Matokeo chanyA+ online




Saturday, May 8, 2021

NDALICHAKO AKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KWA KUIBUA WABUNIFU


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia  Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wake na viongozi wengine wakimuangalia Mbunifu wa FARM CUT kutoka SUA, Mussa Dotto akionyesha matrekta shamba hilo linavyofanyakaz iwakati wa MAKISATU 2021 Dodoma.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard  Akwilapo akitoa maelezo ya mashindano hayo ya MAKISATU 2021 kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua maonesho na mashindano hayo jijini Dodoma.
Wananchi wakimiminika kwenye banda la SUA kuangalia bunifu na teknolojia mbalimbali ambazo wamekuja kuzionyesha kwenye maonesho hayo ya MAKISATU 2021 Jijini Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akiwa kwenye picha ya pamoja na waonyeshaji kutoka SUA Kwenye banda la SUA lililopo kwenye maonesho ya MAKISATU 2021 jijini Dodoma.

Fundi sanifu wa maabara ya Kemia na Fizikia SUA,  Anneth Coster akiwaonyesha Wanafunzi namna Indicator iliyozalishwa na SUA kwa ajili ya somo la kemia kwa wanafunzi wa shule za sekondari.

Na Calvin Gwabara - Dodoma
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa jitihada wanazozifanya katika kuibua Wabunifu,Teknolojia na mbinu zingine za kisayansi pamoja na kuwa saidia na kuendeleza wabunifu hao ili waweze kufikia ndoto zao na kusaidia jamii na taifa.

Pongezi hizo ametoa wakati akitembelea kukagua kazi za wabunifu wa SUA na maonesho yao kabla ya kuzindua rasmi mashindano ya kitaifa ya sayansi,teknolojia na ubunifu (MAKISATU 2021) jijini Dodoma yanayokutanisha wabunifu kutoka nchi nzima kwenye makundi saba ya ushindani.

Akizungumza wakati akifungua mashindano hayo amesema kuwa miongoni mwa mafanikio ambayo Serikali imeyapata katika kuendeleza Sayansi na Ubunifu nchini ni pamoja na kuibua na kutambua wabunifu wachanga 1066 kupitia MAKISATU 2019/2020 ambapo kati ya hao wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Serikali ili bunifu zao zifikie hatua ya kubihasharishwa na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kuchangia kwenye pato la taifa.

 “Ni matumaini na matarajio yangu kuwa bidhaa zinazozalishwa na wabunifu na wavumbuzi nchini zitaongeza tija katika uzalishaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda na kuongeza thamani ya bidhaa zinazo zalishwa pamoja na kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma katika Nyanja mbalimbali” Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Aidha Prof. Ndalichako ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 hadi mwaka 2020 Serikali imefadhili jumla ya miradi 215 ya sayansi teknolojia na ubunifu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na Mifugo, Afya, Nishati, Maliasili na Viwanda aidha kupitia mfuko wa taifa wa uendelezaji Sayansi naTeknilojia Serikali imewajengea  uwezo watafiti 579 katika masomo ya uzamili na uzamivu ili kuwaongezea weledi kwenye utafiti.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi huyo kufungua maonesho hayo ya MAKISATU 2021Katibu Mkuu wa wizara  hiyo Dkt.Leonard Akwilapo amesema mashindano hayo ya MAKISATU yalianzishwa mwaka 2019 yakiwa ni moja ya mikakati ya Wizara ya kuibu,kutambua na kuendeleza bunifu na vumbuzi zinazofanywa na Watanzania na kukuza hamasa ya ubunifu na kuhamasisha matumizi ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu katika shughuli ya kijamii na  kiuchumi utakaotegemeza maendeleo ya uchumi wa viwanda.

Amefafanua kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya MAKISATU jumla ya wabunifu 1066 waliibuliwa na kutambuliwa na Wizara na wabunifu mahiri 130 wanaendelezwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi naTeknolojia (COSTECH) ili ubunifu wao ufikie kubiasharishwa na hivyo kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof.Raphael Chibunda alimwambia Waziri huyo kuwa katika kuhakikisha wabunifu wa SUA wanafikia hatua za kubihasharisha wanatarajia kumpatia kiasi cha shilingi milioni 20 mmoja wa wabunifu wao Mussa Dotto aliyebuni Trekta la kulimia aliloliita FARM CUT ili aweze kuzalisha matrekta hayo matatu yaingie sokoini.

