Kikao
cha Makatibu Wakuu wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi kutoka
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kimefanyika Arusha tarehe 6
Mei 2021.
Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kukamilisha
agenda mbalimbali za msingi zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 12 wa
Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na
Uchumi pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuhusu Mashauriano ya Kibajeti unaotarajiwa kufanyika tarehe 7
Mei 2021.
Miongoni mwa Agenda zitakazowasilishwa kwenye Mkutano
wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi ni pamoja na
Taarifa ya Utafiti wa Kuboresha Mfumo na Muundo wa Uendeshaji wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki kulingana na Rasilimali zilizopo pamoja na kupokea
Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa
Mkutano wa 11 wa Baraza hilo la Kisekta.
Ujumbe wa Tanzania
kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu unaongozwa na Dkt. Juma Malik
Akil, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar na
kuhudhuriwa pia na Bi. Amina KH. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu kutoka
Wizara ya Fedha na Mipango.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma
Malik Akil akizungumza kama kiongozi wa ujumbe wa Tanzania wakati wa
kikao cha Makatibu Wakuu wanaoshughulikia Sekta ya Fedha na Uchumi
kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika
jijini Arusha tarehe 6 Mei 2021 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 12 wa
Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi unaotarajiwa kufanyika
jijini humo tarehe 7 Mei 2021. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi. Amina KH. Shaaban.
Ujumbe
wa Burundi ukiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu wanaoandaa Mkutano wa
12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na uchumi kutoka Jumuiya ya
Afrika Mashariki
Ujumbe wa Uganda nao ukishiriki kikao cha Makatibu Wakuu
Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukishiriki kikao cha Makatibu Wakuu
Sehemu
nyingine ya ujumbe wa Tanzania ukiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar,
Bw. Mussa Haji Ali na Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. James Msina
Kamishna
wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William
Mhoja (kulia) akiwa na Kamishna wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania, Bw. Said Athumni wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta
ya Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment