Matokeo chanyA+ online




Wednesday, November 15, 2023

Wagojwa 32,867 watibiwa moyo JKCI kwa kipindi cha miezi mitatu


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.



Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Daktari bingwa wa usingizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhe. Balozi Ulisubisya Mpoki akielezea maendeleo ya Taasisi hiyo tangu kuanzishwa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akichangia mada wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Afisa Manunuzi na Ugavi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Victor Kapama akielezea mchakato wa manunuzi unavyotakiwa kufuatwa wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akijibu hoja zilizohusu idara yake wakati wa kikao cha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo na wafanyakazi kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Na: JKCI

********************************************************************************************************

Wagonjwa 32,867 watu wazima 30,616 na watoto 2,251 wenye matatizo mbalimbali ya moyo wamepata huduma ya matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miezi mitatu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge wakati akisoma taarifa ya kazi zilizofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Oktoba 2023 katika mwaka wa fedha wa 2023/24 katika kikao cha wafanyakazi wa JKCI kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema wagonjwa waliolazwa walikuwa 1,131 kati ya hao watu wazima walikuwa 1030 na watoto 101.

“Kupitia mtambo wa Cathlab ambayo ni maabara inayotumia mionzi maalumu kwaajili ya uchunguzi wa matatizo na tiba za magonjwa ya moyo wagonjwa 638 watu wazima 630 na watoto nane  walipata huduma za uchunguzi, kuzibuliwa mishipa ya damu ya moyo iliyoziba pamoja na kupandikizwa vifaa visaidizi vya moyo”, .

Wagonjwa 129 ambao ni watoto na watu wazima walifanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kubadilishwa valvu, kupandikizwa mishipa ya damu ya moyo (Coronary artery bypass grafting – CABG), kukarabati mishipa ya damu ya moyo iliyotanuka au kuchanika, kuziba matundu ya moyo, kutoa uvimbe katika kifua au mapafu, kupandikiza na kuzibua mishipa ya damu ya miguu.

Dkt. Kisenge alisema kwa kipindi hicho cha miezi mitatu waliona wagonjwa 61 kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Visiwa vya Comoro, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nje ya Africa ambazo ni nchi za Canada, Ufaransa na India.

“Tulifanya vipimo 14,864  vya jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) na mfumo wa umeme wa moyo (ECG), X-Ray 3,815 zilifanyika,  vipimo vya maabara 7,966 na ultrasound 1,881 zilifanyika pia dawa zilitolewa kwa wagonjwa 30,249”, alisema Dkt. Kisenge. 

Mkurugenzi huyo Mtendaji aliwakumbusha wafanyakazi wa JKCI kumtanguliza Mungu mbele katika kazi zao za kila siku huku wakiiombea taasisi hiyo ili iweze kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaowatibu. 

Dkt. Kisenge alisema kutokana na huduma bora inayotolewa katika Taasisi hiyo imekuwa kivutio cha wagonjwa wengi kutoka ndani na nje ya nchi kutaka kutibiwa hapo na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuimarisha huduma za matibabu ya moyo nchini.

Kwa upande wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo waliohudhuria mkutano huo waliishukuru menejimenti ya JKCI kwa kuwaongoza vizuri na kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata maslahi yao kwa wakati.

“Kuna watu wengi wanaohitaji kupata huduma za matibabu ya moyo tunazozitoa, ni jukumu letu kama Taasisi kutangaza huduma zetu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ili tuweze kuwafikia wananchi wengi zaidi”, alisema Jilala John ambaye ni Afisa Uuguzi katika Taasisi hiyo.


Tuesday, October 10, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Profesa Santishree Dhulipudi Pandit kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India





Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023

Walimu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kilichopo New Delhi nchini India wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo hicho Oktoba 10, 2023

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini India wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini humo

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini India wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini humo

Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini India wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini humo

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.


 

WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA WA SERIKALI WA MKOA WA MARA WAMEKUMBUSHWA KUFUATA WELEDI NA TARATIBU ZA KISHERIA KATIKA KUSHUGHULIKIA MASHAURI YA DAWA ZA KULEVYA ILI KUHAKIKISHA MATOKEO MAZURI.

  







Kamishna wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Bi. Veronica Matikila, alitoa mada kuhusu upelelezi na uendeshaji wa kesi za dawa za kulevya katika kikundi cha wapelelezi na waendesha mashtaka.

Mada zilizojadiliwa zilijumuisha aina za ushahidi, jinsi ya kuthibitisha makosa ya dawa za kulevya, na maeneo muhimu ya kuzingatia kwa waendesha mashtaka katika kuongoza upelelezi wa kesi za dawa za kulevya.

Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Mtwara, Joseph Mauggo, alieleza kuwa mafunzo haya yanafanyika kufuatia maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya. Alisisitiza kuwa mafunzo haya yanalenga kuongeza uelewa wa watendaji wa kesi za dawa za kulevya na kutatua changamoto za kiutendaji. Pia, alitaja kwamba Tume iliyoundwa ilibainisha kuwa Serikali inapoteza kesi nyingi kutokana na kutokuwa na uelewa wa pamoja miongoni mwa watendaji wa kesi za dawa za kulevya.

