Matokeo chanyA+ online




Tuesday, September 29, 2020

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM, RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA MAFINGA


Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili Mafinga kwa ajili ya kuwahutubia wakazi wa eneo hilo wakati akitokea mkoani Iringa


Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi Mafinga mkoani Iringa wakati akielekea Makambako mkoani Njombe katika muendelezo wa Kampeni za CCM leo tarehe 29 Septemba 2020

 


 

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa Mafinga mara baada ya kumaliza kuwahutubia leo tarehe 29 Septemba 2020

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa Mafinga mara baada ya kumaliza kuwahutubia leo tarehe 29 Septemba 2020

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi Mafinga mkoani Iringa wakati akielekea Makambako mkoani Njombe katika muendelezo wa Kampeni za CCM leo tarehe 29 Septemba 2020

 


Sehemu ya Wananchi wa Mafinga wakimsikiliza Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimama Mafinga leo tarehe 29 Septemba 2020

 Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha Kofia Bibi aliyefahamika kwa jina moja Bibi Zainabu mara baada ya kuwahutubia wananchi wa Mafinga mkoani Iringa

MAJALIWA APOKEA WANACHAMA 20 WA CHADEMA BUKOBA MJINI


Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Serikali ya CCM imedhamiria kuhakikisha kilimo kinamnufaisha mkulima wa Tanzania. 

 

"Watu wasije kuwadanganya kwamba Serikali haiwajali, siyo kweli. Kuna sababu zilizochangia kuyumba kwa bei ya kahawa kwenye soko la dunia."

 

Ametoa kauli hiyo  mchana (Jumatatu, Septemba 28, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa Rubale kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Rubale, wilayani Bukoba, mkoani Kagera.

 

"Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani, iliazimia kufufua mazao matano ya kimkakati ambayo ni kahawa, pamba, korosho, chai na tumbaku. Mazao haya bei ilishuka na si katika zao la kahawa tu."

 

"Kuyumba kwa bei haikuwa katika zao la kahawa tu bali katika mazao mengine kama pamba na korosho.  Kahawa bei yake iliathirika kwa sababu ya ugonjwa wa Corona. Korosho bei ilishuka kutoka sh.3,300 hadi sh. 1,900. Pamba pia ilishuka bei," amesema. 

 

Amesema Kenya ndiko mnada wa kahawa huwa unafanyika lakini hadi sasa bado wanasumbuliwa na ugonjwa wa Corona kwa hiyo haikuwa rahisi kufanya biashara katika kipindi chote hicho.


Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewapokea wanachama 20 kutoka Chama cha Demokrasia (CHADEMA) ambao wameamua kurudi CCM.


Wanachama hao wameongozwa na Mwenyekiti wa Vijana wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera, Bw. Francis Mutachunzibwa ambaye pia alimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA, Bi. Getrude Ndibalema ambaye alijiuzulu uongozi tangu mwaka jana.

 

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Bw. Mutachunzibwa alisema: “Ninaijua vizuri CHADEMA, nilipotea, nilitenda dhambi lakini sasa nimeamua kurudi nyumbani, nipokeeni.”

 

“Ninawaomba wana-Bukoba tumchague Dkt. Magufuli, mashine ya kusaga na kukoboa, jembe la nguvu. Kuanzia kesho, nitamnadi yeye na Advocate Byabato hadi kieleweke.”

 

Akizungumza na maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba leo jioni (Jumatatu, Septemba 28, 2020) waliojitokeza kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, Mheshimiwa Majaliwa aliwataka wakazi hao wajitafakari sana wanapofikiria kumchangua mtu wa kuongoza nchi.

 

“Tunataka kiongozi mwenye hofu ya Mungu na ili umpate ni lazima umjue historia yake. Kuongoza nchi si lelemama, kiongozi wa nchi ni Mkuu wa Nchi, tena ni Mkuu wa Majeshi.”