Amesema walipoonaamebuni trekta hilo waliamua kumsaidia kupitia mfuko wa ubunifu wa Chuo lakini lengo lingine ni kutaka kuwaonyesha wanaosema elimu imeshuka waone namna ambavyo vijana  wanawezakufanya mambo makubwa vyuoni na kunufaika pamoja na kunufaisha jamii na taifa.

Chuo Kikuu cha Sokone cha Kilimo SUA kinashiriki maonesho hayo kwa kuonyesha kazi zake mbalimbali za kitafiti na kibunifu lakini pia kimeingiza Wabunifu watatu  kwenyemashindano hayo ya MAKISATU kupitia kundi la vyuo vikuu ambalo lina wabunifu 10.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema Sayansi Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi Endelevu.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA TLS BUNGENI JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza na viongozi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walioongozwa na Rais wa Chama hiyo, Dkt. Edward Hosea (kushoto kwake) walipomtembelea  ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dkt. Edward Hosea alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

TAMUFO YAIOMBA BASATA KUSHIRIKIANA NA WANAMUZIKI KABLA YA KUTOA MAAMUZI

Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel

.

Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard 

Na Dotto Mwaibale
 
Umoja wa Wanamuziki Tanzania ( TAMUFO) imeliomba Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)  kuhakikisha linashirikisha wadau wa muziki kabla ya kutoa maamuzi ya kuwabana wasanii.

Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stella Joel  jijini Arusha jana baada ya kutokea malalamiko ya wanamuziki kulalamikia kitendo cha Basata kuweka utaratibu wa kuwataka wanamuziki nyimbo zao zikaguliwe baada ya kurekodi kwa sababu za kimaadili.

"Jambo hilo ni kuwaumiza wanamuziki wa Tanzania ambao wanahangaika sana kuwezakumudu gharama za kurekodi kazi zao" alisema Joel.

Joel alisema wanamuziki wengi hawana kipato cha kutosha na kurudia rudia katika kurekodi kazi zao na bado hawajaweza kufaidika nazo.

Mlezi wa TAMUFO, Frank Richard, ameiomba Serikali kuziwezesha taasisi zenye nia ya kusaidia maendeleo ya sanaa hapa nchini Ikiwemo Basata.

Richard aliomba kuwepo na 
 utaratibu wa kuandaa semina kwa ajili ya kutoa elimu ya kuwajengea uelewa wasanii juu ya kazi zinazokubalika kimaadili na katika kulinda heshima ya muziki na utamaduni wa Tanzania.

Aidha Richard ameomba Serikali kuhakikisha idadi ya studio zote hapa nchini zinajulikana ili kuweza kutoa elimu kupitia vipeperushi vinavyozungumzia maadali na taratibu zinapaswa kufuatwa kabla ya kutoa wimbo.

Alisema hali hiyo itaepusha hasara zinazosabisha msanii kurudia wimbo pia kuepusha malalamiko hayo yanayojitokeza.

Richard alisema taasisi zinazosimamia kazi za sanaa na wasanii kwa Ujumla ni muhimu ziandae vipindi vya Redio na Tv na mitandao ya Kijamii kwa ajilo ya kutoa elimu kwa wasanii na wamiliki wa studio  ili kuwajengea uelewa   juu ya jambo hilo.

WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA MABOLOZI WANNE, KUPOKEA NAKALA YA HATI YA UTAMBULISHO

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kuzungumza na mabalozi wanne wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na kupokea nakala ya hati ya utambulisho ya balozi mteule wa Msumbiji hapa nchini.

Mabalozi waliokutana na Waziri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba, Balozi wa Indonesia Mhe. Ratlan Pardede, Balozi wa Sweden Mhe. Anders Sjöberg na Balozi wa Norway  Elisabeth Jacobsen.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akipokea nakala ya hati ya utambulisho ya Balozi Mteule wa Msumbiji hapa nchini  Ricardo Ambrosio Sampaio Mtumbuida katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mulamula na mabalozi hao wamejadili juu ya kuimarisha na kuongeza ushirikiano baina ya mataifa wanayoyawakilisha hapa nchini na Tanzania.    

