Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na mamia ya wananchi wakati akiwasili wilayani Bahi mkoa wa Dodoma kwa mkutano wa kampeni wa hadhara leo Jumanne Septemba 1, 2020, ikiwa ni kituo chake cha kwanza toka azindue rasmi kampeni zake za
kugombea Urais
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na mamia ya wananchi wakati akiwasili wilayani Bahi mkoa wa Dodoma kwa mkutano wa kampeni wa hadhara leo Jumanne Septemba 1, 2020, ikiwa ni kituo chake cha kwanza toka azindue rasmi kampeni zake za
kugombea Urais
Na Said Mwishehe,Bahi-Michuzi TV
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM) Dkt.John Magufuli amewahkikishia wananchi wa Wilaya ya
Bahi kuwa wakimchgua katika Uchaguzi Mkuu mwaka unaotarajia kufanyika
Oktoba 28 atahakikisha anaendelea kuleta maendeleo kwa kasi kubwa ikiwa
pamoja na kumalizia viporo vilivyobaki.
Dk.Magufuli amesema hayo
leo Septemba 1, 2020 wakati akizungunza na wananchi wa Wilaya
ya Bahi alipokuwa akiomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka
huu na wingi wa wananchi amewaambia ana deni kubwa ya kuwapelekea
maendeleo na kwamba hatawasahau.
Wakati anaanza kuzungumza
Dk.Magufuli amesema katika kuleta mabadiliko ya kweli katika maeneo
yetu katika mambo ya kitaifa tayari amezungumza juzi, ya kimkoa
ameshazungumza na leo yuko Bahi ambako kuna mengi yamefanyika "ata
hizi nyumba huko nyuma haizikuwa hivyo mmepiga hatua kubwa ndani ya
miaka mitano" amesema Magufuli
"Tumejenga Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya
vitatu vya Bahi, Kifukuta na Mdemu nataka hospital imalizike
haraka,ndio maana naomba mnipe kura nimalizie kiporo kilichobaki kwani
imekamilika kwa asilimia 95
"Nimekuja kuomba kura nataka katika
miaka mingine mitano elimu bure iendele hapa Bahi tumetumia Sh.bilioni
2.1 na tutaendelea kutoa elimu bure,ndio maana nimekuja kuomba kura
kwenu.
Katika miradi ya maji tumetumia Sh.bilioni 2.9 katika maeneo ya
Magage, Bahi,Mkatike, Mdem na Ngugi. Pia tumetekeleza miradi ya
maji katika vijiji vya Zanka,Nondwa na Zegele na kuchimba visima vingine
11 "najua tatizo la maji bado lipo Bahi naomba mnibebeshe hii changamoto,tutaimaliza,"amesema Dk.Magufuli.
Kuhusu umeme,
Dk.Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano vijiji 43 vimepata
umeme kutoka vijiji vinne mwaka 2015 na kwamba kuna vijiji 16 ambavyo
bado havijaunganishiwa umeme,hivyo anaomba kura ili amalizie vijiji
hivyo.
Pia amewaambia wananchi hao kuwa wameendelea kujenga
barabara na kwamba anataka akichaguliwa tena amalizie ujenzi wa barabara
kwa fedha za ndani."Naombe mnipe nafasi nimalizie".
Kwa upande
wa wakulima na wafugaji ,Dk.Magufuli amesema anatambua namna ambavyo
wakulima wanafanya kazi nzuri katika kilimo na anatambua juhudi za
wafugaji katika Wilaya hiyo, hivyo ameahidi kuendelea kuimarisha sekta
ya kilimo na mifugo.
"Nataka kuendelea kusaidia wafugaji, watu
Bahi ni wafugaji wazuri, pia tutaendelea kusaidia wakulima wa
Bahi tumekuwa na jitihada mbalimbali za kuimarisha sekta ya
kilimo,tumefuta tozo za kodi 114 .
Kuhusu kusaidia kaya masikini hapa
Bahi tumetumia Sh.bilioni tano kupitia mfuko wa TASAF,"amesema
Dk.Magufuli na kuwasisitiza ikifika siku ya kupiga kura wampigie ili
aendelee kuleta maendeleo ya wananchi wa Bahi.
Pamoja na hayo
Dk.Magufuli amesema katika miaka mitano watendeleza pale walipoishia,
wataendelea kujenga shule na madarasa,kuendelea na ujenzi wa miundombinu
ya barabara, kuweka umeme, kutoa elimu bure ,kuboresha aekta ya afya na
sekta nyingine mbalimbali.
"Wingi wenu huu nimebaki na deni
kubwa naombeni mnichague , muwachague madiwani wa CCM na mbunge wa CCM hata hivyo kwa sasa Serikali iko Dodoma,na mimi niko Dodoma, sitaisahau
Bahi kwanza haiko mbali na Dodoma,nitaleta maendeleo.
"Mpeni
kura mbunge wa hapa,tumechelewa sana, tupeni nafasi tutafanya kazi isiyo
na mfano miaka mitano ya mwanzo ilikuwa onja onja tu na sasa
tunakwenda kufanya kazi kweli kweli, hata hivyo nchi yetu iko kwenye
nafasi ya 10 katika maendeleo ya kiuchumi, nchi yetu katika usalama na
kwa Afrika iko nafasi ya sita na kwa duniani iko nchi ya 52,"amesema
Dk.Magufuli.
No comments:
Post a Comment