Monday, September 28, 2020

MGOMBEA MWENZA WA URAIS KWA TIKETI YA CCM SAMIA SULUHU HASSAN, AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA IRKIUSHIOBR NA KIJIJI CHA SIMANJIRO



 


Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa kijiji cha Irkiushiobr na kijiji cha Simanjiro alipokuwa njiani akielekea Wilaya ya Babati Vijijini Mkoani Manyara kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa  kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM leo Septemba 28,2020.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


 

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Wilaya ya Babati Vijijini alipowasili katika Uwanja wa Galapo Babati vijijini Mkoani Manyara leo Septemba 28,2020 kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa  kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM leo Septemba 28,2020

 

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Jimbo la Kongwa Dodoma wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa  Galapo Wilaya Babati Vijijini Mkoani Manyara leo Septemba 28,2020.

 

 Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubi Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Wilaya ya Babati Vijijini mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa  Galapo Babati Vijijini Mkoani Manyara leo Septemba 28,2020.


    

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MPUGUZI KATIKA JIMBO LA DODOMA MJINI



Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Mpuguzi katika Jimbo la Dodoma mjini wakati akiwa njiani kuelekea katika mikutano ya Kampeni za CCM mkoani wa Iringa leo tarehe 28 Septemba 2020


 


 

Wananchi wa Mpuguzi mkoani Dodoma wakishangilia mara baada ya Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kusimama katika eneo hilo leo tarehe 28 Septemba 2020 wakati akielekea mkoani Iringa.

 









 

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Manzase Mvumi mkoani Dodoma wakati akielekea mkoani Iringa leo tarehe 28 Septemba 2020

 


Sunday, September 27, 2020

MGOMBEA MWENZA WA URAIS KWA TIKETI YA CCM SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MKUTANO WA KAMPENI KIBAYA, KITETO MKOANI MANYARA

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana Mtoto Leopatra Michael (6) Mwanafuzi wa Darasa la 2 katika Shule ya Msingi Ndachi Kongwa Mkoani Dodoma alipokutana nae katika Kijiji cha Songambele akiwa njiani akielekea katika Uwanja wa  Shule ya Sekondari Zoisa Kongwa kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa Uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM Septemba 27, 2020

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi kitabu cha Ilani ya utekelezaji wa CCM 2020/25  Mbunge mteule wa Jimbo la Kongwa Dodoma Mhe. Job Ndugai kwenye Mkutano wa Uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika Septemba 27,2020 katika Uwanja wa  Shule ya Sekondari Zoisa Mkoka Kongwa Mkoani Dodoma. 

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Jimbo la Kongwa Dodoma wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  alipokuwa akihutubia mkutano wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM Septemba 27, 2020 zilizofanyika katika Uwanja wa  Shule ya Sekondari Zoisa Mkoka Kongwa Mkoani Dodoma
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Jimbo la Kongwa Dodoma baada ya kuwahutubia Mkutano wa Uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM  Septemba 27, 2020 katika Uwanja wa  Shule ya Sekondari Zoisa Kongwa Mkoani Dodoma.

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Wilaya Kiteto katika Kijiji cha Engusero, Dosidosi na Njia panda Nameroko Kiteto Mkoani Manyara alipokuwa njia akielekea Mkoani Manyara kuanza ziara ya awamu ya tatu ya kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM  Septemba 27, 2020
 
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM Septemba 27, 2020 zilizofanyia katika Uwanja wa  Kibaya Kiteto Mkoani Manyara.

Chama cha Mapinduzi CCM kikiendelea kuchanja mbuga Angani na Ardhini, Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Septemba 27,2020 amezindua awamu ya tatu ya kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa  Shule ya Sekondari Zoisa Kongwa Mkoani Dodoma.

 

VITAMBULISHO VYA WAMACHINGA VIMETUTUA MZIGO - MACHINGA KILIMANJARO


Na, Pius Ntiga, Moshi.

Wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga katika Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, wamesema Vitambulisho wa Wajasiriamali wadogo vimewatua Mzigo, hivyo wanawashangaa baadhi ya Wanasiasa wanaopotisha kuhusu Vitambulisho hivyo.

Wakizungumza na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru FM inayoangazia Mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, Wafanyabiashara hao wamesema utamu wa Vitambulisho hivyo wanaujua wao.

