Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally akifungua Kikao cha siku mbili cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Kamati za Utekelezaji za Jumuiya za Chama - UVCCM, UWT NA WAZAZI ukumbi wa
White House jijini Dodoma
Sunday, November 29, 2020
DKT BASHIRU AFUNGUA KIKAO CHA SIKU MBILI CHA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA CCM NA KAMATI ZA UTEKELEZAJI ZA JUMUIYA ZA CHAMA JIJINI DODOMA
Friday, November 27, 2020
WAKULIMA WATAKIWA KUCHUKUA MIKOPO YA PEMBEJEO
Washiriki wa kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya NMB.
Wakulima wa mkoa wa Katavi wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na taasisi za kifedha katika kuchukua mikopo ya pembejeo ili kuinua kuwawezesha kufanya kilimo biashara na kukuza pato lao
Rai hiyo imetolewa na meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mpanda – Alex Massawe wakati akifungua mkutano maalum na wakulima na wafanyabishara wa mkoa huo.
Massawe amesema Benki ya NMB imekuwa ikikutana na wakulima wa maeneo tofauti kwa lengo la kutoa elimu ya kilimo biashara ambayo itamsaidia mkulima kuleta tija katika kilimo.
Akizungumzia mikopo hiyo ya pembejeo, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kilimo Biashara Wogofya Mfalamagoha amesema NMB inatoa mikopo ya pembejeo za aina tofauti kwa wakulima ambapo rejesho lake ni mara moja tu kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu.
Aidha Mwakilishi kutoka NMB foundation – Rogers Shipela amethibitisha kuwa taasisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima
“Taasisi ya NMB foundation imeundwa kwa lengo la kutoa mafunzo ya ujasiriamali ambapo mkulima ataweza kuuza mazao yake kwa bei itakayomnufaisha pamoja na hilo tunatoa elimu ya masoko ambayo inatolewa ili mkulima aweze kuuza mazao yake kwa ufanisi “alisema
OFISI YA BUNGE YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA BUNGE


Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akiwasilisha mada juu ya ‘Mambo Muhimu ya Kuzingatiwa na Waandishi wa Habari za Bunge’ kwenye mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Waandishi wa habari za Bunge wakifuatilia kwa makini mada zilizowasilishwa kwenye Mafunzo ya Waandishi hao yaliyofanyika kwenye hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka Global TV, Ndg. Mohamed Zengwa akichangia jambo kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).

Mwandishi wa habari za Bunge kutoka gazeti la Mwananchi, Ndg. Sharon Sauwa akiuliza shwari kwa Mtoa Mada (hayuko pichani) kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka gazeti la Uhuru, Ndg. Mussa Yusuph akiuliza shwari kwa Mtoa Mada (hayuko pichani) kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).

Mwandishi wa habari za Bunge kutoka Star TV, Ndg. Mozes Blaya akichangia jambo kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).
MADIWANI 31 KARAGWE WAAPA, UCHAGUZI VIONGOZI WA HALMASHAURI UMEMALIZIKA.

Madiwani wateule 31 wa wilaya
ya Karagwe wakila kiapo kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao katika
mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambao ni mahsusi kwa ajiri ya viapo,
kuchagua viongozi wa halmashauri na uundaji wa kamati mbalimbali za
halmashauri baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo
Oktoba 28,2020, kiapo hicho kimetolewa na Hakimu msaidizi wa mahakama ya
wilaya ya Karagwe Bi. V. M Mushi. Leo, Novemba 26,2020(Picha na Eliud
Rwechungura)
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya karagwe na Diwani wa kata ya Nyaishozi, Mhe.
Wallace Mrokozi Mashanda akiomba kura za ndio za kuchaguliwa kuwa
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe katika mkutano wa kwanza
wa Halmashauri ambapo amechaguliwa kwa kura zote 32 za ndio zilizopigwa
na Madiwani na Mbunge wa jimbo la karagwe. Leo, Novemba 26,2020(Picha na
Eliud Rwechungura)
Makamu Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya karagwe na Diwani wa kata ya Rugera, Mhe. Dawson
Paul Byamanyirwohi akiomba kura za ndio za kuchaguliwa kuwa makamu
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe katika mkutano wa kwanza
wa Halmashauri ambapo amechaguliwa kwa kura zote 32 za ndio zilizopigwa
na Madiwani na Mbunge wa jimbo la karagwe. Leo, Novemba 26,2020(Picha na
Eliud Rwechungura)
Mbunge
wa jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa akiongea na madiwani na
kuwasilisha vipaumbele vya utekelezaji wa maendeleo kwa madiwani katika
mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambao ni mahsusi kwa ajiri ya viapo kwa
madiwani, kuchagua viongozi wa halmashauri na uundaji wa kamati
mbalimbali. Leo, Novemba 26,2020(Picha na Eliud Rwechungura).
