Matokeo chanyA+ online




Saturday, October 7, 2023

MAKAMU WA RAIS AKIONGOZA MAPOKEZI YA KARDINALI RUGAMBWA















 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema serikali itaendelea na kufanya kazi na kushirikiana vema na Kanisa Katoliki pamoja na madhehebu mengine ya dini hapa nchini.

 

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa mapokezi ya Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea Vatican alipopewa hadhi ya Ukardinali. Amempongeza Kardinali Rugambwa kwa kuendelea kuhubiri amani na umoja wa Watanzania na kumsihi kuendelea kuwa chachu ya amani, upendo na umoja. Makamu wa Rais amesema ni baraka kwa Taifa la Tanzania kupata Kardinali wa tatu.

 

Kwa upande wake Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa amewaomba watanzania wa kila dini kuendelea kumuombea ili aweze kufanya vema kazi hiyo kwa uaminifu na kuweza kuleta maendeleo ya mwanadamu kwa ujumla kuanzia hapa nchini kimwili na kiroho na baadaye hata nje ya nchi.

 

Kardinali Rugambwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kanisa, Serikali na watanzania wote waliomtia moyo na kumtumia jumbe mbalimbali za pongezi zilizompa moyo na kumuimarisha. 

SKIMU YA UMWAGILIAJI NSIMBO

 






Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Godfrey Chongolo  akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Ugalla katika Kijiji cha Katambike, wilayani Mpanda, ili kuuwekea mpango wa kuukwamua, baada ya mradi huo kukwama tangu 2007. Ndugu Chongolo amefanya ukaguzi wa skimu hiyo iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 800 wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-25 katika Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ijumaa Oktoba 6, 2023.

WAZIRI MAKAMBA ATUA INDIA KUELEKEA ZIARA YA KIHITORIA YA MHE. RAIS DKT. SAMIA NCHINI HUMO


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. January Makamba akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt.Subrahmanam Jaishankar ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakayoifanya nchini humo kuanzia  tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023. Mazungumzo yao yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya India jijini New Delhi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizunguza na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe.Binaya Srikanta Pradhan jijini New Delhi kabla ya Mhe. Makamba kukutana na Waziri wa mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt. Jaishankar
Mhe. Waziri Makamba akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega wakati wa kikao cha kupokea taarifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na India mara baada ya Mhe. Makamba kuwasili nchini India tarehe 6 Oktoba 2023 kwa ajili ya kutathmini na kukamilisha maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo kuanzia tarehe 8 hadi 1 Oktoba 2023
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega (kulia) akiwa na Mkrugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (kushoto) wakati wa kikao na Mhe. Waziri Makamba (hayupo pichani) baada ya kuwasili nchini India. Wengine katika picha ni Mkuu wa utawala Ubalozini, Bw. Deogratius Dotto na Afisa Mwandamizi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Bi. Latifah

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. John Kambona (kulia) akiwa na Afisa Mwandamizi wa Idara hiyo Bi. Eliet Magogo na Katibu wa Mhe. Waziri Makamba, Bw. Seif Kamtunda wakati wa kikao cha ujumbe wa Tanzania na Mhe. Waziir Makamba (hayupo pichani) jijini New Delhi kuelekea ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023
Mhe. Makamba akizungumza na Mkurugenzi wa masuala ya ushirikiano wa India na Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya India mara baada ya kuwasili nchini humo kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega

Picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt.Subrahmanam Jaishankar ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakayoifanya nchini humo kuanzia  tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika hivi karibuni jijini New Delhi, viongozi hao pamoja na mambo mengine wamelezea matarajio yao ya kuimarika zaidi kwa ushirikiano kati ya Tanzania na India kupitia ziara hiyo ya kihistoria.

Kwa upande wake , Mhe. Makamba amemshukuru mwenyeji wake kwa kumkaribisha nchini humo lakini pia kwa maandalizi mazuri ya ziara ya Mhe.  Rais Dkt. Samia nchini humo.

Kadhalika, Mawaziri hao walibadilishana taarifa kuhusu ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili na kukubaliana kuongeza jitihada ili kufikia malengo ya pamoja ya kuinua kuwango cha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili na kuhakikisha ushirikiano uliopo unazaa matokeo tarajiwa.

Mhe. Rais Dkt. Samia anatarajiwa kuwasili India tarehe 8 Oktoba 2023 kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu.

Wakati  wa ziara hiyo kutashuhudiwa ubadilishanaji wa mikataba  mbalimbali ya ushirikiano katika sekta za uwekezaji, uchukuzi,  afya, maji na nyingine nyingi.

Ziara hiyo pamoja  na mambo mengine inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India hususan  kwenye maeneo ya kimkakati  na manufaa kwa Tanzania ikiwemo afya, maji, elimu uchumi wa buluu,  teknolojia, kilimo, na biashara na uwekezaji. 


 











 

Thursday, September 21, 2023

RAIS, DAKT. SAMIA SULUHU HASSAN AHITIMISHIA ZIARA YAKE MIKOA YA KUSINI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Ikwiriri, Rufiji Mkoani Pwani mara baada ya kuhitimisha Ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 20 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Ikwiriri, Rufiji Mkoani Pwani mara baada ya kuhitimisha Ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 20 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Ikwiriri, Rufiji Mkoani Pwani mara baada ya kuhitimisha Ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 20 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Siti Mketo mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Somanga wakati akihitimisha zara vake katika Mikoa va Kusini tarehe 20 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu zawadi yake ya picha aliyopewa na Siti Mketo wakati akihitimisha ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 20 Septemba, 2023.
Watoto wa Shule a Msingi Somanga wakiwa na shauku va kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposimama eneo hilo kuwasalimia Wananchi wakati akihitimisha ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 20 Septemba, 2023.


Wananchi wa Somanga wakiwa kwenye shamrashamra za kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati aliposimama eneo hilo kuwasalimia Wananchi wakati akihitimisha ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 20 Septemba, 2023.

Thursday, September 7, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba, 2023.

 






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mjadala wa masuala ya Kilimo na Vijana wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Septemba, 2023.