ambavyo bado havijaunganishiwa umeme,hivyo anaomba kura ili amalizie vijiji hivyo.

Pia amewaambia wananchi hao kuwa wameendelea kujenga barabara na kwamba anataka akichaguliwa tena amalizie ujenzi wa barabara kwa fedha za ndani."Naombe mnipe nafasi nimalizie".

Kwa upande wa wakulima na wafugaji ,Dk.Magufuli amesema anatambua namna ambavyo wakulima wanafanya kazi nzuri katika kilimo na anatambua juhudi za wafugaji katika Wilaya hiyo, hivyo ameahidi  kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo na mifugo.

"Nataka kuendelea kusaidia wafugaji, watu Bahi ni wafugaji wazuri, pia tutaendelea kusaidia wakulima wa Bahi tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuimarisha sekta ya kilimo,tumefuta tozo za kodi  114 .

Kuhusu kusaidia kaya masikini hapa Bahi tumetumia Sh.bilioni tano kupitia mfuko wa TASAF,"amesema Dk.Magufuli na kuwasisitiza ikifika siku ya kupiga kura wampigie ili aendelee kuleta maendeleo ya wananchi wa Bahi.

Pamoja na hayo Dk.Magufuli amesema katika miaka mitano watendeleza pale walipoishia, wataendelea kujenga shule na madarasa,kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya barabara, kuweka umeme, kutoa elimu bure ,kuboresha aekta ya afya na sekta nyingine mbalimbali.

"Wingi wenu huu nimebaki na deni kubwa naombeni mnichague , muwachague madiwani wa CCM na mbunge wa CCM hata hivyo kwa sasa Serikali iko Dodoma,na mimi niko Dodoma, sitaisahau Bahi kwanza haiko mbali na Dodoma,nitaleta maendeleo.

"Mpeni kura mbunge wa hapa,tumechelewa sana, tupeni nafasi tutafanya kazi isiyo na mfano miaka mitano ya mwanzo ilikuwa onja onja tu na sasa tunakwenda kufanya kazi kweli kweli, hata hivyo nchi yetu iko kwenye nafasi ya 10 katika maendeleo ya kiuchumi, nchi yetu katika usalama na kwa Afrika iko nafasi ya sita na kwa duniani iko nchi ya 52,"amesema Dk.Magufuli.