Madiwani wateule 31 wa wilaya ya Karagwe wamekula kiapo kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao katika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambao ni mahsusi kwa ajiri ya viapo na kuchagua viongozi wa halmashauri na uundaji wa kamati mbalimbali za halmashauri baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo Oktoba 28,2020, kiapo hicho kimetolewa na Hakimu mkuu wa wilaya ya Karagwe Bi. V. M Mushi
Madiwani walioapishwa ni kama ifuatavyo; Mhe. Ladislaus Kamuhangire, Diwani kata ya Ihanda, Mhe. Wallace Mahanda, Diwani kata ya Nyaishozi, Mhe.Shadrack Ntimba, Diwani kata ya Ndama, Mhe.Dawson Byamanyirwohi, Diwani kata ya Rugera, Mhe.Adrian Kobushoke, Diwani kata ya Rugu, Mhe.Charles Bechumila, Diwani kata ya Nyakahanga, Mhe.Magnus Cheusi, Diwani kata ya Kibondo, Mhe.Chrian Pastory, Diwani kata ya Igurwa, Mhe.Thomas Rwentabaza, Diwani kata ya Nyabiyonza, Mhe.Mugisha Mathias, Diwani kata ya Bugene, Mhe.Levina Kibogoyo, Diwani kata ya Ihembe, Mhe. Anord Rwenseleka, Diwani kata ya Chonyonyo, Mhe.Xavery Buguzi, Diwani kata ya Nyakakika, Mhe.Justine Fidelis, Diwani kata ya Nyakabanga, Mhe.Rwamuhangi Mugasha, Diwani kata ya Kihanga, Mhe.Fidel Belebe, Diwani kata ya Kamagambo, Mhe. Mzakiru Mussa, Diwani kata ya Bweranyange, Mhe. Valensi Kasumuni, Diwani kata ya Nyakasimbi, Mhe.Longino Rwenduru, Diwani kata ya Chanika, Mhe. Evarister Sylvester, Diwani kata ya Kiruruma, Mhe.Tayebwa Murishid, Diwani kata ya Kituntu, Mhe. Frolian Rwamafa, Diwani kata ya Kanoni, Mhe.Germanus Byabusha, Diwani kata ya Kayanga, Mhe. Jane Bilaro, Diwani viti maalum kata ya Nyaishozi, Mhe.Prisca Busenene, Diwani viti maalum kata ya Kibondo, Mhe.Genegeva Busenene, Diwani viti maalum kata ya Kituntu, Mhe. Anitha Richard, Diwani viti maalum kata ya Nyaishozi, Mhe.Jovitha Kombe, Diwani viti maalum kata ya Nyabiyonza, Mhe.Edina Mugashe , Diwani viti maalum kata ya Chanika, Mhe.Siima Ezekiel, Diwani viti maalum kata ya Ihembe, Mhe. Joyce Aenda, Diwani viti maalum kata ya Kayanga.
Kulingana na shughuli katika mkutano wa kwanza wa Halmashauri ambao ni mahsusi kwa ajiri ya kuchagua viongozi wa halmashauri, Mwenyekiti wa kikao na Katibu tawala wa wilaya ya Karagwe Ndg. Innocent Nsena ameongoza uchaguzi wa kuwachagua Mwenyekiti wa halmashauri na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya karagwe ambapo Diwani wa kata ya Nyaishozi, Mhe. Wallace Mrokozi Mashanda amechanguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya karagwe kama mgombea pekee kwa kura zote 32 za ndio, pia amechaguliwa Diwani wa kata ya Rugera, Mhe.Dawson Paul Byamanyirwohi kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe kama mgombea pekee kwa kura zote 32 za ndio zilizopigwa na madiwani na Mbunge wa jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa.
Aidha, Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa amepata nafasi ya kuongea katika mkutano huo na ameaanza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa ushindi wa kishindo alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni, pia amaekishukru Chama Cha Mapinduzi na Madiwani wote kwa kuamini na wanannchi na kuwatuma kuwawakilisha katika baraza la madiwani, Samabamaba na hao amempngeza msimamizi wa uchaguzi na mkurugenzi wa wilaya ya Karagwe kwa kusimamia uchaguzi ulioisha amabao umekuwa huru na wa haki ambao umepelekea Chama Cha Mapinduzi kushinda viti vya udiwani 22 kati ya 23 kwa wilaya ya Karagwe.
Sambamba na hayo Bashungwa amepata kuwasilisha vipaumbele vya maendeleo kwa madiwani ambavyo vitafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha ahadi walizozitoa katka kampeni zinatekelezwa kwa haraka na ndani ya muda mfupi na kuhakikisha ilani ya Chama Cha Mapinfuzi ya 2020 -2025 inatekelezwa kwa asilimia 100 bila kujali kata yenye diwani kutoka upinzani.
Wednesday, November 25, 2020
MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI YAZINDULIWA KITAIFA KILIMANJARO
Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yamezinduliwa kitaifa mkoani Kilimanjaro na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira na kusema kuwa lengo la maadhimisho haya ni sehemu ya kuwakumbuka wapendwa wetu waliotangulia mbele za haki kwa sababu ya ugonjwa wa UKIMWI.
Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho hayo Dkt Anna Mghira amesema kuwa kuanzia leo hadi Disemba mosi huduma za afya mbali mbali zitakuwa zinatolewa bila malipo katika viwanja vya Mandela kata ya Pasua manispaa ya Moshi.
Amewahimiza wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani kutochesea fursa walioipata kwani afya ni uhai, ameongeza kuwa mkoa wetu wa Kilimanjaro umepata fursa ya kuwa mwenyeji katika maadhimisho ya mwaka huu ambayo yanabebwa na kauli mbiu isemayo “Mshikamano wa Kimataifa- Tuwajibike kwa Pamoja. “nitafurahi kuona uwanja huu unajaa kila siku kwa ajili ya kupata huduma na ushauri wa kiafya unaotolewa hapa’ alisema Anna Mghira.
Uzinduzi huo ulitanguliwa na matembezi ya hisani kwa ajili ya kutangaza na kuhamasisha uchangiaji wa Mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI-(AIDS TRUST FUND)
Akizungumzia umuhimu wa Mfuko wa udhamini wa Kudhibiti UKIMWI (ATF)alisema kuwa Mfuko huu ni muhimu katika kukabiliana na upungufu wa rasilimali za udhibiti UKIMWI pamoja na kupunguza utegemezi kwa wahisani, nawaomba wananchi wenzangu tuchangie mfuko huu kupitia namba ya airtel money 0684 90 90 90 uchangiaji huu uwe endelevu tushikamane tuwajibike kwa pamoja.
Amefafanua kuwa takwimu zinaonyesha kuwa vijana wenye umri wa miaka 15-24 ndio wanaochangia asilimia 40 ya maambukizi mapya, hivyo kupitia maadhimisho haya vijana wataweza kupata elimu sahihi na njia za kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya VVU kupitia kijiji cha vijana ambacho kitakuwepo kwenye uwanja wa maadhimisho.
Aidha kutakuwa na mdahalo wa wanavyuo wenye lengo la kubadilishana uzoefu wa namna ya kujikinga na maabmukizi mapya ya VVU katika mazingira ya vyuoni na nje ya vyuo ambalo litawahusisha vijana.
Ameongeza kuwa Kutakuwa na kongamano kubwa la kisayansi litakalohusu masuala ya UKIMWI litakalofanyika kwa muda wa siku mbili Novemba 26-27 ambapo katika kongamano hilo wataalamu watajadili mafanikio, changamoto na namna ya kukabiliana na changamoto hizo katika kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.
Amezitaja huduma zinazopatikana uwanjani hapo bila malipo kuwa ni pamoja na upimaji wa hiari VVU,uchunguzi wa kifua kikuu, kisukari, shinikizo la damu, saratani ya shingo ya kizazi na uwiano wa uzito na urefu.
Amesisitiza kuwa hamasa ya upimaji wa hiari VVU inawalenga watanzania wote kutambua hali zao za maambukizi ya VVU, hususani vijana wenye umri wa miaka 15-24 na watu wa makundi maalum walio kwenye hatari zaidi ya kuambukiza au kuambukizwa VVU wakiwemo wanaojihusisha na biashara ya ngono na majidunga.
“Natoa msisitizo kwa wanaume kujitokeza kwa wingi katika kupima ili kujua hali za maambukizi kwa sababu takwimu za upimaji wa kawaida zinaonyesha idadi ndogo ya 45% ya wanaume hujitokeza kupima VVU, kwa sababu wanaume wengi hutafsiri majibu ya vipimo vya wenzi wao kwamba ndio majibu yao badala ya wao kwenda kupima”.
Nitoe rai kwa wananchi kujitokeza katika kupima ambapo watakaogundulika kuwa na VVU watapata ushauri nasaha na kuanza kutumia dawa za ARV mapema ambapo kutumia dawa za ARV huwezesha kufubaza na kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa nyemelezi,wajawazito kupunguza hatari ya kuambukiza watoto pamoja na kupunguza hatari ya kuambukiza VVU kwa wenzi wa ngono.
Aidha amezungumzia kiwango cha maambukizi ya VVU katika mkoa wa Kilimanjaro kuwa yameendelea kupungua kutoka aslimia 7.3 mwaka 2004 hadi asilimia 2.6 mwaka 2017, kiwango hiki kipo chini ya wastani wa maambukizi ya kitaifa ambacho ni asilimia 4.8
Japokuwa kiwango cha maambukizi kwa mkoa wetu wa Kilimanjaro kipo chini ya wastani wa Kitaifa haimaanishi kuwa tuko salama hivyo kwa pamoja tunapaswa kuongeza juhudi ili tufikie lengo la maambukizi sifuri ifikapo mwaka 2030.
