Matokeo chanyA+ online




Tuesday, May 28, 2019

RAIS MAGUFULI AWASILI NCHINI ZIMBABWE KWA ZIARA RASMI YA KITAIFA YA SIKU 2


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe. PICHA NA IKULU

 

WATOTO 20 KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KWA TUNDU DOGO NA WATAALAMU KUTOKA ISRAEL


Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete imepokea wataalamu wa moyo kutoka Canada na Israel ambao watafanya upasuaji kwa  wa moyo kwa watoto 20 ndani ya wiki moja na hiyo ni kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete profesa Mohamed Janabi amesema kuwa taasisi ya Save a Chil's h Heart   kutoka Canada imekuja nchini zaidi ya mara tano kuanzia mwaka 2015 na ujio wao umekuwa na manufaa kwa kuwa walifundisha namna ya kufanya upasuaji kwa tundu dogo na safari hii wamewaalika wenzao kutoka nchini Israel nchi ambayo imetoa mafunzo kwa manesi wa uangalizi maalumu kutoka taasisi hiyo ya JKCI.

Janabi amesema ikiwa ni mara ya pili ya wataalamu hao kufanya upasuaji wa namna hiyo, wamelenga kuokoa maisha ya watoto huku akieleza kuwa upasuaji huo unatumia gharama nafuu na muda wa kulazwa ni mchache zaidi, (takribani siku 2 pekee.)

Amesema kuwa ushirikiano baina ya nchi hizo umekuwa na manufaa hasa katika kubadilishana ujuzi na kukutana kwa madaktari bingwa hao kwa muda wa wiki moja kutakuwa ni kwa kujifunza baina ya pande zote mbili.

Awali akieleza historia na majukumu yanayofanywa na taasisi hiyo Profesa Janabi amesema kuwa mikakati ya taasisi hiyo ni kuzidi kuwahudumia watoto wenye matatizo hayo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Amesema kuwa Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa ushirikiano katika kuhakikisha matibabu ya watoto hao yanafanikiwa na tayari mwezi uliopita manesi 2 wamepelekwa Nairobi, Kenya kwa ajili ya mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya Save a Child's Heart kutoka Canada Marni Brinder Byk amesema kuwa taasisi hiyo imedhamiria kuokoa maisha ya watoto pamoja na kudumidha mahusiano bora yenye tija kwa sasa na baadaye.

Brinder amesema kuwa wamefurahi sana kuja Tanzania na wanataraji kujifunza mengi kutoka taasisi hiyo pamoja na kudumisha mahusiano bora hapo mbeleni

Vilevile wakili na Mkurugenzi wa taasisi ya Save a Child's Heart kutoka Israel Simon Fisher amesema kuwa Tanzania ni nyumbani na wanaamini wataendelea kusaidia watoto Tanzania na kote duniani katika kuokoa maisha yao.
WhatsApp%2BImage%2B2019-05-27%2Bat%2B4.20.18%2BPM
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Janabi Mohamedi akizungumza wakati kutambulisha ugeni wa madaktari bingwa kutoka Israel ambao watafanya upasuaji kwa watoto 20 ndani ya wiki moja, leo jijiji Dar es Salaam.
WhatsApp%2BImage%2B2019-05-27%2Bat%2B4.20.19%2BPM
 Wakili na Mkurugenzi wa Taasisi ya Save a Child's  Heart kutoka Israel Simon Fisher akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa wamedhamiria kuokoa maisha ya watoto hao pamoja na kudumisha mahusiano bora ya sasa na baadaye, leo jijini Dar es Salaam.
WhatsApp%2BImage%2B2019-05-27%2Bat%2B4.20.21%2BPM
 Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.
WhatsApp%2BImage%2B2019-05-27%2Bat%2B4.20.15%2BPM
Wataalamu na madaktari bingwa kutoka Israel na Canada (walioketi mstari wa mbele) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Profesa Mohamed Janabi wakati wa kikao kazi kitakachowakutanisha madaktari hao katika kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto 20, leo jijini Dar es Salaam
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

NAIBU SPIKA AKUTANA NA MKURUGENZI UNDP


NAIBU-SPIKA-1
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ndugu Verity Nyagah alipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. 
NAIBU-SPIKA-2 NAIBU-SPIKA-3

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA SHADA LA MAUA KATIKA MAKABURI YA MASHUJAA WA NCHI YA NAMIBIA KATIKA ENEO LA HEROES’ ACRE JIJINI WINDHOEK NAMIBIA

3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuweka shada la maua.
 1..
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuwasili katika eneo hilo
1.

4
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka pamoja na mwenyeji wake Rais wa Namibia Hage Geingob mara baada ya kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre
5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Namibia Hage Geingob mara baada ya kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre
6
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha nyama cha Meatco kilichopo jijini katikati mwa mji wa Windhoek Namibia. PICHA NA IKULU 
7

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2019 ametembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa (Heros Acre) waliopigania ukombozi wa Namibia, lililopo nje kidogo ya Jiji la Windhoek nchini humo. 

Katika eneo hilo wamezikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia ambao baadhi yao walipata mafunzo katika kambi ya Kongwa nchini Tanzania, wengine walikuwa maafisa wa Chama cha SWAPO ambao ofisi zao zilikuwa Jijini Dar es Salaam na wengine ni viongozi wakuu walioendesha mapambano wakiwa nchini Namibia. 

Baadhi ya mashujaa waliozikwa katika eneo hilo ni Ndimo Hamaambo, Peter Nanyemba, Theo-Ben Gurirabo na Toiro ya Toire. 

Mhe. Rais Magufuli ameongozana na mwenyeji wake Mhe. Rais Hage Geingob. 

Baada ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha nyama cha kampuni Meatco kilichopo Jijini Windhoek na kuelezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Jannie Breytenbach kuwa kiwanda kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 630 kwa siku, kimeajiri wafanyakazi 650 na kwamba kampuni hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania kuanzisha viwanda vya nyama. 

Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Barani Afrika na ameikaribisha kampuni ya Meatco kuja kuwekeza nchini Tanzania. 

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi. 

Kabla ya kuondoka nchini Namibia kwenda nchini Zimbabwe ambako anakwenda kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Pili wa Namibia Mhe. Hifikepunye Pohamba Jijini Windhoek. 

Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Windhoek 
28 Mei, 2019

RAIS MAGUFULI PAMOJA NA RAIS WA NAMIBIA WAZINDUA MTAA JULIUS K. NYERERE KATIKA JIJI LA WINDHOEK NCHINI NAMIBIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimweleza Mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob alichokiandika kwenye kitabu cha kumbukumbu kwa Lugha ya Kiswahili Katika kuhakikisha Kiswahili kinatangazwa kimataifa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Jijini Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimweleza Mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob alichokiandika kwenye kitabu cha kumbukumbu kwa Lugha ya Kiswahili Katika kuhakikisha Kiswahili kinatangazwa kimataifa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Jijini Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob kuashiria uzinduzi rasmi wa mtaa Julius K. Nyerere ulipo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob alipokuwa akimuonyesha Makongoro Nyerere mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mtaa mpya unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob mara baada ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob mara baada ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob wakati wa hafla ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia. Mei 27, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob wakati wa hafla ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia. Mei 27, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza Watanzania wanaoishi Namibia mara baada ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019


RAIS MAGUFULI AWASILI NCHINI NAMIBIA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS WA NAMIBIA HAGE GEINGOB KATIKA IKULU YA NCHINI NAMIBIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Namibia kulia kwake ni Rais wa Namibia Mheshimiwa Hage Geingob akishuhudia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Namibia kulia kwake ni Rais wa Namibia Mheshimiwa Hage Geingob akishuhudia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Hage Geingob wakati wa nyimbo za mataifa mawili zikipigwa katika viwanja vya Ikulu ya Namibia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la Heshma aliloandaliwa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Namibia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Hage Geingob mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Hage Geingob mara baada ya kuwasili Namibia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo yake na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Hage Geingob mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza  ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Hage Geingob ambaye alikuwa akiongoza ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu hiyo ya Namibia. PICHA NA IKULU