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha uelewa wa wapelelezi na waendesha mashtaka, kutatua changamoto, na kuonyesha jitihada za Serikali katika kushughulikia tatizo la dawa za kulevya nchini Tanzania.

 Mafunzo haya yanaendelea mkoani Mara na yamefanyika awali katika mikoa mingine ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, na Iringa. Jumla ya washiriki 101 wamehudhuria mafunzo haya kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS).

 

Saturday, October 7, 2023

MAKAMU WA RAIS AKIONGOZA MAPOKEZI YA KARDINALI RUGAMBWA















 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema serikali itaendelea na kufanya kazi na kushirikiana vema na Kanisa Katoliki pamoja na madhehebu mengine ya dini hapa nchini.

 

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa mapokezi ya Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam akitokea Vatican alipopewa hadhi ya Ukardinali. Amempongeza Kardinali Rugambwa kwa kuendelea kuhubiri amani na umoja wa Watanzania na kumsihi kuendelea kuwa chachu ya amani, upendo na umoja. Makamu wa Rais amesema ni baraka kwa Taifa la Tanzania kupata Kardinali wa tatu.

 

Kwa upande wake Mwadhama Kardinali Protase Rugambwa amewaomba watanzania wa kila dini kuendelea kumuombea ili aweze kufanya vema kazi hiyo kwa uaminifu na kuweza kuleta maendeleo ya mwanadamu kwa ujumla kuanzia hapa nchini kimwili na kiroho na baadaye hata nje ya nchi.

 

Kardinali Rugambwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kanisa, Serikali na watanzania wote waliomtia moyo na kumtumia jumbe mbalimbali za pongezi zilizompa moyo na kumuimarisha. 

SKIMU YA UMWAGILIAJI NSIMBO

 






Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Godfrey Chongolo  akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Ugalla katika Kijiji cha Katambike, wilayani Mpanda, ili kuuwekea mpango wa kuukwamua, baada ya mradi huo kukwama tangu 2007. Ndugu Chongolo amefanya ukaguzi wa skimu hiyo iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 800 wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-25 katika Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ijumaa Oktoba 6, 2023.

WAZIRI MAKAMBA ATUA INDIA KUELEKEA ZIARA YA KIHITORIA YA MHE. RAIS DKT. SAMIA NCHINI HUMO


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. January Makamba akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt.Subrahmanam Jaishankar ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakayoifanya nchini humo kuanzia  tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023. Mazungumzo yao yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya India jijini New Delhi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizunguza na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe.Binaya Srikanta Pradhan jijini New Delhi kabla ya Mhe. Makamba kukutana na Waziri wa mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt. Jaishankar
Mhe. Waziri Makamba akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega wakati wa kikao cha kupokea taarifa kuhusu ushirikiano wa Tanzania na India mara baada ya Mhe. Makamba kuwasili nchini India tarehe 6 Oktoba 2023 kwa ajili ya kutathmini na kukamilisha maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo kuanzia tarehe 8 hadi 1 Oktoba 2023
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega (kulia) akiwa na Mkrugenzi wa Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (kushoto) wakati wa kikao na Mhe. Waziri Makamba (hayupo pichani) baada ya kuwasili nchini India. Wengine katika picha ni Mkuu wa utawala Ubalozini, Bw. Deogratius Dotto na Afisa Mwandamizi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Bi. Latifah

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. John Kambona (kulia) akiwa na Afisa Mwandamizi wa Idara hiyo Bi. Eliet Magogo na Katibu wa Mhe. Waziri Makamba, Bw. Seif Kamtunda wakati wa kikao cha ujumbe wa Tanzania na Mhe. Waziir Makamba (hayupo pichani) jijini New Delhi kuelekea ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini India tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023
Mhe. Makamba akizungumza na Mkurugenzi wa masuala ya ushirikiano wa India na Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya India mara baada ya kuwasili nchini humo kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega

Picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki   Mhe. January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt.Subrahmanam Jaishankar ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakayoifanya nchini humo kuanzia  tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika hivi karibuni jijini New Delhi, viongozi hao pamoja na mambo mengine wamelezea matarajio yao ya kuimarika zaidi kwa ushirikiano kati ya Tanzania na India kupitia ziara hiyo ya kihistoria.

Kwa upande wake , Mhe. Makamba amemshukuru mwenyeji wake kwa kumkaribisha nchini humo lakini pia kwa maandalizi mazuri ya ziara ya Mhe.  Rais Dkt. Samia nchini humo.

Kadhalika, Mawaziri hao walibadilishana taarifa kuhusu ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili na kukubaliana kuongeza jitihada ili kufikia malengo ya pamoja ya kuinua kuwango cha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili na kuhakikisha ushirikiano uliopo unazaa matokeo tarajiwa.

Mhe. Rais Dkt. Samia anatarajiwa kuwasili India tarehe 8 Oktoba 2023 kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu.

Wakati  wa ziara hiyo kutashuhudiwa ubadilishanaji wa mikataba  mbalimbali ya ushirikiano katika sekta za uwekezaji, uchukuzi,  afya, maji na nyingine nyingi.

Ziara hiyo pamoja  na mambo mengine inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India hususan  kwenye maeneo ya kimkakati  na manufaa kwa Tanzania ikiwemo afya, maji, elimu uchumi wa buluu,  teknolojia, kilimo, na biashara na uwekezaji.