Kwa mujibu wa utafiti huu kiwango cha kufubaa kwa VVU kwa mkoa wa Kilimanjaro ni asiimia 67 dhidi ya asilimia 52 ya kitaifa hivyo matokeo haya yameuweka mkoa wa Kilimanjaro kuwa wa pili kitaifa kwa kuwa na kiwango cha juu cha kufubaa kwa VVU ukitanguliwa na mkoa wa Lindi.
Changamoto kubwa kwa mkoa wa Kilimanjaro katika kudhibiti maambukizi mapya ya VVU ni huduma ya tiba na matunzo ambapo baadhi ya WAVIU kutokuwa na ufuasi mzuri wa dawa za ARV pindi afya zao zinapoonekana kuimarika.
Natoa rai kwa WAVIU wote waliokwisha anza kutumia dawa za ARV, wazingatie ufuasi mzuri wa dawa,nawaagiza wadau wote mhakikishe mnawashirikisha vyema WAVIU hasa waliojiweka wazi juu ya hali zao katika kuhamasisha WAVIU wasiokuwa na ufuasi mzuri wa matumizi ya dawa za kufubaza (ARV).
Ametoa shukrani kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia TACAIDS kuupa mkoa wetu heshima ya kuwa mwenyeji wa wiki ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani kufanyikia kitaifa mkoani Kilimanjaro.
Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau pamoja na wafadhili wa ndani na nje ya katika Mwitikio wa VVU na UKIMWI na kuhakikisha dawa zinaendelea kuwepo bila kukosekana.
Pia amewashukuru wadau wote wa maendeleo kwa misaada yao ya kifedha na kitaalamu katika Mwitikio wa VVU na UKIMWI mkoani zinazoendelea kutolewa katika mkoa wa Kilimanjaro.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la watu wanaoishi VVU (NACOPHA) ameishukuru serikali kwa kuendelea kutambua haki za watu wanaoishi na VVU ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwapa huduma stahiki,na uhakika wa dawa za kufubaza VVU(ARV)ni hatua kubwa katika kuhakikisha tunadhibiti maambukizi mapya na kufikia zero mwaka 2030.
Mkurungezi Mtendaji wa TACAIDS Dr Leonard Maboko ameushukuru Mkoa wa Kilimanjaro kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha maandalizi ya maadhimisho haya yanafanikiwa.
Amewaomba wadau kuendelea kuonesha ushirikiano katika kuhakikisha maadhimisho haya yanaleta chachu ya mabadiliko katika kudhibiti maambukizi mapya ya VVU pamoja na kutoa elimu ya VVU na UKIMWI kwa wananchi.
Kilele cha maadhimisho haya yatahitimishwa Disemba mosi, ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.
Imetolewa na
Kitengo cha mawasiliano Serikalini-TACAIDS
AFISA VIJANA SINGIDA AWATAKA VIJANA KUTUMIA FURSA YA MSIMU HUU WA MVUA KWA KILIMO
Akizungumza mkoani hapa jana, Ndahani alisema anaamini kijana yeyote atakayethubutu kujiingiza katika kilimo kamwe hatajutia kutokana na faida kubwa atakayoipata.
"Nawahamasisha vijana wenzangu tujitokeze tukalime, tusiiache mvua hii ikapita bure. Kwa wasio na mashamba wasisite kwenda kukodi...shamba la kukodisha gharama yake ni wastani wa kati ya shilingi elfu 25 na 30 kwa ekari moja," alisema.
Alisema wakati serikali ikipambana kuhamasisha mageuzi ya kilimo ni jukumu la vijana kuhakikisha wanaunga mkono juhudi hizo kwa kutambua kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa.
Ndahani alisema takribani asilimia 60 za malighafi ya viwanda vilivyopo nchini hutegemea kilimo hivyo ni jukumu la vijana kuhakikisha wanakwenda na kasi ya mheshimiwa Rais John Magufuli katika kulifanya taifa hili kuendelea kustawi kiuchumi.
"Niwaombe sana tusiwaachie wazee na wanawake peke yao bali vijana tuingie rasmi shambani tusiache mvua hizi zikapita hivi hivi,"alisema afisa huyo wa vijana.
Alisisitiza mathalani kwa vijana wa mkoa wa singida, wana kila sababu ya kuchangamkia fursa ya kilimo chenye tija kutokana na uwepo wa viwanda vingi vinavyohitaji malighafi, hususan zao la alizeti ambalo ndio zao kuu mkoani humo.
Pia aliwakumbusha vijana kuwa mbali ya alizeti tayari serikali imekwishafungua dirisha lingine kwa kilimo cha korosho kwenye mikoa yote ya Kanda ya Kati ikiwemo Singida, zao ambalo lina usalama zaidi na soko la uhakika ndani na nje ya nchi...na kwamba wasichelewe kuchangamkia fursa hiyo ili kuondokana na umasikini na kuinua kipato.