 Wamesema awali walikuwa wanalipa Shilingi 500 kwa siku, sawa na shilingi 182,000 kwa mwaka, kiasi ambacho wamesema ni kikubwa ukilinganisha na shilingi 20,000 wanayolipa sasa kwa mwaka.

"Tulikua tukilipa shilingi 200 ya usafi kwa siku, sawa na shilingi 73,000 kwa mwaka, ambapo sasa mateso kama hayo hatuyapati Tena tunashukuru sana Rais Magufuli kwa kutuona na tutampa zawadi mwaka huu" wamesema Machinga.

Kwa mujibu wa Wafanyabiashara hao wadogo, Mkombozi wao ni rais Magufuli amekuja na Mpango wa shilingi 20,000 tu kwa mwaka, na sasa kero za Migambo kutufukuza hazipo tena.

" Nikwambie tu kuwa Mabenki nayo yamesema kwa kuwa tuna Vitambulisho, shughuli zetu zimerasimishwa sasa, hivyo tumeanza kupewa mikopo, huku Vitambulisho vikiwa ni dhamana yetu". Wamesema

Wamesema hivi sasa hawasumbuliwi tena na askari wa jiji wala mgambo kama ilivyokuwa hapo awali "Vitambulisho vya wamachinga vimetusaidia sana, tunanunua kwa ridhaa yetu, hatulazimishwi" Wamesema Machinga.

Aidha, wamefafanua kuwa uwepo wa Vitambulisho hivyo vimeaaondolea kero na kwa sasa Biashara yao imeimarika zaidi na kipato chao kimeongezeka na wamefanikiwa kununua Ardhi na kujenga Nyumba.

Kutokana na mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Moshi, Michael Mwandezi, amesema tangu kuanza kwa utaratibu huo zaidi ya Asilimia 70 ya Wamachinga wamepatiwa Vitambulisho katika Manispaa ya Moshi.

Mwandezi amesema fedha inayotokana na vitambulisho hivyo kuenda Hazina na kisha kurudishwa katika Manispaa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo ambayo inawagusa moja kwa moja wananchi.

"Pia tumewasaidia hawa wajasiriami kuwajengea uwezo wa kimtaji ambapo sasa wanakopesheka kupitia Vitambulisho, hivyo vimewanufaisha kwa kukopa fedha Benki". Amesema Mkurugenzi.

Hivi karibuni baadhi ya Wanasiasa wamekuwa wakipotosha kuhusu Vitambulisho hivyo vya Wamachinga kuwa haviwanufaishi na badala yake wanaibiwa, kauli ambayo Rais John Magufuli ambaye ni Mgombea wa Urais Kupitia CCM, amewataka wafanyabiashara hao kuwapuuza Wanasiasa na badala yake waunge juhudi za serikali za kuwakomboa Wamachinga.



Friday, September 25, 2020

MOROGORO YAJIPANGA KUWA KINARA UZALISHAJI KOROSHO KWA TIJA


Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, Dkt.Geradina Mzena (kulia), akiwaelekeza Afisa Kilimo na Mratibu wa Zao la Korosho Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Isabella Chilumba (kushoto) na  Afisa Kilimo wa Wilaya ya Gairo, Eunice Kyungai jinsi ugonjwa wa Ubwiriunga unavyoathiri zao la korosho. Mafunzo hayo kwa vitendo yalifanyika jana kwenye shamba la korosho la Shule ya Msingi Mnjilili wilayani Gairo, Morogoro.  