 “Leo nimekutana na mabalozi kadhaa wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, akiwemo Balozi wa Rwanda, Sweden, Norway na pia nimepokea nakala ya hati ya utambulisho ya balozi mteule wa Msumbiji na kuwahakikishia ushirikiano wetu kama wizara, kama nchi katika kuboresha na kukuza mahusiano yetu,” amesema Balozi Mulamula

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Nae Balozi wa Rwanda hapa nchini, Meja Jenerali Charles Karamba amesema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda ni mzuri hivyo wataendelea kuudumisha uhusiano huo kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Nchi zetu mbili zimekuwa zikishirikiana vizuri hivyo tumekubaliana kuendelea kudumisha ushirikiano huu kwani Watanzania na Wanyarwanda ndugu na marafiki,” amesema Balozi Karamba

Kwa upande wake Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Ratlan Pardede amesema Indonesia na Tanzania zitaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo uchumi, utalii na kijamii na kuhakikisha kuwa ushirikiano huo unazidi kuimarika.

Balozi wa Sweden nchini,  Anders Sjöberg akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati balozi huyo alipomtembelea Waziri ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

“Tumejaribu kuwahamasisha wawekezaji kutoka Indonesia kuja kuwekeza hapa Tanzania na hadi sasa kampuni kumi (10) zimewekeza katika sekta za biashara na uwekezaji, madini, uvuvi, ujenzi na viwanda,” amesema Balozi Pardede     

Nae Balozi wa Sweden  Anders Sjöberg amesema kuwa Sweden itaendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, utunzaji wa mazingira na masuala ya kijamii kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki za binadamu.

Mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Ratlan Pardede yakiendelea.

“Tumejadiliana kuhusu kuimarisha mahusiano, biashara na uwekezaji, utunzaji wa mazingira pamoja na masuala ya kijamii kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu,” amesema Balozi Sjöberg.

Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen amesema Norway na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri ambapo kwa sasa Norway inaangalia fursa za uwekezaji na biashara hapa nchini ili kuimarisha mahusiano na kukuza uchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Meja Jenerali Charles Karamba katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kulia ni baadhi ya Wakurugenzi na Afisa kutoka Wizarani.

“Norway itaendela kutumia fursa za uwekezaji na biashara zilizopo Tanzania ili kuimarisha mahusiano yetu na kukuza uchumi wa pande zote mbili,” amesema Balozi Jacobsen

Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Msumbiji hapa nchini Mhe. Ricardo Ambrosio Sampaio Mtumbuida.

MAWAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI WA EAC WAKUBALIANA KUBORESHA TUME YA KISWAHILI

Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Mashauriano ya Kibajeti umefanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 2021 huku Mawaziri hao wakikubaliana na hoja ya kuiboresha Tume ya Kiswahili ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi badala ya kuivunja.

Awali hoja ya kuivunja Tume ya Kiswahili iliwasilishwa kupitia ripoti ya mshauri mwelekezi na kuungwa mkono na takriban Nchi zote Wanachama isipokuwa Tanzania  kama moja ya mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji ndani ya Jumuiya. Hata hivyo,nchi hizo ziliafiki kwa kauli moja hoja zilizolizotolewa na Tanzania kuhusu umuhimu wa Tume hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alieleza umuhimu wa Tume hiyo na kwamba ni kielelezo pekee muhimu cha Jumuiya na kuwataka kuunga mkono hoja ya kuiboresha na kuiimarisha ili iendelee kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

“Hoja ya kuvunja Tume ya Kiswahili kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa Jumuiya inalenga kudidimiza malengo na misingi iliyopo ya kuiunganisha jumuiya. Hivyo nasisitiza kuwa bado upo umuhimu mkubwa wa kuienzi Tume hiyo ambayo ni kielelezo muhimu cha Jumuiya  badala ya kufikiria kuivunja” alisema Mhe. Nchemba.

Awali, akifungua mkutano huo, Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Ukur Yatani Kanacho,  alisema ana matarajio makubwa mkutano huo utafanyika kwa mafanikio na kutoa pole kwa niaba ya Mawaziri walioshiriki Mkutano huo kwa Ujumbe wa Tanzania na Serikali kwa ujumla kwa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Pia alitoa pole kwa Nchi Wanachama kufuatia janga la ugonjwa wa Corona na kuwataka wajumbe kuendelea kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine umepokea na kujadili agenda mbambali zilizowasilishwa ikiwemo taarifa za Kamati zinazoshughulikia masuala ya Fedha ikiwemo ile ya Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Nchi Wanachama pamoja  na taarifa ya Utafiti wa kuboresha Mifumo na Miundo ya Uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na rasilimali zilizopo.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo umewahusisha pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji Uchumi na Ajira Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga, Waziri, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,   Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina HK. Shaaban na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.