Ndahani ambaye ameshawahi kushiriki kwenye timu maalumu ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru miaka ya hivi karibuni, alisema anaamini misingi bora ya taifa lolote lenye amani, utulivu na usalama hutokana na watu wake hususan vijana kujikita ipasavyo katika uwajibikaji kwenye nyanja mbalimbali-ikiwemo shughuli za kilimo.
VIJIJI VYA LIWALE MKOANI LINDI VYANEEMEKA NA UHIFADHI WA MISTU
Na Calvin Gwabara, Liwale.
Zaidi ya shilingi milioni 957 zimepatikana kwenye vijiji kutokana sekta ya misitu katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi na hivyo kuchangia katika kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya na maji.
Hayo yamebainishwa na KatibuTawala wa Wilaya hiyo, Rajabu Kambangwa wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mchango wa sekta ya misitu na ushiriki wa wilaya hiyo kwenye uhifadhi shirikishi wa misitu ya vijiji.
Alisema kuwa wilaya ya Liwale misitu ni chanzo kikubwa cha mapato ya wilaya kwani katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 iliingizia serikali kiasi cha shilingi bilioni 2.6 ikifuatiwa na sekta ya kilimo na hivyo kuifanya sekta ya misitu kuwa sekta muhimu kwauchumi.
” Sisi kama wilaya tunanufaika sana na uwepo wa rasilimali hizi kwa hiyo tunafarijika sana ujio wa miradi kama huu ya Uhifadhi shirikishi wa misitu kwani inasaidia kuwajengea uwezo wananchi kwenye vijiji vyetu kuona umuhimu wa misitu na uhifadhi wake kwa maendeleo endelevu lakini kubwa zaidi kuona misitusi ya serikali bali ni mali yao” alisema Kambangwa.
Katibu Tawala huyo alisema kwenye Kijiji cha Likombola pekee kiliingiza kiasi cha shilingi milioni 253 huku Kijiji cha Mtawatawa wakiingiza kiasi cha shilingi milioni 122 ambazo zimetumika kufanya shunguli mbalimbali za maendeleo kwenye vijiji hivyo ikiwemo kujenga vyumba vya madarasa, Zahanati, Nyumba ya Mtendaji wa Kijiji Pamoja naTrekta la Kijiji ambalo linawasaidia kwenye kilimo kwa kukodishiana kwa gharama za chini na kwa wakati.
Alisema pamoja na mafanikio hayo makubwa lakini swala la uhifadhi bado linahitaji elimu kwa jamii maana Wananchi wasipoona faida za moja kwa moja kwenye vijiji vyao hawawezi kuitunza wala kuilinda na hivyo kusababisha misitu kupotea wakidhani ni mali ya Serikali.
Kwa upande wake Afisa Sera na Majadiliano wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA)Elida Fundi alisema kuwa vijiji vinafanyakazi kubwa na nzuri katika kuhifadhi misitu ya vijiji na hii inatokana na elimu na motisha wanayoipata kwenye vijiji vyao baada ya kuvuna misitu hiyo kwa uendelevu.
Alisema MJUMITA kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo na misitu wataendelea kushiriki kikamilifu kwenye kuzisaidia Halmashauri na vijiji katika awamu hii ya tatu ya mradi kuweka mipango bora yamatumizi ya ardhi na utengaji wa maeneo ya misitu ya hifadhi za vijiji ili itunzwe na kuvunwa kwa njia endelevu ambazo zitatunza misitu hiyo.
Kwa upande wake Afisa Misitu wa wilaya hiyo, Nassoro Ali Mzui alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo kwenye uhifadhi wa misitu hiyo ni vitendea kazi hasa vyombo vya usafiri kama pikipiki na zana zingine kwani misitu mingine inaukubwa wa zaidi ya hekta elfu 13 hivyo kuwawia vigumu kufanya doria na kuizunguka kwa miguu.
Alisema kwa kuwa vijiji vinachangia asilimia kumi ya mapato yatokanayo namisitu kwenda kwenye halmashauri wamekuwa wakifanya doria za pamoja na wanavijiji na kamati zao za maliasili za kijiji pamoja na maafisa wa maliasili na askari ili kusaidia kuongeza nguvu na kurahisha zoezi la ulinzi kwenye misitu hiyo.
PROF OLE GABRIEL AWAFUNDA WANAFUNZI WA CHUO CHA HOMBOLO
Prof Gabriel ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada iliyohusu nafasi ya viongozi wa kuchaguliwa katika kuleta maendeleo kwa jamii anayoiongoza kwenye hafla ya kuwatunuku zawadi wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao na wafanyakazi bora wa chuo cha Hombolo iliyofanyika katika chuo hicho kilichopo Dodoma Novemba 25, 2020.
Amesema katika kipindi hiki ambacho nchi ya Tanzania imeingia katika uchumi wa kati viongozi wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba wanakidhi matarajio ya Watanzania.
Prof Gabriel ameongeza kuwa nchi nyingi na taasisi zimekuwa zikikwama kufikia malengo tarajiwa kwa sababu ya kukosa usimamizi mzuri.