Mtafiti Mwandamizi na Mdhibiti wa Visumbufu vya Wadudu na Magonjwa kwenye zao la korosho, kutoka Tari- Naliendele  Mtwara, Dkt.Wilson Nene, akiwaeleza  Maafisa Ugani na Wakulima namna ya kudhibiti magonjwa mbalimbali ya zao hilo.
Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa shamba, kulipima na upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Maafisa Ugani na Wakulima wakijifunza kwa vitendo namna ya upimaji wa shamba la korosho kabla ya kupanda.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Madege Wilaya ya Gairo, Fideli Ntumo (Aliye chuchumaa akipima shamba kwa kamba katika mafunzo hayo ya vitendo. 
Mkulima Julius Senyagwa kutoka Kijiji cha Majawanga wilayani Kilosa,  akijifunza namna ya kuweka 'mambo' wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Gairo, Mary Gasper (kulia) na wenzake,  akijifunza namna ya kuweka 'mambo' wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho. Kushoto ni Afisa Kilimo, Lucy Mushi na Jacquline Roland.
Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Gairo, Laya Abbas,  akijifunza namna ya kuweka mambo wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Mtafiti Mwandamizi na Mdhibiti wa visumbufu vya wadudu na magonjwa kwenye zao la korosho, kutoka Tari- Naliendele  Dkt.Wilson Nene, akiwaonesha kwa vitendo Maafisa Ugani na Wakulima namna ya kudhibiti magonjwa mbalimbali ya zao hilo.

Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Gairo, Nasibu Said, akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo kabla ya kupanda miche bora ya mikorosho katika shamba hilo lililopo shule ya Msingi Mnjilili, Gairo.


Mkulima  Elizabeth Senyagwa kutoka Gairo,  akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba hilo la mfano la korosho la Shule ya Msingi Mnjilili.


Mtafiti  kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya kupanda mche wa korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima.


Mtafiti wa Kilimo kutoka  Tari Naliendele, Selemani Libaburu,  akitoa mafunzo ya jinsi ya kuchanganya viuatilifu na maji  kwa Maafisa Ugani na Wakulima kabla ya kupulizia kwenye mikorosho. 

Mtafiti wa Kilimo kutoka  Tari Naliendele, Selemani Libaburu, akionesha namna ya kupulizia viuatilifu kwenye mikorosho.


Afisa Kilimo kutoka Kata ya Magubike wilayani  Kilosa, Iston Kutita, akijifunza kwa vitendo namna ya kupulizia viuatilifu mikorosho.


Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Morogoro.

Wakulima wa zao la korosho mkoani hapa wameahidi kufanya mageuzi makubwa ya kilimo cha zao hilo baada ya kuhamasika na programu maalumu ya mafunzo ya nadharia na vitendo inayoendelea kutolewa na Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi yake ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI)

Taasisi hiyo kupitia kituo chake cha Naliendele kwa sasa kinaendesha mafunzo ya kilimo bora cha zao la korosho kwa wakulima na maafisa ugani wa Halmashauri zilizo kwenye mikoa ya Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini lengo likiwa kuongeza tija na kuinua kiwango cha uzalishaji wa zao hilo.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti wakati wa mafunzo hayo eneo la Shule ya Msingi Mnjilili, Mji Mdogo wa Gairo mkoani hapa wadau hao walisema mafunzo hayo yamekuja wakati mwafaka.

"Mafunzo haya yamenisaidia na kunipa mwanga wa namna ya kuboresha shamba langu la ekari mbili, kwa sasa nina matumaini makubwa ya kulima kitaalam zao hili." alisema mkulima wa korosho kutoka Dumila, Samwel Dede.

Mkulima mwingine Elizabeth Senyangwa kutoka Gairo alisema kabla ya kupata mafunzo hayo miongoni mwetu tulikuwa kwenye mtazamo wa kustawisha zao hilo kimazoea. Lakini kwa sasa nimejifunza mengi hasa kwenye eneo la udhibiti wa wadudu na magonjwa na namna bora ya kuandaa shamba langu.

Naye Afisa Ugani Elina Dastan kutoka Kilosa anaeleza kuwa anaona fahari kwa Taifa la Tanzania kupitia watafiti wake kuzidi kubuni teknolojia mpya kwa ustawi wa sekta ya kilimo nchini.

"Ugunduzi wa teknolojia za aina zote hizi za mbegu bora za korosho kutoka Tari ni fursa kubwa kwa wakulima na watanzania kwa ujumla." alisema Dastan.

Aidha, kutokana na hamasa iliyotawala wakati mafunzo yakiendelea, wadau hao wa zao la korosho walitaka kufahamu kwa kina ni aina ipi ya mbegu za korosho ambazo ni bora zaidi na zinazaa kwa wingi kama mkulima atahitaji kupata mavuno zaidi?.