Mkutano huo ambao umeitishwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulitanguliwa na kikao cha Ngazi ya Wataalam kutoka Sekta za Fedha na Uchumi uliofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika tarehe 6 Mei 2021.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 2021. Mkutano huo ulitanguliwa na vikao vya Wataalam  na Makatibu Wakuu vilivyofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 6 Mei 2021. Kulia ni Waziri, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali na kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga akichangia jambo wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kushoto ni Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina HK. Shaaban
Ujumbe wa Burundi ukiongozwa na Mhe. Balozi Ezechiel Nibigira (katikati) wakishiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Wajumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mhe. Waziri Nchemba kwa pamoja na Mawaziri kutoka Zanzibar wakifuatilia Mkutano. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji, Uchumi na Ajira Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga

Mhe. Balozi Nibigira kutoka Burundi akichangia jambo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na Kamishna Msaidizi, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. James Msina

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Elias Bagumhe akiwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Ujumbe wa Tanzania

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania

Mkutano ukiendelea

Wajumbe wakifuatilia mkutano

Mkutano ukiendelea

Friday, May 7, 2021

KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA SEKTA YA FEDHA NA UCHUMI WA EAC CHAFANYIKA ARUSHA

Kikao cha Makatibu Wakuu wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kimefanyika Arusha tarehe 6 Mei 2021.


Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kukamilisha agenda mbalimbali za msingi zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Mashauriano ya Kibajeti unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 Mei 2021.

Miongoni mwa Agenda zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi ni pamoja na Taarifa ya Utafiti wa Kuboresha Mfumo na Muundo wa Uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na Rasilimali zilizopo pamoja na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza hilo la Kisekta.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu unaongozwa na Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar na kuhudhuriwa pia na Bi. Amina KH. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil akizungumza kama kiongozi wa ujumbe wa Tanzania wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wanaoshughulikia Sekta ya Fedha na Uchumi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika jijini Arusha tarehe 6 Mei 2021 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi unaotarajiwa kufanyika jijini humo tarehe 7 Mei 2021. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina KH. Shaaban.

Ujumbe wa Burundi ukiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu wanaoandaa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na uchumi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki

Ujumbe wa Uganda nao ukishiriki kikao cha Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukishiriki kikao cha Makatibu Wakuu

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ukiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. James Msina

Kamishna wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja (kulia) akiwa na Kamishna wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Said Athumni wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta ya Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha Makatibu Wakuu

Kikao kikiendelea

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania

Ujumbe wa Tanzania

Wajumbe wakifuatilia kikao

Kikao kikiendelea

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM,KUZUNGUMZA NA WAZEE LEO JIONI





 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021.

Thursday, May 6, 2021

MPANGO WA KITAIFA WA RASILIMALI WATU UMEANDALIWA KUSIMAMIA NA KUWEZESHA MATUMIZI MAZURI YA RASILIMAL IWATU SERIKALINI


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael akifungua kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Bw. Elisante Mbwilo akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael kufungua kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Dkt. Edith Rwiza akiwasilisha mada kuhusu Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu kwa Washiriki wa kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma baada ya kufungua kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Rasilimaliwatu TAMISEMI Bw. Marko Masaya akizungumzia umuhimu wa Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu unaojadiliwa na unaojadiliwa jijini Dodoma na wadau kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma.


Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 06 Mei, 2021

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael amesema, Serikali kupitia Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu imeandaa rasimu ya Mwongozo wa Kitaifa wa Mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma utakaowezesha kuainisha mahitaji sahihi ya kitaifa ikiwa ni pamoja na kuwezesha usimamizi na matumizi mazuri ya rasilimaliwatu.

Dkt. Michael amesema hayo leo jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI wakati akifungua kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Dkt. Michael amesema, bila kuwa na mpango wa rasilimaliwatu, Serikali inaweza kupata changamoto ya upungufu wa watumishi au kuwa na watumishi wengi wanaotosheleza kwa idadi lakini hawana ujuzi wa kutekeleza majukumu yao kikamilifu, hivyo ndio maana Serikali imeona umuhimu wa kuhuisha Mpango wa Rasilimaliwatu wa Kitaifa.