“ Kuwa na rasilimali ni jambo moja, lakini kusimamia rasilimali hizo ni jambo la muhimu zaidi, taasisi nyingi zimekwama kwa kushindwa kusimamia rasilimali zake ikiwemo rasilimali watu, rasilimali fedha na rasilimali miundombinu,” amesema Prof. Gabriel.
Kwa mantiki hiyo ameupongeza Uongozi wa Chuo cha Hombolo kwa kusimamia agenda ya uongozi huku akisema kuwa elimu hiyo wanayoitoa kwa wanafunzi wa chuo hicho itawasaidia wanafunzi hapo mbeleni watakapokuwa viongozi.
Ameendelea kusema kuwa kiongozi yeyote wa kuchaguliwa au kuteuliwa ili awe kiongozi bora ni muhimu kuzingatia mambo matatu ambayo ni kufahamu hasa anaowaongoza wana mahitaji gani pia Kiongozi atambue kuwa hatakumbukwa kwa cheo chake bali kwa mchango wake kwa jamii ile anayoiongoza na tatu, awe mtu anayewashirikisha wale anaowaongoza katika kutatua changamoto zao.
“Washirikishe wale unaowaongoza na ndipo utakapoweza kutatua changamoto, kiongozi mzuri ni yule anayeziona changamoto na kuzibadilisha kuwa fursa, na kwa kufanya hivyo ndipo utaweza kukidhi matarajio ya wale unaowaongoza,” Amesisitiza Prof. Gabriel.
Katika hafla hiyo ya 12 ya chuo hicho, Prof Ole Gabriel alikuwa Mtoa mada maalum na aliwasilisha mada hiyo ya nafasi ya viongozi wa kuchaguliwa na wakuteuliwa katika kuleta maendeleo kwa jamii ili kuwakumbusha wajibu wao mkubwa kwa jamii.
Tuesday, November 24, 2020
KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AWATAKA WALIOJINUFAISHA MALI ZA USHIRIKA KUZIRUDISHA
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya amewataka wale wote waliojinufaisha na mali za vyama vya ushirika hapa Nchini kurudisha Mali zote walizochukua kinyume na utaratibu akionya kuwa kwa kushindwa kufanya hivyo serikali itawafuata na hizo mali watazirudisha kama ambavyo baadhi yao wameanza kufanya.
Aidha Kusaya ameongeza kuwa mipango ya kufanya mabadiliko ya Uongozi katika Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) yako mbioni akisema kuwa mabadiliko hayo ni suala la wakati kwani mipango ya Serikali ni kuhakikisha Vyama vya Ushirika vinajiendesha kibiashara na kwa faida.
Katibu Mkuu Gerald Kusaya amesema hayo jana wakati Kamati ya Maalum ya iliyoundwa na Waziri Mkuu kufuatilia Mali za SHIRECU ilipokabidhi mali nane za SHIRECU zenye thamani ya Bilioni 3.3 ikiwemo viwanja na Ghara la kuifadhia mizigo liliko Kurasini pamoja na nyumba moja iliyoko Ilala Jijini Dar es Salaam.
Hati za Mali za Chama Cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU ziliwasilishwa kwake na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Asangye Bangu ambaye alisema kamati yake tayari imewezeza kurejesha Mali nane ambazo zinajumuisha ardhi, mitambo na nyumba zilizo kuwa nje ya SHIRECU na sasa zimerejeshwa katika Chama hicho.
Bangu amesema kuwa kipindi cha mwaka 2000hadi 2005 baadhi ya viwanja ambavyo vilikuwa mali ya SHIRECU vilichukuliwa kwa njia za ujanja ujanja na baadhi ya Maafisa Ardhi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kujimilikisha wenyewe na vingine kuviuza na wamiliki viwanja hivyo kwa kuwa walisha viendendeleza walitoa viwanja vingine vinye ukubwa na thamani sawa na viwanja walivyochukua ambavyo Sasa ni mali ya SHIRECU.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alisema sasa SHIRECU inahitaji utaalam na utawala wa kuiwezesha kujiendesha kwa kuwa tayari ina mali nyingi akitaja Jengo la Ghorofa Tatu liloko Ilala na Ghala la liliko Kurasini Jijini Dare es Salaam ambalo pia lina sehemu yenye kiwanda cha kusindika Kahawa kama sehemu ya mali inayotosha kuendesha kibiashara Shirika hilo.
Aidha Telack ameongeza kuwa ni lazima SHIRECU ijiendeshe kutokana na mali zilizopo kwa kuwa sasa Shirika hilo halikopeshiki kutokana na kuwa na mzigo mkubwa wa madeni ambapo kwa sasa inadaiwa zaidi ya Bilioni 15 ukiachilia mbali madai ya watumishi.