Lingine lililojitokeza kwenye majadiliano ni je mbegu za zao hilo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo zinachukua muda gani hadi kuanza kuvunwa korosho yake sanjari na umakini wa palizi yake?

Na washiriki wa mafunzo hayo walitaka kufahamishwa endapo wanataka mbegu za Tari kwa haraka watazipataje na kwa utaratibu gani?.

Na zaidi wakionesha mwamko mkubwa walitaka kujua uhakika wa mwenendo wa soko kwa sasa...huku wale wengine waliopatiwa mbegu na Serikali huko nyuma wakitaka kuhakikishiwa ubora na uhalali wa mbegu hizo.

Akijibu maswali hayo Mratibu wa zao hilo kitaifa, Dkt Geradina Mzena alisema mbegu zote zilizogunduliwa na kufanyiwa utafiti na Serikali kupitia taasisi hiyo zina ubora na zinafaa kwa matumizi ya mkulima katika kupata tija inayostahili.

Huku Mtafiti kutoka Kituo cha Tari Naliendele Mtwara, Kasiga Ngiha akibainisha kuwa mbegu za korosho zinazozalishwa na kituo hicho huchukua kati ya miaka miwili mpaka mitatu kabla ya kukomaa na korosho yake kuanza kuvunwa.

Ngiha alisema mkulima anapaswa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha zao hilo ili kuleta tija na ustawi, na anapofikia wakati wa kupalilia hupaswa kuwa makini kwa kuhakikisha jembe analotumia lisizame zaidi ya sentimeta 20 kinyume chake anaweza kujikuta akikata mizizi ya mkorosho inayoota kwa kwenda chini na ile inayotambaa.

Akifafanua utaratibu wa kupata mbegu hizo hususan kwa wakulima wa mkoa wa Morogoro, Dkt  Mzena alisema mkulima yeyote anayehitaji mbegu hizo awasiliane na Bwana Shamba aliye karibu naye, na yeye atawasiliana na Tari Naliendele ili kupatiwa huduma hiyo.

Aidha kwa wakazi wa mkoa wa Morogoro wanaweza kutumia kituo cha mauzo ya mbegu cha Tari kilichopo Bagamoyo maarufu 'Cash Development Centre (CDC)'

Akifafanua kuhusu uhakika wa soko la korosho Mzena aliwahakikishia wakulima kuwa zao hilo kwa miaka yote limeendelea kuwa ni 'dhahabu ya kijani' na soko lake halijawahi kuyumba.

Alisema zao hilo linauzwa kwa mfumo kamili unaosimamiwa hatua kwa hatua yaani mfumo wa stakabadhi ghalani sambamba na mkulima wa zao hilo kuendelea kuwa na fursa lukuki za kukopesheka kupitia taasisi za fedha.

Na kuhusu hoja iliyoibuliwa juu ya zile mbegu zilizotolewa na Serikali huko nyuma kipitia mabwana shamba alisema mbegu hizo zipo salama na zinafaa kwa matumizi.

Kwa upande wake Afisa Kilimo na Mratibu wa Zao la Korosho mkoani hapa Isabella Chilumba alisema azma ya mkoa huo ni kuzalisha tani 500 za korosho ifikapo 2023, huku msimu ujao 2020/21 wakitarajia kuzalisha tani 300 ya zao hilo.

Hata hivyo Chilumba alibainisha hatua kwa hatua maendeleo kadhaa ya ongezeko la uzalishaji wa zao la korosho kwa misimu 3 iliyopita, ambapo mwaka 2017/18 mkoa ulipata tani 63, na 2018/19 ulipata tani 155, mwaka 2019/20 kiwango hicho kiliongezeka na kufikia tani 181.5, huku shabaha ya taifa ni kufikia tani milioni 1  ifikapo 2023.

"Naamini kwa mafunzo haya yanayotolewa  na taasisi ya utafiti wa  kilimo, pamoja na stratejia zingine tulizonazo kama mkoa yatachochea kwa kiasi kikubwa kasi ya ongezeko la uzalishaji kwa tija na ubora." alisema Chilumba