Amefafanua kuwa, ili kufikia uchumi wa kati wa juu kupitia Sera ya Maendeleo ya Viwanda ni dhahiri kuwa Utumishi wa Umma unapaswa kuwa na watumishi wa kutosha na wenye sifa stahiki hivyo amewataka washiriki kutumia uzoefu wao kujadili kwa kina rasimu ya mpango huo kwa lengo la kuiwezesha Serikali kupata mwongozo mzuri wa kuandaa Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu utakaokuwa na tija kwa maendeleo ya taifa.

“Tumieni uzoefu wenu na elimu mliyonayo pamoja na ubunifu ili kuiwezesha Serikali kupata Mpango Mzuri wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu.” Dkt. Michael amesisitiza.

Kwa upande wa washiriki, Mkurugenzi Msaidizi Utawala wa Wizara ya Maji Bi. Wanyenda Kuta amesema, Mpango huo wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu utawezesha Utumishi wa Umma nchini kuwa na rasilimaliwatu yenye sifa na kukidhi utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Naye, Mkurugenzi Msaidizi Rasilimaliwatu TAMISEMI, Bw. Marko Masaya amesema kuwa, Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu utaziwezesha Taasisi za Umma kuandaa mipango ya kati, muda mfupi na mrefu  itakayosaidia kuwa na watumishi wenye sifa stahiki na malengo yanayopimika na kuongeza kuwa utawezesha kujua aina ya watumishi wanaohitajika na sehemu watakayopatikana aidha ndani au nje ya Utumishi wa Umma.

Sanjali na hilo, Bw. Masaya ameongeza kuwa, mpango huo utaiwezesha Serikali kujua katika kipindi cha miaka miwili au mitatu ijayo itahitaji kuwa na watumishi wa aina gani, wenye weledi upi na kiwango kipi cha elimu.

Kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kimejumuisha wasimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

UVCCM SINGIDA YAANZA ZIARA YA KIKAZI WILAYA YA IRAMBA

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt.Denis Nyiraha, akizungumza na vijana wa chama hicho wa Wilaya ya Iramba baada ya kuanza ziara ya kikazi  na kamati ya utekelezaji jana.

Ziara ikiendelea.
Safari ya kuelekea kukagua miradi ya maendeleo ikifanyika.
 
Na Mwandishi Wetu, Iramba

Mwejikiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Dkt.Denis Nyiraha ameiomba Serikali kutoa kwa wakati gawio la asilimia nne kwa vijana.  

Nyiraha alitoa ombi hilo jana wakati alipokuwa na Kamati ya utekelezaji katika ziara ya kikazi  wilayani Iramba ambapo  walitembelea vikundi viwili vya vijana vilivyonufaika na asilimia 4 ya mkopo kutoka halmashauri.

"Naiomba Serikali itoe gawio 
hilo wa wakati  na kwa mgao sawa ili iweze kuwa daraja la maendeleo kwa vijana wetu na kwa taifa zima."alisema Nyiraha.

Wajumbe wa  kamati hiyo pia 
 walikagua ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM wilayani humo na kuitaka kamati ya ujenzi kumaliza  haraka jengo hilo.

"Haya na mimi natoa hii laki moja kwa ajili ya kuchangia juhudi za kumalizia jengo hili pia nawaomba watu wote walio toa ahadi basi wamalizie kutoa kwa wakati ili tufikie malengo yetu." alisema Nyiraha.

Katika hatua nyingine  Dkt.Nyiraha alifanya vikao vya ndani lengo likiwa  kukagua uhai wa jumuiya na chama katika Kata ya Kiomboi, Ulemo na Kata Ya  Kyengege.

Wakiongea kwa nyakati tofauti viongozi wa vikundi vya vijana walio patiwa mikopo ya asilimia 4. kutoka halmashauri wameushukuru umoja wa UVCCM kwa kuwapigania na kuwaweka pamoja na kuwa na uwezo wa kukopesheka bila vikwazo.

Kamati hiyo ya utekelezaji chini ya Dkt.Nyiraha leo  itaendelea na ziara hiyo Singida mjini.