Mali za Vyama vya Ushirika nchini zinarejeshwa kufuatia Agizo la Rais John Magufuli alilotoa Mwaka 2016 katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza kutaka wale wote waliochukua mali za Vyama vya Ushirika bila kufuata utaratibu kuzirejesha na baadae kuundwa Tume Maalum ya kufutilia mali hizo Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Tanzania kufuatia Agizo hilo.
Monday, November 23, 2020
TBS YATEKETEZA VIPODOZI VYENYE VIAMBATA VYA SUMU VYA THAMANI ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 125
Picha ikionyesha namna uteketezaji ukiendelea eneo la dampo
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza vipodozi vyenye viambata sumu vya thamani ya Shilingi milioni 125 baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa kushitukiza kwenye maghala ya kuhifadhia vipodozi ambayo hayajasajiliwa.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mwishoni mwa wiki na TBS, Vipodozi hivyo vilivyopigwa marufuku vilikutwa katika maghala la kampuni ya Kimario Cosmetics hivi karibuni na wakaguzi wa TBS Jijinii Arusha na kukamatwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009 pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2019.
Vipodozi vikishushwa kwenye gari mbili Aina ya fuso
“Mmiliki wa ghala hilo Pamphil L. Kimario amelipa shilingi milioni 3.5 ikiwa ni gharama ya kuteketeza bidhaa hizo hatarishi kwa afya ya binadamu kwani zinapotumiwa huweza kusababisha madhara mbambali kwa mtumiaji”,Inasisitiza taarifa hiyo
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Baadhi wa Watanzania wamekuwa wakitumia vipodozi hivyo vyenye viambata vya sumu ambavyo vina kemikali ya Mercury na Hydoroquinone kwa lengo la kung’arisha ngozi zao na hata kubadili rangi ya ngozi hizo bila kujali madhara yatokanayo na bidhaa hizo.
Vipodozi vyenye kemikali ya Mercury kwa Mujibu ripoti ya Shirika la Afya Duniani(WHO) ya mwaka 2020, vikitumika kwa muda mrefu vinasababisha magonjwa ya figo, mapafu, ngozi, macho mfumo wa fahamu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na mfumo wa kinga ya mwili na kwa upande wa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali ya hydroquinone husababisha magonjwa ya kansa ya ngozi.
Aidha, Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sheria ya Fedha Na. 8 ya mwaka 2019 iliipa Mamlaka TBS ya kusimamia usajili wa bidhaa za chakula ,vipodozi , maghala ya kuhifadhia chakula na vipodozi pamoja na migahawa na mahoteli jukumu lillilokuwa likifanywa hapo awali na iliyokuwa Mamlaka ya Dawa Chakula na Vipodozi (TFDA).
Utekelezaji wa Sheria hiyo ya Fedha ulianza rasmi tangu Julai 2019, hivyo kuwalazimu wauzaji wazalishaji na wauzaji wa vipodozi kusajili bidhaa hizo pamoja na maghala ya kuhifadhia.
Na Mwandishi wetu- Arusha
Shirika pia limeteketeza bidhaa nyingine zisizofaa za vipodozi na vyakula zilizokamatwa katika kaguzi zilizofanyika nyakati tofauti katika maeneo mengine Arusha na nje ya Arusha katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2020.
TBS inaendelea na ukaguzi huu nchi nzima pamoja na kuwahimiza wazalishaji na wauzaji wa vipodozi kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu zilizopo kwa kusajili bidhaa hizo pamoja na maghala ili kuepuka usumbufu. Pia wauzaji wa vipodozi wanahimizwa kuwa na orodha ya bidhaa za vipodozi visivyoruhusiwa ambayo inapatikana katika tovuti ya Shirika www.tbs.go.tz
WAKULIMA WA TARIME KUPATA MBEGU NA MBOLEA KWA BEI ELEKEZI YA SERIKALI - KATIBU MKUU KUSAYA
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akisoma kibao kinachoonyesha aina ya kahawa inayovumilia ukame alipokagua shamba darasa la kituo cha utafiti wa kahawa Sirari (Nyamwaga) wilayani Tarime. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TACRI Dkt. Deusdedit Kilambo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya ( aliyevaa suti) akikagua shamba bora la kahawa na migomba Kituo cha Utafiti wa kahawa Sirari ( Nyamwaga) Tarime ambapo ameagiza wataalam wa mazao ya migomba na mihogo toka TARI Maruku na Ukirigulu wafike hapa Tarime na kutoa ushauri wa kutatua tatizo la ugonjwa wa migomba inayosababisha hasara kwa wakulima wetu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiwa kwenye mkutano wa hadhara na wakulima na wanachi wa kijiji cha Nyamwaga wilaya ya Tarime
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akitazama mti wa kahawa wenye umri wa mwaka mmoja ukiwa umezaa matunda ambao umepandwa na taasisi ya utafiti wa kahawa ( TACRI) Sirari kwa ajili ya shamba darasa kwa wakulima ikiwa ni mkakati wa serikali kufufua zao la kahawa wilayani Tarime.

…………………………………………………………………..
Wizara ya Kilimo imesema itahakikisha wakulima wa wilaya ya Tarime na mkoa wote wa Mara wanapata mbegu bora za mahindi na mbolea kwa bei elekezi ya serikali ili kudhibiti biashara ya magendo mpakani.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa (21.11.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alipozungumza na wakulima na wananchi wa kijiji cha Nyamwaga wilaya ya Tarime wakati alipokagua mashamba darasa ya kahawa,mihogo na migomba.
Kusaya alisema hayo kufuatia malalamiko ya wakulima wa Tarime kusema hawapati mbegu bora za mahindi na mbolea zinazozalishwa nchini hali inayowafanya wategemee bidhaa hizo toka nchini Kenya zinazoingizwa kinyemelea mpakani Sirari.
Akizungumzia suala la uhaba wa mbegu na mbolea Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhandisi Mtemi Msafiri alimweleza Katibu Mkuu huyo kuwa wakulima wanapata shida ya kupata pembejeo za serikali na kuwa Tarime hazifiki hali inayowafanya wakulima kushindwa kuzalisha kwa tija mazao hususan mahindi yanayotegemewa kwa chakula.
“Tuna shida kubwa ya mbegu bora za mahindi hapa Tarime na zinazopatikana zinauzwa bei kubwa mfano kilo mbili kwa shilingi 15,000 na nyingi zinatoka nje ya nchi “alisema Mhandisi Msafiri
Katibu Mkuu Kusaya aliwahakikishia wakulima hao kuwa wizara yake kupitia Wakala wa Mbegu (ASA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) utafikisha mbegu za mahindi na alizeti pia mbolea mkoani humo mapema kabla ya Desemba mwaka huu .
“Nimeagiza Mtendaji Mkuu wa ASA Dkt. Sophia Kashenge afike hapa Mara na ahakikishe mbegu bora za mahindi zinauzwa kwa bei elekezi ya serikali ili wakulima wengi wamudu na kutoendelea kuumizwa na wafanyabiashara. Mbegu hizi zitauzwa chini ya shilingi 10,000 “alisema Kusaya hatua iliyopokelewa kwa shangwe na wakulima.
Kusaya aliongeza kuwaeleza wakulima hao kuwa tayari ameelekeza mbolea iletwe mapema kabla ya Desemba na Malmaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) na kuwa iwafikie wakulima kwa bei elekezi ya serikali.
“Niwasihi wakulima wangu muwe na subira kabla ya Desemba mwaka huu TFRA wataleta mbolea hapa Tarime na mkoa wote wa Mara itakayouzwa kwa bei elekezi “alisisitiza Kusaya.
Akiwa kijijini Nyamwaga kwenye mkutano wa hadhara wakulima walieleza kuwa wanauziwa mbolea aina ya NPK mfuko wa kilo 50 kwa bei ya Shilingi 60,000 hadi 80,000 kwa inayotoka Kenya na ya Tanzania kwa Shilingi 80,000 hadi 100,000 hivyo kushindwa kumudu.
Katika hatua nyingine Kusaya aliwashauri wakulima wa wilaya ya Tarime pamoja na kulima mazao ya chakula wajikite pia kuzalisha mazao ya kahawa, chai na migomba yanayostawi vema kutokana na hali ya hewa nzuri na kuwa wizara yake itatoa utaalam na pembejeo ikiwemo mbegu bora.
Kusaya aliongeza kuwahakikishia wakulima wa migomba na mihogo kuwa tatizo la wadudu wasumbufu litapatiwa suluhisho mapema kupitia taasisi ya Utafiti wa kilimo (TARI) ambapo watafiti watafika Tarime na Butiama kukutana na maafisa ugani na wakulima
“Niwatoe hofu wakulima wa mihogo na migomba kuhusu tatizo la ugonjwa unaoharibu mazao hayo, kuwa wiki ijayo wataalam toka TARI Maruku (Bukoba) na wale wa TARI Ukirigulu (Mwanza) watafika hapa Tarime kutatua changamoto za magonjwa haya kwa kuwafundisha maafisa ugani namna ya kukabiliana na wadudu hawa” aliahidi Katibu Mkuu Kusaya.
Ili kuhakikisha wakulima wanapata elimu na teknolojia ya kuwasadia kutatua changamoto za kilimo, Katibu Mkuu huyo wa kilimo alitoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini kuacha kuwatumia maafisa ugani kwenye kazi za utawala ikiwemo kazi ya utendaji wa vijiji na kata.
“Hawa maafisa ugani wameajiliwa kwenda shambani hivyo wasipangiwe kukaimu utendaji wa vijiji au kat. Tunataka kila kijiji kiwe na afisa ugani kuwasaidia wakulima kutatua changamoto za mazao yao” alisema Kusaya.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Kilimo amehitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Mara kwa kutembelea wilaya za Musoma, Butiama na Tarime ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na wakulima pamoja na kukagua shughuli za kilimo mashambani.





























